Kushoto
ni Mkuu wa vipindi vya Radio 5 Mathew Philip na Ashura Mohamed wakiwa
katika picha ya pamoja na wanafunzi wa sekondari walioshiriki katika
maadhimisho hayo ya Radio duniani.
Akizungumza na waandishi wahabari hivi karibuni Mkuu wa
vipindi wa Radio 5 Bw.Mathew Philip alisema maadhimisho hayo
yalidhaminiwa na kituo hicho pamoja na Farm Radio, ikiwa ni kuhadhimisha
siku ya Radio duniani ambapo ilifanyika tarehe 13/2/2015 jijini Arusha.
Bw.Mathew alisema kuwa wakulima
pamoja navijana wa kanda ya kaskazini wakiwemo wanafunzi wa shule za
sekondari,walipatana fursa ya kutembelea kituo hicho na kuona namna
inavyoendesha vipindi vyake ikiwemo kipindi cha afya ya akili kwa
vijana(Positive mood),Fahari yangu kipindi kinacho wagusa wakulima
Alitoa wito kwa Radio zingine
kuwa na utaratibu wa kuhadhimisha siku hiyo kwa kuwa itasaidia kuongeza
uaminifu mkubwa na wasikilizaji kwa ujumla
Kwa upande wake Mtaalamu wa
mnyororo wa dhamani kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya
kiserikali la Farm Radio Bw.Terevael Aremu alisema kuwa lengo la kufanya
hivyo ni kusisitiza jamii kusikiliza radio hasa vipindi vya elimishi
vinavyopatikana katika vituo vya radio hapa nchini na Afrika.
Aidha alisema kuwa Jamii hasa
wakulima wakisikiliza radio watapata elimu na taarifa mbalimbali za kile
wanachokiitaji kwa wakati sahihi ikiwemo taarifa za hali ya hewa.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog).
Wakulima pamoja na vijana kanda
ya kaskazini wakiwa katika majadiliano mara baada ya kufanya ziara
katika kituo cha Radio 5 nakuona namna inavyoendesha vipindi vyake
katika maadhimisho siku ya radio duniani iliyofanyika 13/2/2015 jijini
Arusha.
Mkuu wa vipindi vya radio 5 Mathew Philip akiteta jambo na mkulima aliyefika katika maadhimisho hayo.
Mtaalamu wa mnyororo wa dhamani
kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya kiserikali la Farm
Radio Bw.Terevael Aremu akizungumza katika maadhimisho hayo
Wafanyakazi wa kituo cha radio 5 wakiwa wanafurahia jambo.
Watangazaji mahiri wa kituo cha radio 5 wakiwa katika pozi Semio Sonyo kushoto,katikati Mwangaza Jumanne na Linus Kilembu
Kulia Hilda Kinabo na Semio Sonyo watangazaji wa Radio 5
Mkuu wa vipindi vya radio 5 Mathew Philip pamoja na Mtangazaji Linus Kilembu wakiwa katika majadiliano
Mtangazaji mahiri wa kituo cha Radio 5 Tonnie Kaisoi katika pozi
Kituo cha Radio 5 chenao yake makuu jijini Arusha
imeadhimisha siku ya Radio duniani kwa kuwakutanisha wakulima na vijana
kanda ya kaskazini ikiwa nikuhamasisha vijana kujieleza namna Radio
hiyo imesaidia katika kukuza uchumi,kijamii,kisiasa na kiutamaduni.
No comments:
Post a Comment