Monday, February 16, 2015

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yatoa mafunzo kwa wataalamu wake

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi imeendesha mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya stashahada ya ununuzi na ugavi. 

Mafunzo hayo yalifunguliwa jana, na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi, Bw, Aziz Kilonge, ambaye aliwaasa wataalam hao kuhakikisha kwamba wanasimamia wanafunzi kwa ukamilifu ili kuongeza ubora wa kazi za utafiti zinazofanywa. 

Aidha, alifafanua kuwa uzingatiaji wa maadili katika kufanya tafiti, ndio msingi na matakwa ya Bodi, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafanya tafiti na sio kuchukua kazi zilizofanywa na wanafunzi/watafiti wengine au kufanyiwa na watu wengine. Pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti, pia wanafunzi wanajengewa uwezo wa kuandika ripoti na hata kuwasilisha ripoti katika sehemu zao za kazi. 

Hivyo lengo kuu ni kuwejengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa taifa. Aliwakumbusha wasimamizi hao kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa kujiamini na kujieleza kwani ufaulu wa mwanafunzi, unategemea sana uwezo wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani huo mwanafunzi atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima uwezo wake.
1
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya PSPTB, Bw, Aziz Kilonge akifungua mafunzo ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwa kutoa mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya stashahada ya ununuzi na ugavi mafunzo hayo yamefanyika kaktika ukumbi baraza la Maaskofu TEC jijini Dar es salaam.
02Tesha Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Dr Clemence akizungumza katika mafunzo hayo mara baada ya kufunguliwa rasmi. 2Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr.Eli Tumsifu akitoa mafunzo kwa wataalamu hao wa usimzmizi wa Manunuzi na Ugavi 3Baadhi ya wataalamu wa Manunuzi na Ugavi wakifyuatilia mafunzo hayo. 4Wataalamu hao wakiandika mambo muhimu wakati wa mafunzo hayo.  9Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya PSPTB, Bw, Aziz Kilonge akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu hao mara baada ya kufungua rasmi mafunzo hayo.

No comments: