Waziri wa maji ,Jumanne Maghembe (wa kwanza kulia) akizungumza na wakandarasi wanaojenga bomba la maji la Mlandizi Kimara Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati alipotembelea miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na maji Taka (DAWASA), kwalengo la kupata tathimini ya mradi huo ulipofikia sasa.
Waziri wa maji Jumanne Mghembe (wa pili kulia) akiwa ameongozana na meneja mradi Pintu Dutta (watatu kulia) wakati akikagua maendeleo ya mradi wa kituo cha kusafisha maji cha ruvu juu .
Waziri wa Maji Jumanne Maghembe (wapili kulia) akioneshwa mchoro wa mradi wa bomba la maji mlandizi kimara linalopitia makongo juu na Mhandisi wa Mradi huo, Bw Severin Mkendala jinsi mabomba mradi wa mlandizi kimara yalipopita .
Gari aina ya Catterpilar la kampuni ya Megha Enginearing Infastructure Limited, likiwa linasafisha eneo ambalo linatakiwa kulazwa mabomba ya yanayotoka Mlandizi Kimara kwenda Ruvu JUU.
Kushoto ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Megha Engenearin Infastructure Limited Mural Mohan, akimweleza maendeleo ya mradi huo Waziri wa Maji Jumanne Maghembe,aliyekuwa katika ziara ya kutembelea miradi inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka.
Waziri wa Maji Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha ziara hiyo.
No comments:
Post a Comment