Wednesday, January 21, 2015

Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji yaridhishwa na miradi ya maji ya Kibiti, Ikwiriri

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu (kushoto) akimuongoza Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi aliyeambatana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada ya kuwasili ofisi za Mradi wa Maji Kibiti ulioko wilayani humo mkoani Pwani kabla ya kuukagua.Ukaguzi wa mradi huo ni sehemu ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara inayofanywa na wajumbe wa Kamati hiyo.
Meneja wa Mradi wa Maji Kibiti Mhandisi Juma Ndaro akitoa ufafanuzi kwa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, juu ya mradi huo wakati kamati ilioptembelea kukagua mraddi huo.
Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati Amina Makilagi akipanda ngazi za tanki la maji la mradi wa maji wa Kibiti wakati akikagua mradi huo, huku Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu na watendaji wengine wakishuhudia.
Mhandisi wa Maji mkoa wa Pwani Mhandisi Alphonce (kulia), akiwaeleza jambo baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiwa juu ya tanki la maji la mradi wa Kibiti.Kutoka kushoto ni Amina Makilagi (Mb) Kiongozi wa wajumbe, Meneja Mradi wa Ikwiriri Ladislaus Komba, Asaa Hamad (Mb),Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu, Abdallah Haji Ali (Mb).
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtawanya Kati Mwanaisha Mohamed akieleza hoja yake mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji walipotembelea mradi wa maji Kibiti.
Meneja wa Mradi wa Maji Ikwiriri Ladislaus Komba (aliyeshika jalada) akitoa ufafanuzi wa mradi huo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na watendaji wa wilaya ya Rufiji na wawakilishi wa Ikwiriri, baada ya kuwasili kwenye tanki la mradi huo.
Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi akinywa maji yaliyotoka kwenye kisima cha mradi wa maji Ikwiriri wilayani Rufuji mkoani Pwani, kwenye ziara ya kamati hiyo kukagua miradi ya maji katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Wawakilishi wa wananchi wa Ikwiriri na wataalamu wa Wizara ya Maji, wakiwa kwenye eneo la mtambo wa kusukumia maji wa mradi wa maji wa Ikwiriri, kukamilisha ziara ya kukagua miradi ya maji wa Ikwiriri. Picha zote na Hussein Makame, MAELEZO

No comments: