Wednesday, January 21, 2015

Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii yafurahishwa na miradi ya Vijana

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Mhe.Maabad S. Hoja akifafanua jambo wakati wa kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii walipofanya ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyopata mkopo kutoka Wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Bw. P. Kagimbo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia (MB) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad Mtanda.
Baadhi ya maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia taarifa fupi kuhusu Vikundi vilivyokopeshwa kupita Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyosomwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Manispaa hiyo jana.
Kushoto ni mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Dkt. Maua Daftari akifuatilia taarifa fupi kuhusu Vikundi vilivyokopeshwa kupita Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyosomwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Manispaa hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Said Mtanda akizungumza na wafanyakazi wa Manispaa ya Temeke kamati hiyo ilitofanya ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyonufaika na Mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika manispaa hiyo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Maabad S. Hoja na wamwisho kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw.P. Kagimbo
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Manedeleo ya Jamii, na wataalamu kuto Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia taarifa fupi ya maendeleo ya Temeke Youth Saccoss wakti wa ziara ya kamati hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Temeke Vijana Saccoss Bw. Swaka Abbas akisoma taarifa fupi ya maendeleo ya Saccoss yao mbele ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilifanya ziara ya kutembelea niradi ya inayoendeshwa na Vijana kupitia Vikundi vilivyopata mkopo kutoka katika Mfuiko wa Maendeleo ya Vijana.
Bango likionyesha mahali zilipo ofisi za Temeke Vijana Saccoss.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia(kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad Mtanda (mwenye miwani) wakisikiliza taarifa fupi ya maendeleo y a Kikundi cha Vijana Waungwana kinachoendesha mradi wa Saloon na kujishughulisha na kazi za sana ya muziki katika Kata ya Sandali Manispaa ya Temeke jana wakati wa ziara ya kutembelea Vikundi vilivyopata mkopo kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Vijana uliopo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Baadhi ya Vijana wa Kikundi hicho wakiendelea kutoa huduma kwa wateja wao kama wailvokutwa na Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii jana jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mandeleo ya Jamii walipotembelea katika shamba la matikiti linalomilikiwa na Kikundi cha Vijana cha Sokoine Youth Development cha Somangila - Kigamboni jijini Dar es Salaam. Mwenye kofia ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho Bw, Bike Jirani,Mwenye miwani ni Mweneyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Said Mtanda, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw.P. Kagimbo na mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Obama. Kikundi hicho kimewezeshwa kwa kupatiwa mkopo wa jumla ya shilingi milioni tano kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mwenyekiti wa Temeke Vijana Saccoss ambaye pia ni mwanachama wa Kikunsdi cha Sokoine Youth Development Bw. Swaka Abbas akifafanua namna ambavyo Mkopo kutoka Mfulo wa Maendeleo ya Vijana,unaoratibiwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo umewawezesha kuanzisha na kumudu gharama za uendeshaji wa kilimo cha umwagiliaji katika shamba lao la Matikiti lilipo katika kata ya Somangila, Kigamboni jijini Dar es Salaam.Mwenyekoti la kijivu ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia(MB) na mwenye miwani ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Said Mtanda (MB).
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia(MB) akikagua mpira unaotumika katika umwagilia kwenye shamba la matikiti linalomilikiwa na Kikundi cha Vijana cha Sokoine Youth Development cha Somangila - Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii jana jijini Dar es Salaam.
Picha ikionyesha miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Matikiti linalomilikiwa na Kikundi cha Vijana cha Sokoine Youth Development cha Somangila - Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad Mtanda (Mwenye miwani kushoto) akisisitiza jambo kwa mwanachama wa Kikundi cha Sokoine Youth Development Bw. Swaka Abbas wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyonufaika na Mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika Manispaa hiyo jana.

No comments: