Sunday, January 11, 2015

MKUU WA MKOA WA DODMA ATEMBELEA TAASISI ZA DINI MKOANI HAPO

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akipokelewa na Viongozi wa BAKWATA Dodoma na baadhi ya taasisi zilizo chini yake alipofanya ziara ofisini kwao Januari 9, 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alkizungumza na viogozi wa Dini ya Kiislamu na baadhi ya wajumbe wa BAKWATA Dodoma alipofanya ziara ofisini kwao Januari 9, 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akiwa kwenye picha ya pamoja na viogozi wa Dini ya Kiislamu na baadhi ya wajumbe wa BAKWATA Dodoma alipofanya ziara ofisini kwao Januari 9, 2015.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Chiku Gallawa akilakiwa na Askofu Amon Kinyunyu wa Kanisa la Kiinili Kilutheri Tanzania Mkoa wa Dodoma alipofanya ziara kutembelea taasisi za dini Januari 9, 2015.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Chiku Gallawa (kulia) akizungumza na viogozi wa Kanisa la Kiinili Kilutheri Tanzania Mkoa wa Dodoma alipofanya ziara kutembelea taasisi za dini Januari 9, 2015.
Mzee wa Kanisa la Sabato Dodoma Wallace Lusungwi akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Dodoma Chiku Gallawa zawadi ya vitabu wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa kutembelea taasisi za dini Januari 9, 2015.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Chiku Gallawa akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vionozi na waumini wa kanisa la Sabato Dodoma wakati Mhe. Gallawa alipotembelea taasisi za dini Januari 9, 2015.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Chiku Gallawa Mwishoni mwa wiki (Jan 9,2015) amefanya ziara ya kutembelea taasisi za Dini zilizopo Mkoani Dodoma kwa lengo la kufahamiana nazo tangu awe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na pia kuimarisha mahusiano kati ya serikali ya Mkoa na taasisi hizo za dini.

Hiyo ni mara ya kwanza Mkuu huyo wa Mkoa anatembelea taasisi hizo za dini Mkoani humo tangu ameanza kuongoza Mkoa wa Dodoma kufuatia mabadiliko ya wakuu wa Mikoa yaliyofanywa na Rais Kikwete mwezi Novemba 2014.

Mheshimiwa Chiku Gallawa ameielezea ziara hiyo kuwa ya umuhimu Mkubwa na lengo kuu ni kukutana na taasisi hizo, kufahamiana na kuimarisha mahusiano kwa kutambua kuwa taasisi hizo zinafanya kazi kubwa kwa kusaidiana na serikali kuhakikisha Mkoa na Taifa kwa ujumla linaendelea kuwa na Amani na Utulivu na watu wake wanaendelea kuwa wananchi wema.

Amesema anatambua kazi kubwa inayofaywa na taasisi za Dinina ameahidi serikali itaendelea kushirikiana nazo kwa karibu na kuwa ziara kama hizo zitakua endelevu kwa taasisi nyingine lengo Serikali kufaya kazi kama timu na taasisi mbalimbali kwani kazi ya kuongoza inahitaji ushirikiano mkubwa na jitihada za pamoja kutoka taasisi mbalimbali.

Kwa upande wake viongozi wa taasisi hizo za dini wamepongeza hatua hiyo ya Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma na kuelezea kuwa kuna umuhimu mkubwa serikali kushirikiana na taasisi za dini na wameahidi kuendelea kuwa karibu na uongozi wa mkoa.

Akiwasilisha salamu za Sheikh wa Mkoa wa Dodoma ambaye alikuwa safarini, kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Ahmed Said amesema sheikh wa Mkoa anampongeza Mkuu wa Mkoa kwa kutembelea taasisi za Dini na amemtaka Mkuu wa Mkoa kutambua kuwa BAKWATA ndio taasisi na Baraza kuu la kiislamu Tanzania siku zote imekua ikishirikiana na serikali na itaendelea kufanya hivyo.

Vilevile BAKWATA itaendelea kushauri masuala ya dini ya kiislamu, itaendelea kushirikiana na serikali kutoa huduma za jamii kama elimu na amemkaribisha Mku huyo wa Mkoa wakati wote milango iko wazi.

Nae Katibu wa Jimbo Katoliki Dodoma Padre Thomas Lali amemwelezea Mkuu wa Mkoa kuwa pamoja na kazi ya kanisa kuhudumia Jamii kiroho hapa Mkoani, Kanisa linaprgramu ya huduma za vyuo na shule mbalimbali kwa kuwa kwa sasa mkoa wa Dodoma ni Mkoa wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya elimu ya Juu.


Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoa wa Dodoma Amon Kinyunyu amesema kanisa linatambua kuwa kipindi hiki ni nyeti, Nchi inaelekea kwenye Chaguzi, changamoto ni nyingi na Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi na Jichola Nchi. Dodoma imekua na utamadui na desturi ya kushirikiana kwa karibu na serikali kupitia umoja wao wa viongozi wa dini mbalmbali ambao kwa muda mrefu umesaidia sana kukuza umoja wa wananchi Mkoani Dodoma.

No comments: