Thursday, January 22, 2015

MAMA MKULIMA ASHINDA MIL. 10/- ZA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM

Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao(kulia)akiandika namba ya Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa aliyeibuka mshindi wa Shilingi Milioni 10/- katika droo ya nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,wengine katika picha kutoka kushoto Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu na Meneja uhakiki wa mapato Vodacom Zakaria Kamweru.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na mshindi wa shilingi Milioni 10/- Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa,aliyeibuka na ushindi huo katika droo ya nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na mshindi wa shilingi Milioni 10/-Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa,aliyeibuka na ushindi huo katika droo ya nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo,kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Mkazi wa kijiji cha Inyonga Mkoani Rukwa Hyness Petro Kanumba (20) leo ameibuka mshindi wa kwanza wa Milioni 10 katika droo ya nane ya promosheni ya Jaymilions inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Hyness ambaye ni mama mwenye mtoto mmoja pia mkulima amesema kuwa amepokea taarifa hizo kwa furaha akiwa shambani katika kazi zake za kilimo, kwa kuwa anaamini Mungu amemuona na kwa ushindi huu utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.

“Kwa muda mrefu nimekuwa nikihangaika na kazi za kilimo na kukumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa masoko ya mazao ,pembajeo za kisasa .Kwa ushindi huu naamini nitaboresha shughuli zangu za kilimo ikiwemo kuanzisha biashara ndogo na kuboresha makazi yetu,nashukuru Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii”.Alisema Hynes kwa furaha.

Akiongea muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi,Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja wote wa Vodacom kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda.

Alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja watano wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya nane hivyo bado kuna mamilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.

Promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions inawahusisha wateja wote wa Vodacom,kiasi kikubwa cha fedha kitaendelea kutolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu”.Alisema.

Vodacom imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-

No comments: