Thursday, January 22, 2015

ISACA TANZANIA YATOA SEMINA KUHUSU USALAMA WA MITANDAO

 Makamu wa Rais wa Isaca Tanzania Chapter ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao, Dk. Jabir Bakari akitoa hotuba yake wakati akifungu semina kuhusu usalama wa mifumo ya kompyuta pamoja na ukaguzi wa mifumo hiyo kwa kuwakutanisha wataalumu na kujadiliana kuhusu ukuaji wa teknolojia na usalama.

Aidha Dk. Jabir alisema kuwa semina hiyo inawakutanisha wataalamu wa mifumo ya kompyuta kutoka ndani na nje ya nchi watakaojifunza na kuongeza utaalamu wa kulinda mifumo ya mitandao. 

Naye Mratibu wa Semina hiyo ambaye pia ni Rais wa Isaca Tanzania, alisema kuwa semina hiyo kwa ajili ya kuelezea wadau wa mitandao kuhusu mwelekeo wa teknolojia duniani na ukubwa wa tatizo katika wizi wa mitandao  'miaka ya nyuma kulikuwa na wizi wa kuvunja katika mabenki lakini siku hizi mbinu za wizi zimebadilika na wezi wanaiba kupitia mifumo ua mitandano hasa kompyuta pamoja na simu, kutoa elimu ya ajili ya mifumo ya kompyuta namna ya kuilinda na kuiendeleza.
Katibu wa Tanzania Chapter, Nemayani Kaduma (kulia)akiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina ya ya kimataifa kuhusu usalama wa mitandao wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Taasisi ya Isaca Tanzania Chapter, Dk. Jabiri Bakari (hayupo pichani) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Washiri wa semina wakifuatikilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa.
Washiriki wa semina hiyo.
Washiriki.

George Wahome kutoka Isaca-Kenya akitoa mada kuhusu usalama wa mitandao.
Washiriki wa semina.
Rais wa Isaca Tanzania Chapter, Boniface Kanemba akifuatilia mada katika semina hiyo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania, Adebowale Atobatele akitoa mada katika semina hiyo.
Rais wa Isaca Tanzania Chapter, Boniface Kanemba akizungumza na waandishi wa habari.
Washiri wa semina hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Rais wa Isaca Tanzania Chapter, Boniface Kanemba (kulia) akimpongeza Isack Maheri  aliyefaulu mitihani ya ukaguzi wa Mitandao ijulikanayo kama CISA.
Rais wa Isaca Tanzania Chapter, Boniface Kanemba (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Isaca Tanzania, Dk. Jabir Bakari (wa tatu kushoto), Katibu wa Tanzania Chapter, Nemayani Kaduma (kushoto) na Mkurugenzi wa Elimu Mtandao, Dk. Carina Wangwe (kulia) na Peter Baziwe (wa tatu kulia)

No comments: