Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz Prof. Peter Msolla na Naibu Waziri wa Maji Mh. Amosi Makalla wakifungua koki za maji kando kidogo ya manispaa ya Iringa.
Kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz wakiongozwa na Prof. Peter Msolla na Naibu Waziri wa Maji Mh. Amosi Makalla wakikagua miundombinu ya maji katika Halmashauri ya Ilola.
Mhandisi wa maji Manispaa ya Iringa akisoma taarifa ya miradi ya halmashauri ya manispaa hiyo mbele ya kamati, Naibu Waziri na Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Na: Athumani Shariff
Wizara ya Maji imelazimika kuwapeleka wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Klimo, Mifugo na Maji katika miradi mbalimbali ya maji Tanzanina bara, ili kujionea hali ya utekelezaji wa miradi ya maji,mafanikio ya sekta ya maji, changamoto zinazoikumba sekta ya maji pamoja na hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Maji na Halmashauri za Wilaya na Mikoa husika katika kukabiliana na changamoto hizo.
Ziara hizo zilianza tarehe 20, Januari mara baada ya kikao kati ya Kamati hiyo ya Bunge na watendaji wa Wizara ya Maji wakiwemo viongozi wa DAWASA na DAWASCO katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya majadiliano ya kina juu ya sekta ya maji, changamoto na hatua zinazochukuliwa, wajumbe wa kamati hiyo waligawanyika katika makundi manne (Kundi la Pwani, Lindi na Mtwara), kundi la (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara), kundi la Mwanza, Simiyu, Geita na Mara) na kundi la Morogoro, Iringa na Mbeya).
Katika ziara hiyo waheshimiwa wabunge waliambatana na wataalamu kutoka Wizara ya Maji kwenda kujionea miradi ya maji, vyanzo vya maji, kuongea na wananchi kujua matatizo yao katika sekta ya maji na kutoa ushauri wao kwa serikali ili kutatua kero za maji.
Kundi la Morogoro, Iringa na Mbeya linalohusisha wabunge; Prof. Peter Msolla, Prof. David Mwakyusa, Dr. Lucy Nkya, Dr. Christine Ishengoma pamoja na Mch. Peter Msigwa walianza ziara yao Mkoani Morogoro.
Baada ya kujionea halihalisi, kamati ilishauri mambo kadhaa kwa wanachi na watendaji wa serikali na mamlaka husika ikiwemo, uchangiaji wa miradi ya maendeleo, kulinda vyanzo vya maji, kutunza miundombinu ya maji, kuhamisha na kuwachukulia hatua waharibifu wa vyanzo vya maji.
“Sisi ni Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji tumekuwa tukisoma tu kwenye makaratasi hali ya miradi ya maji, hivyo sasa tumeamua kuja wenyewe kujionea halihalisi ya miradi ya maji huku kwa wananchi, kwani kuona ni kuamini” alisema Prof. Msolla mwenyekiti wa kamati hiyo.
Naye kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji Amos Makalla aliwaambia wananchi wa Fulwe Mkoani Morogoro kuwa kuchangia miradi ya maendeleo ni muhimu sana ili wananchi waweze kuhisi umiliki wa mradi, hata hivyo ni kiasi kidogo sana ambacho wananchi wanachochangia ni kati ya asilimia 2 hdi tano.
Naye kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Anthony Mtaka aliwataka wanasiasa kushikiriana na watendaji serikalini katika kuwaelimisha wananchi kufata sheria zinavyoelekeza.
“Swala la kuwahamisha wanaoharibu vyanzo vya maji kwa shughuli za kibinaadamu linawezekana na huwa tunalifanya, shida kubwa tunayokumbana nayo ni utetezi wa wanasiasa, tukiambiwa serikali hatuna huruma kwa wananchi wetu, hivyo tunawaomba sana waheshimiwa wabunge mutusaidie na mtuunge mkono ili tufanikiwe katika adhma hii na kwa hapa Morogoro tayari Mkuu wa Mkoa amekataza kuona mkaa”. Alisema Mtaka.
Siku ya pili ziara hiyo ipo mkoani Iringa na inatarajiwa kukamilika tarehe 23, Januari 2015.
No comments:
Post a Comment