Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge(wa kwanza) akishuka ngazi
mara baada ya kukagua kivuko cha MV-Utete ambacho hakitoi huduma ya
usafirishaji kutokana na kupungua kwa kina cha maji cha mto Rufiji.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA), Eng.
Manase Ole-Kujan (wa kwanza kushoto) akitoa taarifa ya kivuko cha MV-
Utete kwa naibu waziri wa ujenzi Eng. Gerson Lwenge.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge (wa pili kulia) akitoa
maelekezo na maagizo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme(TEMESA), Eng. Manase Ole-Kujan baada ya kukagua kivuko
cha Mv-Utete wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Muonekano wa kivuko cha MV-Utete ambacho kimeegeshwa na kusitisha
huduma zake kutokana na kupungua kwa kina cha maji cha mto rufiji.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge (wa kwanza kulia) akimpa
pole Mkuu wa mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo kufuatia mauaji ya
askari polisi wawili katika kituo cha polisi cha Ikwiriri Wilayani Rufiji.
No comments:
Post a Comment