Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohammed Shein akikabidhi tuzo ya heshima ya mwanamichezo bora wa mwaka kwa Mama Fatma Karume Mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Usiku huu, Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA Bw. Juma Pinto.)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohammed Shein akisoma hotuba yake mara baada ya kukabidhi tuzo hiyo kwa Mama Fatma Karume Mjane wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Usiku huu.
Mama Fatma Karume Mjane wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume akitoa nasaha zake kwa wanamichezo usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA Bw. Juma Pinto na Maulid Kitenge Mtangazaji wa Redio ya EFM ambaye alikuwa MC wa hafla hiyo.
Waziri wa Habari , Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara akikabidhi tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka katika mchezo wa wa kulipwa katika mchezo wa gofu Hassan Kadilo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Bw. Jamal Malinzi akikabidhi tuzo ya mwanamichezo bora chipukizi wa mwaka katika mchezo wa gofu Nuru Molel
Waziri wa Habari , Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara akimkaribisha Rais Dr. Shein ili aongee na wanamichezo.
Mkurugenzi wa TV 51 na The Fadhaget Sanitarium Clinic Dr. Fadhili Emily chini ya Fadhaget Media Limited akiwa katika hafla hiyo.
baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment