Mgeni
Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikata utepe kuzindua
ukarabati wa Madarasa manne na Jengo moja la Utawala katika Shule ya
Msingi Hasanga uliofanyika leo Uyole Mbeya.
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro, viongozi wa Shirika la
Nyumba la Taifa Tanzania (NHC), Viongozi wengine wa Serikali na Walimu
wa Shule ya Msingi ya Hasanga wakifurahia Baada ya Kuzindua Rasmi
ukarabati wa ujenzi huo.
Meza kuu
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akizungumza na wananchi,
wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi ya Hasanga katika Sherehe ya
kukabidhi Majengo ya Shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigallah King akimkaribisha Mkuu wa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro
Meya wa Jiji la Mbeya Atanus Kapunga akitoa neno la Shukurani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Akiwakaribisha Wageni katika Sherehe hizo
Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Mbeya Anthony Komba akisoma Taarifa ya ukarabati wa Shule hiyo
Mwalimu Neema Sanga (Kushoto) akisoma Risala ya Shule
Baadhi ya Wageni waalikwa na Meza Kuu
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikagua Baadhi ya Majengo
Muonekano wa Baadhi ya Majengo ya Shule ya Msingi Hasanga yaliyokarabatiwa na Shirika la Nyumba la Taifa
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua tukio.
CHINI NI VIDEO FUPI YA HARAMBEE ILIYO ONGOZWA NA MKUU WA MKOA
***********
SHIRIKA
la Nyumba la Taifa(NHC) limefanya ukarabati wa majengo ya shule ya
Msingi Hassanga iliyopo Uyole jijini Mbeya ambayo alisoma Mkurugenzi
Mkuu Nehemia Mchechu.
Makabidhiano
ya mradi huo umefanyika leo katika sherehe zilizofanyika katika viwanja
vya shule hiyo na kuhudhuriwa na Mkurugenzi mkuu, viongozi wa
Halmashauri ya Jiji, Wilaya na Shirika la Nyumba ambapo Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Abbas Kandoro alikuwa mgeni rasmi.
Aidha
ukarabati wa majengo manne na jengo moja la utawala uliofanywa na
shirika la Nyumba(NHC) umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 31.
Mkurugenzi
mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu,katika taarifa yake iliyosomwa na Meneja
wa Shirika hilo Mkoa wa Mbeya,Antony Komba, amesema Shirika hilo
liliamua kufanya ukarabati wa jengo la utawala na madarasa manne ya
shule hiyo kama sehemu ya mchango wake kwa jamii kufuatia maombi
yaliyofanywa na Kamati ya shule ya kuombwa ukarabati wa majengo hayo.
Amesema
kazi ya ukarabati ilianza Aprili 19 na kukamilika Agosti 20, Mwaka huu
ambapo Shirika lilikarabati Jengo la utawala katika ujengaji upya wa
kuta za jengo , bimu na uezekaji upya wa paa, upigaji lipu, sakafu na
rangi pamoja na kuweka milango na madirisha ya alminium kwa gharama ya
shilingi Milioni 22,77,900.
Ameongeza
kuwa ukarabati katika madarasa manne ulihusu upigaji upya wa lipu
ukutani, utengenezaji wa sakafu , utengenezaji wa shata za madirisha
pamoja na upakaji rangi uliogharimu shiringi Milioni 8,803,000 na
kufanya jumla ya shilingi Milioni 31, 577,900.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, mbali na kulishukuru
shirika hilo kwa msaada wao huo pia ametoa wito kwa Wanafunzi na Walimu
pamoja na uongozi wa kamati ya shule kuyatunza majengo hayo ili yaweze
kudumu.
Hata
hivyo katika hatua Nyingine Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alilazimika kuendesha
harambee nyingine baada ya Mkurugenzi wa NHC, Mchechu kujibu risala ya
walimu walioomba kukarabatiwa majengo mengine ambapo alisema kama
wataweza kuchangia chochote Shirika litaweza kumalizia.
Katika
harambee hiyo ambayo pia ilichangiwa na Shirika Mkuu wa Mkoa
alifanikiwa kukusanya Shilingi Milioni moja na laki tatu ambazo
alizikabidhi kwa Mkurugenzi wa Shirika ambaye baada ya kupokea aliahidi
kuanza ujenzi kesho wa majengo mengine manne.
Nao
Walimu wa Shule ya Msingi Hassanga katika Risala yao kwa Mgeni
rasmi,iliyosomwa na Mwalimu Neema Sanga, wamelipongeza shirika la Nyumba
kwa kukarabati majengo hayo.
Wamesema
ukarabati wa Vyumba vine vya madarasa, ofisi ya Walimu pamoja na Ofisi
ya Mwalimu Mkuu ni moja ya kutambua umuhimu wa Elimu na kujenga
mazingira rafiki ya kufundisha na kujifunzia.
No comments:
Post a Comment