Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (kulia) akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati akizindua ushirikiano wa kampuni yake na
Benki ya Afrika (BOA) Tanzania unaowawezesha mawakala wa M-pesa na
wasambazaji wa huduma za Vodacom kupata miko nafuu na bila dhamana
kuinuua biashara zao. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya BOA, Ammish Owusu – Amoah.Hafal hiyo imefanyika Makao Mkauu ya Vodacom, Dar es salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Afrika (BOA) Tanzania Ammish Owusu – Amoah
(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza
wakipongezana mara baada ya kutangaza rasmi ushirikiano
unaowawezesha mawakala wa M-pesa na wasambazaji wa huduma za Vodacoyam
kupata mikopo nafuu na bila dhamana kutoka BOA kwa lengo la kuinuua
biashara zao. Mikopo hiyo ni kati ya Sh 10 Milioni na 75 Milioni.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Afrika (BOA), Ammish Owusu –
Amoah(kushoto)akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani)kuhusiana na kuingia ubia na Vodacom Tanzania ambao
utawawezesha mawakala wa kuuza na kusambaza bidhaa za kampuni hiyo
kupata mikopo ya masharti nafuu na bila amana ili kuwawezesha kutoa
huduma bora kwa wateja wao,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom
Tanzania,Rene Meza.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Afrika (BOA)-Tanzania na wa Vodacom Tanzania
wakifuatilia mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa ushirikiano kati ya BOA benki na Vodacom Tanzania ambao
utawawezesha mawakala wa M-pesa na wauzaji wakubwa wa bidhaa za Vodacom
kupata mikopo ya kati ya Sh 10 Milioni na 75 Milioni kwa masharti nafuu
na bila amana ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja.
Ofisa
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh(kulia) na
Mkuu wa Mauzo wa M pesa Franklin Bagala wakifuatilia mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa ushirikiano kati ya BOA benki na Vodacom Tanzania ambao
utawawezesha mawakala wa M-pesa na wauzaji wakubwa wa bidhaa za Vodacom
kupata mikopo ya kati ya Sh 10 Milioni na 75 Milioni kwa masharti nafuu
na bila amana ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja.
========= ======== =======
-Kupatiwa mikopo ya masharti nafuu
-Pia kuanzisha huduma ya kuwahudumia wateja wa M-pesa
Dar es Salaam Sep 3,2014.Benki
ya Africa (BOA)-Tanzania imeingia ubia na kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania, ambao utawawezesha mawakala wa kuuza na kusambaza
bidhaa za Vodacom kupata mikopo ya masharti nafuu na bila amana ili
kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja wao.
Chini
ya mpango huu mawakala wa Vodacom wataweza kuchukua mkopo unaofikia
mara 6 ya kamisheni wanayokuwa wamepata katika kipindi cha miezi 6 kabla
ya kuomba mkopo. Wataweza kukopa kuanzia kiasi cha shilingi milioni 10
na kiasi cha juu ya kukopa ni shilingi milioni 75 .Mkopo huu ambao ni
mkombozi kwa mawakala hao una riba ya asilimia 1.7 kwa mwezi na
unatakiwa kulipwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza,amesema kuwa mpango huu
umeanzishwa kwa ajili ya kuwawezesha makala waliopewa jukumu kusambaza
nchi nzima bidhaa za Vodacom ikiwemo vocha za kununua muda wa maongezi
kuwa na mzunguko mzuri wa pesa utakaowawezesha kutoa huduma bora kwa
wateja .
“Mpango
huu utawawezesha mawakala wetu kuimarika kibiashara wakati huohuo kutoa
huduma bora kwa wateja wetu na kiwango chao cha mauzo
kitaongezeka.Kwetu Vodacom mpango huu ni wa muhimu sana na makala wa
kuuza na kusambaza bidhaa zetu ambao watachangamkia fursa hii ambayo
itawasaidia kufanya biashara kwa kujiamini na kuhakikisha wateja wetu
ambao kila kukicha wanaongezeka mara dufu wanapata huduma za kuridhisha
popote walipo nchini”Alisema Meza.
Kwa
upande wake,Afisa mtendaji wa Benki ya BOA, Ammish Owusu –
Amoah, amesema ushirikiano huu na Vodacom umefungua ukurasa mpya kwa
benki,wateja wake na kwa wanajamii ya Tanzania kwa ujumla, kwa kuwa
wanaelewa kiu ya wajasiriamali wa Tanzania wanavyohangaika kutafuta
mikopo kwa ajili ya kukuza na kuboresha biashara zao.
“Kama
benki ili kufanikisha huduma hii ya kutoa mikopo tumeanzisha kitengo
maalumu cha kusimamia huduma hii ya kutoa mikopo kwa wajasiriamali bila
urasimu katika matawi yetu yote nchini pia benki itahudumia wateja wa
M-pesa”Alisema Ammish.
Alisema
mpango huu ambao umezinduliwa leo unawawezesha wauzaji na wasambazaji
wa bidhaa za Vodacom kupatiwa mtaji wa kufanya biashara zao wanapotaka
kukununua bidhaa nyingi zaidi ya mtaji walionao.Mkopo unaanzia shilingi
milioni 10 mpaka milioni 75 kwa awamu ya kwanza na kwa wateja
watakaotimiza vizuri taratibu na masharti ya mkopo wanaweza kufikiriwa
kupatiwa mkopo mkubwa zaidi ya shilingi milioni 75.
Aliongeza
kuwa huduma hii inawalenga wauzaji na wasambazaji wakubwa wa bidhaa za
Vodacom zaidi ya 100 ambao wataweza kununua bidhaa kupitia matawi ya
BOA-Tanzania na pesa zitaingizwa katika akaunti ya Vodacom iliyopo
kwenye benki hiyo na ana imani huduma hii itawarahisishia kufanya
biashara zao kwa kupata bidhaa wanazohitaji haraka kutoka Vodacom.
Vodacom
imekuwa ikibuni huduma mbalimbali za kuwarahishia
wananchi maisha.Moja ya huduma ni M-pesa ambayo tangu ianzishwe hapa
nchini imepokelewa vizuri na wananchi ikiwa inarahisisha maisha wakati
huohuo ikiwa imetoa ajira kwa wananchi wengi.Mpaka sasa mtandao wa
M-pesa una mawakala wapatao zaidi ya 70,000.
Mawakala
watakaohitaji kupata mkopo huu watapaswa kutembelea matawi ya benki ya
BOA- Tanzania ambayo yako katika mikoa ya Dar es Salaam ambako ina
matawi 11 na matawi mengine yapo katika mikoa
ya,Arusha,Shinyanga-Kahama, Kilimanjaro,Mbeya,Morogoro, Mtwara na Mwanza.
Benki
ya BOA Tanzania iko chini BOA Afrika,kwa hivi sasa inaendesha shughuli
zake za kibenki katika nchi 17 za Afrika na nchi moja ya Ulaya ambazo ni
: Benin, Burkina Faso, Burundi, Djibouti, Ethiopia, Togo, DRC, France,
Ghana, Ivory Coast, Kenya, Madagascar, Mali, Niger, Senegal, Tanzania
and Uganda.
No comments:
Post a Comment