Wednesday, September 3, 2014

YOUNG AFRICANS NA BENKI YA CRDB WAINGIA MAKUBALIANO YA UTENGENEZAJI WA KADI ZA KISASA ZA UANACHAMA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kulia) akisaini mkataba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Yanga, Fatma Karume kwa ajili ya kutengeneza kadi za kisasa za uanachama wa klabu hiyo za mfumo wa kieletroniki 'Gold Premium Card'. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Yanga, Mama Fatma Karume akipitia mkataba walioingia na Benki ya CRDB. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akionyesha kadi ya kisasa ya uanachama wa Yanga ikiwa katika mfumo wa kieletroniki kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo, mama Fatma Karume.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga,  Fatma Karume kadi namba moja ya mfumo wa kieletroniki 'Gold Premium Card' mara baada ya benki hiyo kuingia mkataba wa kutengeneza kadi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga,  Fatma Karume akizungumza katika hafla hiyo. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay. (katikati)
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei  akizungumza wakati wa hafla hiyo.


NA CLEZENCIA TRYPHONE

BENKI ya CRDB imeingia mkataba na klabu ya Yanga kwa ajili kutengeneza kadi za kisasa za uanachama wa klabu hiyo, ambazo pia watazitumia kuingilia viwanjani katika mechi mbalimbali za mfumo wa tiketi za kieletroniki.

Yanga imefikia hatua hiyo, kwa lengo la kuitafutia klabu vyanzo vya mapato kwa ajili ya kujiendesha, ili iweze kufikia hatua nzuri zaidi kama ilivyo kwa timu kubwa kama TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na nyinginezo.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei, alisema kuwa mkataba huo ni wa kudumu, ila utaweza kuvunjwa endapo mambo yakienda tofauti na makubaliano.

Kimei aliyasema hayo, katika zoezi hilo lilishuhudiwa na Fatma Karume ambaye ni Mwenyekiti katika Bodi ya wadhamini wa Yanga aliyeweka sahihi katika mkataba huo, pamoja na Francis Kifukwe na Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga.

Akizungumza kwa niaba ya Yanga, Fatma alisema, wao kama timu kongwe hapa nchini, imefarijika kuona benki kubwa kama hiyo ikiwapa sapoti kubwa, ambapo yeye amepewa kadi namba moja.

“Tunafarijika sana, sisi kama Yanga kupata udhamini huu mnono, na Yanga ni taasisi kubwa na ndio maana hata bendera za Taifa zinafanana na rangi ya klabu yetu, sio hao Simba damu tu,”alisema.

No comments: