Tuesday, September 16, 2014

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakutana na wadau wa Maendeleo jijini DSM kufanya Mapitio ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini PSSN.

Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Maendeleo, maafisa wa serikali na TASAF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo kwenye ukmbi wa miktrano wa Mwalim Nyerere jijini DSM.

 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw Ladislaus Mwamanga akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa Mkutano wa pamoja baina ya wadau wa maendeleo,Maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini DSM leo.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo akifungua mkutano wa wadau wa Maendeleo ,maafisa wa Serikali na watendaji wa TASAF uliofanya mapitio ya Mpango wa kunusuru kaya maskini uliofanyika kwenye Ukumbi kimataifa wa  Nyerere Jijini DSM.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Peter Ilomo (aliyeketi katikati) akiwa na viongozi wengine Katika meza kuu wakifuatilia maelezo ya Mkurgenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani) wakati wa ufungzi wa Mkutano wa mapitio ya Mpango wa Kunusuru kaya maskini uliofanyika jijini DSM.
 Wakurugenzi wa TASAF Bw.Amedeus Kamagenge wa kwanza mbele na  Fariji Mishael wa pili wakifuatilia mjadala wa mapitio ya Mpango wa Kunusuru kaya maskini kati ya wadau wa maendeleo ,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF kwenye ukumbi wa kimataifa wa MWL jk Nyerere jijini DSM.
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abass Kandoro katikati akifuatilia mada kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo ,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF ambao mefanya mapitio ya Mpango wa knusuru kaya maskini kwenye ukmbi wa Kimataifa wa JK Nyerere jijini DSM.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadao wa maendeleo na wale wa serikali na TASAF wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano uliojadili maendeleo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini PSSN.
 Mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini Kong’enza Mfunda Chanzi  mkazi wa Mwanabwito  wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani akitoa ushuhuda wa namna alivyonufaika na Mpango wa kunusuru kaya maskini kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF.



No comments: