Tuesday, September 16, 2014

WAKAZI WA TABORA WAKIRI WAZI KUWA MASOKO NDIO CHANGAMOTO YAO KUBWA KATIKA SHUGHULI ZAO ZA UJASILIAMALI

SEMINA ya Kamata Fursa Jitathimini,Jiamini,Jiongeze inayoendeshwa sambamba na burudani za Fiesta 2014, jana imeendelea kwa kuwapatia dira ya maisha na namna ya kuwafanya wajikwamue kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi wakazi wa Mkoa wa Tabora mjini ndani ya ukumbi wa chuo cha TEKU,kilichopo katikati ya mji wa Tabora.
Semina hiyo ambayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (pichani juu) ilikuwa ya aina yake, kwani baadhi ya vitu na mbinu alizowapatia wakazi wa Mkoa wa Tabora,wengi wao wameonesha kuvutiwa nayo kutokana na mafunzo,maelekezo na mbinu mbalimbali za kupambana na changamoto zinazowakabili/zitakazowakabili katika miradi yao mbalimbali wanayotarajia kuianzisha ama wamekwishaianzisha.
 Msanii muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Weusi,Niki wa Pili  akizungumza na vijana mbalimbali waliokuwa wamegawanywa katika makundi ili kusikiliza mipango na miradi waliyonayo na namna wanavyoiendeleza,lakini pia Washiriki hao walielezwa namna ya kujikwamua na changamoto wanazokumbana nazo katika kuendeleza miradi yao,ikiwamo na namna ya kujitafutia soko ,jambo ambalo Washiriki hao wamekiri wazi kuwa ndio changamoto yao kubwa katika shughuli zao za ujasiliamali.

  Meneja wa Maxcom Africa, ‘Max malipo’,  Bernard Munubi  akiwa katikati ya vijana akiwaeleza namna ya kufanikiwa katika shughuli zao kimaendeleo na pia kuwapatia mbinu za kupambana na changamoto na hatimae kuelekea kwenye kilele cha mafanikio .Bernad pia aliwaeleza washiriki hao kwa wale ambao wanafikiria kuanza miradi ya ujasiliamali,kwamba si vibaya wakaanza kujaribu kujitafutia maendeleo kupitia mashine na Max Malipo na kujionea wenyewe namba zinavyoweza kusaidia kiasi kikubwa cha umaskini miongoni mwao.Mnubi alisema kuwa mmpaka sasa mashine hizo zimewaletea mafanikio makubwa ya kiuchumi watu wengi.
 Mmoja wa Wajasiliamali kutoka mjini Tabora ,Dada Flora Zakaria ambaye amejiunga kwenye moja ya kikundi kinachofanya shughuli mbalimbali kupitia kikundi chao kiitwacho JACANA Natural Products,akionesha aina ya sabuni zilizotengenezwa na kikundi chao,ambapo pia kikundi hicho hujishughulisha na utengenezaji wa vipodozi vya asili kwa akina mama pamoja na mafuta ya aina mbalimbali.Flora alieleza kuwa wamekuwa wakijitahidi kutengeneza bidhaa mbalimbali lakini changamoto yao kubwa imekuwa ni namna ya kupata soko la kuziuza bidhaa zao.
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha VETA wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikichambuliwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba (hayupo pichani).Ambapo washiriki wa semina hiyo waliunda vikundi na kubainisha wana miradi gani ama  wanatarajia kuanza kufanya miradi gani,ili kusaidia kutatua vikwazo na kutoa miongozo kwa namna moja ama nyingine.
 Niki wa Pili akifafanua jambo kwa baadhi ya Washiriki wa Semina hiyo ya Fursa,ambayo imekuwa ikiwavutia watu wa rika mbalimbali wakiwemo vijana kwa wazee.
 Pichani juu na chini ni washiriki wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye semina ya Fursa na wengine waliweza kuandika jambo lolote waliloliona lina manufaa kwao.
 Sehemu ya Washirikiwa semina ya Fursa wakiwa ndani ya ukumbi wa Chuo cha TAKE wakifautilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo .
 Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi,Mdau Mussa akizungumza na wakazi wa mjii wa Tabora waliofika kwenye semina ya Fursa,iliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha TEKU mjini Tabora.
Baadhii ya Washiriki wakitoka nje ya ukumbi baada ya semina ya Fursa kuisha.

No comments: