Tuesday, June 17, 2014

BENKI YA CRDB YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUTUMIA AKAUNTI YA JUNIOR JUMBO

Na Mwandishi Wetu

Benki ya CRDB imetoa misaada mbalimbali kwa watoto wasiojiweza katika kituo cha Msimbazi centre.

Hatua hiyo imetokana na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yenye kauli mbiu ya elimu bora kwa wote.

Akizungumza Jana jijini Dar es salaam Meneja wa benki hiyo Tawi la Premier, Fabiola Mussula, alisema kuwa benki hiyo imeadhimisha siku ya mtoto  wa Afrika kwa kupitia akaunti ya Junior Jumbo.

Alisema kuwa akaunti ya mtoto  humsaidia mzazi kuhakikisha anahifadhi ada na kulipa kwa wakati pindi inapotakiwa.

Fabiola alisema kuwa ni vyema wazazi wa kitanzania wakaweka akiba ya mtoto  ili kupunguza ukali wa maisha unaowakuta wazazi wengi.

" akaunti hii itambana mzazi kutokutoa hela Mara kwa Mara, na itamruhusu katika msimu wa ada pekee lakini pia anaweza akatuambia sisi watu wa Benki na tukamlipia shuleni na ni akaunti isiyo na makato"alisema.

Naye Neema Tarimo, alisema yeye kama mzazi Hutumia akaunti ya mtoto  kwa kuhifadhi ada za watoto wake na kuongeza kuwa humsaidia kumbana kutotoa fedha kila wakati na badala yake huzitoa pindi anapohitaji ada.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Premier, Fabiola Mussula akizungumza waandishi wa habari kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika waliyoandaa kupitia akaunti ya Junior Jumbo kwa ajili ya watoto.
 Kila aina ya michezo ilikuwepo katika kuipamba Siku ya Mtoto wa Afrika. 
 Watoto wakicheza michezo mbalimbali nje ya Benki ya CRDB Tawi la Premier, uongozi wa Benki ya CRDB iliwaandali michezo mbalimbali watoto ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Meneja wa Akaunti ya Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Mary Kimasa akimlisha keki mmoja wa watoto wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Tawi la Premier  jijini Dar es Salaam.

 Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Premier, Fabiola Mussula (kushoto), akimkabidhi zawadi mtoto,  Hildegalde Moris ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika tawi hilo jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha watoto kutoka  shule mbalimbali za msingi.
 Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Premier, Fabiola Mussula (kushoto), akimkabidhi zawadi mtoto,  Owen Gerald ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika tawi hilo jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha watoto kutoka  shule mbalimbali za msingi.
 Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Premier, Fabiola Mussula (kushoto), akimkabidhi zawadi mtoto,  Jorren Nkongoki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika tawi hilo jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha watoto kutoka  shule mbalimbali za msingi. 
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Smiley Kidz Events, Hilda Nakajumo akitoa maelekezo kwa watoto waliojumuika katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika katika Tawi la Premier jijini Dar es Salaam.  
 Watoto wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Benki ya CRDB.
 Baadahi ya Wazazi walioleta watoto wao katika Benki ya CRDB tawi la Premier wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa benki hiyo mara baada ya wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Premier, Fabiola Mussula (wa tatu kulia kushoto), akiwafariji watoto wanaolelea katika Kituo Cha Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipoenda kuwafariji watotio hao na kutoa zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimishio ya siku ya Mtoto Afrika. 
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Premier, Fabiola Mussula (kulia), akimsikiliza Sista wa zamu wa Kituo cha kulelea watoto cha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipoadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika na watoto wa kituo hicho.
 Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Msimbazi Centre wakicheza
  Sista wa zamu katika Kituo cha kulelea Watotio cha Msimbazi Centre akiwakatika picha ya pamoja na maofisa wa Benki ya CRDB walipotembelea kituo hicho na kutoa zawadi kwa watoto hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Premier  wakiwa wamewabeba na watoto wanaolelewa katika kituo cha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam walipowatembelea watoto hao na kutoa zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.Wa nne kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Premier, Fabiola Mussula. 
Baadhi ya wanafuzi wa shule mbalimbali wakimsiliza Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB Tawi la Tabata, Burtony Mbogella wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika kupitia akaunti ya Junior Jumbo.
 Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Tabata, Hawa Sasya akizungumza na wanafunzi wa shule mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kupitia akaunti ya Junior Jumbo.
Baadhi ya wanafunzi wa Macedonia Nursery & Primary school wakiwasikiliza Maofisa wa Benki ya CRDB walipokuwa wakitoa elimu kuhusu akaunti ya Junior Jumbo.
 Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Water Front, Donath Shirima akifafanua jambo wakati wafanyakazi wa tawi hilo walipojumuika na wanafunzi wa Shule ya Fortune Nursery & Primary katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kupitia akaunti ya Junior jumbo. Kulia ni Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Crala Rogatas na Meneja Mikopo wa benki hiyo, Isaya Lyimo. 
Wanafunzi wa Shule Fortune Nursery & Primary wakionesha umahiri wa kucheza ngoza za asili wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kupitia akaunti ya Junior Jumbo.
Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Water Front, Donath Shirima (kushoto) na Mwalimu wa shule hiyo, Kharifa Rashidi wakikata keki sambamba na wanafunzi wa Fortune Nursery & Primary School wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipojumuika na wanafunzi hao katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. 
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Quality Centre, Clementina Kinabo akitoa elimu kuhusu akaunti ya Junior Jumbo kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Buguruni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.

No comments: