Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (PE. 1656) akila kiapo rasmi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian
Matembele kwa mujibu wa sheria ya usajili wa wahandisi (Engineer's Registration Act (Cap 63), Kanuni na sheria ndogo zote zilizowekwa na zitakazowekwa ikiwemo mwendo wa utendaji kazi pamoja na maadili katika taaluma ya uhandisi.
Kiapo hicho kimeafanyika leo katika ukumbi wa "video comference" uliopo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo tarehe 23-05-2014. Awali kiapo hicho kilikuwa kifanyike Dodoma pamoja na mawaziri na wabunge wengine ambao ni wahandisi lakini kutokana na majukumu yasiyozuilika Eng. Manyanya ameruhusiwa aape akiwa Sumbawanga.
Kiapo hicho kimeafanyika leo katika ukumbi wa "video comference" uliopo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo tarehe 23-05-2014. Awali kiapo hicho kilikuwa kifanyike Dodoma pamoja na mawaziri na wabunge wengine ambao ni wahandisi lakini kutokana na majukumu yasiyozuilika Eng. Manyanya ameruhusiwa aape akiwa Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian Matembele wakisaini hati ya kiapo
hicho mbele ya mashuhuda mbalimbali walioalikwa katika hafla hiyo fupi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza muda mfupi
baada ya kuapishwa, pamoja na mambo mengine amesema ni marufuku kwa wahandisi
ambao hawajasajiliwa kuidhinisha au kupitisha kazi za miradi mikubwa katika Mkoa wake wa
Rukwa. Aliendelea kusema kuwa kwa Mhandisi yeyote ambaye hajasajiliwa hana mamlaka ya kutumia tittle PE. Eng.....kama inavyoelekezwa kwa mujibu wa
sheria, hata hivyo aliwaahidi wahindisi wote ambao hawajasajiliwa katika Mkoa
wa Rukwa ushirikiano katika kuwapa miongozo itakayowawezesha kukamilisha taratibu zao za usajili. Kwa upande mwinine aliipongeza bodi ya ERB kwa kuwa madhubuti na kuweka utaratibu unaowezesha uwajibikaji.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian
akizungumza muda mfupi kabla ya kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella
Manyanya. Katika salam zake za ufunguzi amesema lengo la kiapo ni kula yamini
kwa anayeapishwa kufanya kazi yake kwa kuzingatia uadilifu wa hali ya juu kwa kuzingatia
miiko, kanuni na taratibu zilizowekwa bila kuzivunja ili kuleta ustawi
unaokubalika katika jamii.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa kushoto
akizungumza katika hafla hiyo. Alisema kuwa kwa upande wa wataalamu wa uchumi wanachangia sana katika kuongezeka au kuzorota kwa maendeleo ya nchi lakini hakuna utaratibu rasmi wa kusajiliwa na kuapishwa, Aliongeza kuwa pengine ingekua hivyo wataalamu hao wangekuwa makini zaidi katika kupanga mipango ya nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta kulia akitoa
salam zake katika hafla hiyo. Katika salam hizo alitoa pongezi nyingi kwa niaba ya viongozi wote wa Mkoa wa Rukwa na wananchi kwa ujumla kwa Eng. Manyanya kwa kuwa mfano kwa kuapa kama ambavyo matakwa ya sheria ya usajili wa uhandisi inavyomtaka. Hiyo imekua ni chachu kwa wengine wote ambao hawajajisajiliwa na kuapa waone ni muhimu sasa kufanya hivyo. Kiapo hicho kinatoa funzo kwa watumishi wa kada zote kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo wa hali ya juu.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya
(katikati waliokaa) na Wakuu wa Idara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa
(nyuma waliosimama). Wengine kushoto waliokaa ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian na Bi. Z. A. Mpangule Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Wilaya ya Sumbawanga kulia.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya
na baadhi ya wahandisi waliosajiliwa na ambao hawajasajiliwa kutoka Mkoa wa Rukwa (nyuma waliosimama) muda mfupi
baada ya kuapishwa.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katikati na baadhi ya
wananfunzi waalikwa katika hafla hiyo kutoka Shule ya Sekondari Mazwi ambao wanasomea masomo ya sayansi. Aliwaasa wanafunzi hao kutoogopa masomo ya sayansi, kufanya kazi kwa bidii na kuwa ili kufikia aslimia 50/50 katika ngazi za maamuzi ni muhimu wanawake kusoma masomo ya fani zote ikiwemo uhandisi ili kuongeza ajira zenye tija kwa wanawake na kipato cha familia na sauti za maamuzi kwa ujumla.
Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa(Rukwareview.blogspot.com)
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa(Rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment