Saturday, May 24, 2014

MH. MOHAMMED DEWJI AKIWA KATIKA ZIARA YA KUKAGUA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO YA JIMBO LAKE

DSC_0073
MO akisalimiana na wazee wa kijiji cha Uhamaka kabla ya kuanza kuzungumza na wananchi.
DSC_0094
MO akisalimiana na mmoja wa watoto waliofika kwenye mkutano wake Uhamaka.
DSC_0086
Mbunge MO akilakiwa na mmoja wa bibi kizee aliyefika kwenye mkutano wake , Karibu mjukuu wangu hapa Uhamaka.
DSC_0107
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO), akiweka saini kwenye kitabu cha ofisi ya kijiji cha Uhamaka Manispaa ya Singida wakati akiwa kwenye ziara ya kiazi ya siku moja kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika jimbo hilo, kulia ni diwani wa kata hiyo na Shaban Kiranga. Kushoto ni mjumbe wa NEC Manispaa ya Singida, Hassan Mazala.
DSC_0184
Diwani wa Kata ya Uhamaka CCM, Kiranga akimkaribisha Mbunge MO, Katani kwake kujionea ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili sekondari ya Kata hiyo.
DSC_0198
Afisa Mtendaji wa Kata ya Uhamaka akisoma taarifa ya ujenzi huo.
DSC_0220
Mbunge Dewji akizungumza na wananchi wa kijiji cha Uhamaka wakati wa mkutano wake wa kutembelea jimbo hilo.
DSC_0111
Sehemu ya umati wa Kinamama na watoto wa kijiji cha Uhamaka Manispaa ya Singida wakimsikiliza Mbunge wao.
DSC_0119
Kikundi cha Ngoma na Kwaya ya kijiji cha Uhamaka wakiimba wimbo wa kumkaribisha Mbunge wao Mohammmed Dewji (MO).
DSC_0243
Mjumbe wa NEC Manispaa ya Singida, Hasan Mazala akizungumza kwenye mkutano huo.
DSC_0177
Vijana nao walihudhuria mkutano wa Mbunge wao MO katika kijiji cha Uhamaka.
DSC_0278
: MO akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari ya Uhamaka.
DSC_0274
DSC_0287
Sheikh wa msikiti wa kijiji cha Ititi akimkaribisha MO.
DSC_0294
Sehemu ya Msikiti wa kijiji cha Ititi ambapo MO aliguswa na kuwachangia mifuko 30 ya Saruji na Mabati 30 kwa ajili ya kuedeleza ujenzi wao.
DSC_0344
MO akishiriki kucheza ngoma ya Kinyaturu.
DSC_0380
Viongozi wa kijiji cha Uhamaka wakiwa ofisini kwao na Mbunge MO .
DSC_0387
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ititi, Jumanne Ivanga akisoma taarifa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ititi kwa Mbunge MO.
DSC_0404
MO akihutubia wananchi wa kijiji cha Ititi, pia aliahidi kutoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo.
DSC_0425
“ Kwa hiyo mimi kama Mbunge wenu nitatoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huu sawa jamani.” Alisisitiza MO huku akishangiliwa na wananchi hao.
DSC_0449
DSC_0433
Kinamama wa kijiji cha Uhamaka wakimshangilia Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho jana.
DSC_0454
Sehemu ya viongozi wa dini na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ititi wakimsikiliza mbunge wao.
DSC_0468
Jamani mmeona utekelezaji wa ilani ya CCM..??? Ni maneno ya MNEC Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ititi.
DSC_0473
Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
DSC_0488
Mh. Mohammed Dewji akimsikiliza MNEC Hassan Mazala.
DSC_0522
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ititi Jumanne Ivanga akimwonyesha Mbunge Mh. Mohammed Dewji sehemu ambapo Zahanati hiyo itajengwa.
DSC_0526
Muonekano wa sehemu ya Zahanati ya Kijiji cha Ititi itakapojengwa.
DSC_0537
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO), akisalimiana na viongozi wa kijiji cha Unyianga mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kijiji wakati wa ziara jimbo kwake.
DSC_0557
MO akicheza na baadhi ya wanakikundi wa uhamasishaji kwenye hafla hiyo.
DSC_0565
MO akisikiliza mashairi kutoka kwa kijana Masoud Mkari mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kijiji wakati wa ziara jimbo kwake.
DSC_0581
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Unyianga, Ramadhani Mpondo akisoma taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa Sekondari ya kijiji hicho mbele ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini.
DSC_0607
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO), akizungumza na wapiga kura wake kuhusu mchango wake katika ujenzi wa shule hiyo inayojengwa kwa nguvu za wanakijiji pamoja na mfuko wa jimbo la Singida Mjini ambapo ameahidi mifuko 100 ya Saruji pamoja na Mabati 100.
Ujenzi wa mradi wa Sekondari ya Kijiji cha Unyianga ulibuniwa na Halmashauri ya kijiji na kuafikiwa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa kijiji baada ya kubaini changamoto nyingi zinazohusu wanafunzi wanaoendelea na masomo sekondari ya kata ya Mwankoko ikiwa ni umbali uliopo kati ya Unyianga na Mwankoko takribani Kilometa 18 kwenda na kurudi, hali inayowalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu na hivyo kuchoka na kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo.
DSC_0586
Baadhi ya wanakijiji wa Unyianga wakimsikiliza Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji.
DSC_0589
DSC_0622
MNEC wa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akiwahamisha wananchi kushiriki kuchangia shughuli za maendeleo.
DSC_0653
Mh. Mohammed Dewji akipata picha ya pamoja na wapiga kura wake.
DSC_0656
Mh. Mohammed Dewji akikagua mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kijiji wakati wa ziara ya jimboni kwake.
20140523_181746
Mh. Mohammed Dewji, akifurahi na watoto walipomwambia wanampenda sana wangetamani kuwa kama yeye.

No comments: