Saturday, May 24, 2014

CCBRT, Vodacom Foundation na UNFPA kusaidia kampeni za kukuza uelewa wa jamii wa kupambana na fistula

Baadhi ya wakazi wa Tandika sokoni jijini Dar es Salaam,wakisoma vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo linalowasumbua wanawake kuwa linatibika kwa ushirikiano wa wadau wa CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani.
Mmoja wa wasanii wa kundi la “Mpoto Theater”akigawa vipeperushi kwa Mariam Khamis vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo linalowasumbua wanawake kuwa linatibika kwa ushirikiano wa wadau wa CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani.
Wakazi wa Mbagala mwisho jijini Dar es Salaam Bi.Fatuma Ali(kushoto)na Khadija Rajabu wakiwa wakionesha vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo linalowasumbua wanawake kuwa linatibika. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani na ratibiwa na CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.
Kikundi cha wasanii wa muziki wa kiasili cha “Mpoto Theater”wakitumbuiza na kuonesha vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo linalowasumbua wanawake kuwa linatibika. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani,zilizoandaliwa na CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.
Msaani wa muziki wa kugani Mrisho Mpoto akitoa elimu kwa wakazi wa Mbagala rangi tatu kwa njia ya kugawa vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo linalowasumbua wanawake kuwa linatibika. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani na ratibiwa na CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.
Wafanyabiashara ndogondogo wa Mbagala rangi tatu jijini Dar es Salaam Abdalla Juma(kushoto) Albart Mhogo(kulia)wakisoma vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo linalowasumbua wanawake kuwa linatibika. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani na ratibiwa na CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.

Katika maadhimisho ya pili ya siku ya kutokomeza fistula ya uzazi duniani, mabalozi 100 wa kijamii wataendesha warsha za wazi kueneza ujumbe “Fistula Inatibika”

Leo Mei 23, 2014 mabalozi 100 wa CCBRT  wataendesha mafunzo ya wazi sehemu mbalimbali nchini yenye lengo la kuzijengea jamii uelewa kuhusu fistula na kuwataka wanawake wenye matatizo hayo kujitokeza kupata matibabu. Wiki iliyopita, mabalozi 100 kutoka mikoa 25 Tanzania walihudhuria mafunzo ya namna bora ya kuendesha simian hizo za kijamii kwa mafanikio pamoja na kuwezeshwa vifaa vya kazi tayari leo kwa sauti moja iliyoungana watu hao 100 wanasambaza ujumbe wa “Fistula inatibika.”

Juhudi hizi ni matokeo ya ushirikiano kati ya CCBRT na wadau wake ambao wote kwa pamoja wameweka azima ya dhati ya kupambana na fistula na kumaliza tatizo hilo hapa nchini. 

Akizungumza jijini Dar es salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Erwin Telemans alisema “ Maelfu ya wanawake sehemu mbalimbali hapa nchini wanaishi maisha ya aibu na kutengwa kutokana na kusumbuliwa na fistula bila kufahamu kwamba CCBRT na wabia wake wanatoa matibabu bure ikiwa ni pamoja na kubeba gharama zote za usafiri wa wagonjwa kufika Dar es salaam,malazi na chakula. 

Mabalozi wetu wa kijamii wapo katika nafasi nzuri ya kuwafikia wanawake hao na kimisingi katika kipindi cha mwaka mzima wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya kuwafikisha kwetu wanawame hao kwa matibabu. Leo tunawaomba wachukue hatua za ziada na tunaimani kuwa wakiwa na nguvu mpya katika mikakati yetu ya kueneza ufahamu kwa jamii kuhusu fistula watawashawishi wanawake wengi zaidi  kutoka mafichoni.”

Mtandao wa mabalozi wa CCBRT hutumika kuwabaini na hatimae kuwasafirisha wanawake wenye tatizo la fistula kwa ajili ya matibabu. Pindi balozi wa fistula anapombainisha na kumthibitisha mgonjwa hufanya mawasiliano na CCBRT kupitia nambari maalum ambayo ni bure kwa wateja wote wa Vodacom na baada ya hapo CCBRT hufanya utaratibu wa kutuma fefha za nauli zinazotumwa kwa njia ya M-pesa na hapo mwanamke mwenye fistula huanza safri kuelekea CCBRT Dar es salaam au kwenye moja ya hospitali zinazofanya nazo kazi ya Kigoma, Arusha na Moshi.

Kwa kila mgonjwa mmoja anaefikishwa hopsitali balozi wa CCBRT hupata Sh 10,000/- kama motisha kwa kusaidia kumaliza tatizo la fistula Tanzania.

Kwa sasa mtandao wa mabalozi wa fistula unafikia mabalozi 500 wanaofanya akzi kwa utaratibu w akujitolea  wakifikisha hopsitali wagonjwa wapatao 2,000

“Kutumika kwa tekonolojia ya Vodacom kumesaidia kupunguza vikwazo kwa wanawake wanaotafuta matibabu na ni moja kati ya ubunifu mkubwa kwenye sekta ya afya kuwahi kushuhudiwa hapa Tanzania. Urahis wa kutumia huduma za kifedha za simu ya mkononi umeokoa heshima ya maelfu ya wanawake walio masikini na waliotengwa hapa nchini kwa sababu tu ya fistula. “Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw Rene Meza na kuongeza

“Ubia wa Vodacom Foundation na CCBRT umekuwa ukiimarika siku hadi siku na tunajivunia kufanya kazi na wabia wetu mahiri katika kuadhimisha siku moja ya juhudi zetu pana za kumalzia fistula hapa nchini.”   

Siku ya kimataifa ya kutokomeza fistula huadhimishwa Mei 23 ya kila mwaka kutambua umuhimu wa juhudi za kumaliza tatizo hilo na pia kuonesha nia ya dhati ya Umoja wa Mataifa kwa juhudi zote zinazofanywa za kutibu na kukinga fistula duniani. 


“Kama sehemu ya jamii, tunawajibu wa kumaliza janga hili la kiafya na kiutu, Tunavyoadhimisha siku hii leo,  wote lazima tukubaliane kwamba kumaliza fistula hakuhsu tu upasuaji kwa mgonjwa. Ukweli wa mambo ni kwamba tunaweza kumaliza tatizo hili nchini kwa kuwekeza kimkakati kwenye maeneo matatu ambayo ni kinga, matibabu na kuwarejesha katika maisha ya awali ya kijamii wale waliowahi kuugua na kupona.  


Una mtu mwenye fistula? Ungependa kuwa balozi wa CCBRT? Piga CCBRT (bure kwa wateja wote wa Vodacom) ili kupata taarifa zaidi au kumfikisha hospitalikwa ajili ya matibabu  mwanamke anaegua fistula  0800752227

No comments: