Monday, April 14, 2014

Mhe. Kairuki asimikwa kuwa Kamanda wa UVCCM Same

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Ndg. Sixtus Mapunda akimkabidhi Mhe. Angellah Kairuki (MB), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, nyenzo za vitendea kazi za kimila wakati wa kusimikwa kuwa Kamanda wa UV CCM wa Wilaya ya Same.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Ndg. Sixtus Mapunda akimweleza majukumu ya Kamanda wa Vijana Mhe. Angellah Kairuki kabla ya kusimikwa kuwa Kamanda wa UV CCM wa Wilaya ya Same.
Mhe. Kairuki akila kiapo cha Kamanda Mpya wa UVCCM wa Wilaya ya Same wakati wa kusimikwa kwake kuwa kamanda wa umoja hu huku akisikilizwa kwa makini na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjanro na Wilaya ya Same waliokuwepo katika sherehe hizo.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Same wakimvalisha mgolole Mhe. Angellah Kairuki kuashiria kwamba amsimikwa rasmi kuwa Kamanda wa UVCCM wa Wilaya ya Same.
Kamanda Mpya wa UV CCM wa Wilaya ya Same, Mhe. Kairuki akitoa hotuba yake mara baada ya kusimikwa.
Mhe. Kairuki ambaye ni Kamanda Mpya wa UV CCM wa Wilaya ya Same akicheza ngoma za kimila pamoja na wakereketwa wa CCM wa Wilaya ya Same mara baada ya kusimikwa.
Mhe. Kairuki, Kamanda Mpya wa UV CCM wa Wilaya ya Same akipokea cheti cha heshima kutoka kwa mgeni rasmi ndg. Sixtus Mapunda baada ya kusimikwa
Kamanda Mpya wa UVCCM wa Wilaya ya Same, Mhe. Kairuki akiwa katika picha ya pamoja viongozi wa CCM na baadhi ya wawakilishi wa Timu mbalimbali za Wilaya ya Same waliopokea zawadi za jezi na mipira kutoka kwake mara baara ya kuapishwa kuwa Kamanda wa CCM Wilaya ya Same.
Mhe. Kairuki ambaye ni Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Same akipadisha bendera ya CCM katika mojawapo ya Mashina ya chama cha Mapinduzi Wilayani Same mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda.
Mhe. Kairuki (Kamanda mteule wa UVCCM Wilaya ya Same) akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Chama Wilayani Same wakiwa katika safari ya kufungua mashina mbalimbali ya CCM katika Wilaya ya Same.
Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia kwa makini tukio ya kumsimika Mhe. Kairuki (Hayupo pichani) kuwa Kamanda wa UVCCM wa Wilaya wa Same.
Hivi ndivyo wananchi na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Same walivyomkaribisha na kumpokea Mhe. Angellah Kairuki Kamanda Mpya wa UVCCM wa Wilaya hiyo.

No comments: