Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Ndugu Betty Mkwasa mara baada ya kuwasili mjini Bahi kushiriki mkwenye sherehe ya uzinduzi wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi tarehe 14.4.2014.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akiwapungia wanafunzi na wananchi wa Bahi waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa saratani ya shingo ya kizazi mjini hapo tarehe 14.4.2014.
Mama Salma Kikwete akipokewa kwa shangwe
Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa Macho wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Frank Magupa, wakati alipotembelea maonesho ya kitabibu yaliyofanyika sambamba na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa wilayani Bahi tarehe 14.4.2014.
Mamia ya wananchi wa Bahi wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na viongozi wa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi iliyofanyika huko Bahi, Mkoani Dodoma
Mamia ya wananchi wa Bahi wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na viongozi wa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi iliyofanyika huko Bahi, Mkoani Dodoma
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Kebwe Staphen Kebwe akitoa salamu hotuba kwa niaba ya wizara ya Afya wakati wa uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi huko wilayani Bahi.
Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Bahi muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi kampeni ya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma
Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Bahi muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi kampeni ya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma
Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa Wilaya ya Bah
Mama Salma Kikwete akionyesha vifaa mbalimbali vinavyotumika na madaktari wakati wa kuwapima wanawake ili kufahamu kama wana maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo wilayani Bahi
Mama Salma Kikwete akijumuika na wacheza ngoma na wananchi mbalimbali wa wilaya ya Bahi mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa akinamama.
Kwaya ikitoa burudani
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) Bwana Hamis Mwege kwa kazi kubwa ya kuelimisha umma kuhusu kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake hapa nchini. Vyombo vingine vilivyopata cheti ni Channel Ten na ITV.
Mama Salma Kikwete akiwapungia wanafunzi na wananchi wa Bahi waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa saratani ya shingo ya kizazi Picha na John Lukuwi
No comments:
Post a Comment