Tuesday, April 15, 2014

KINANA AWAOMBA RADHI WANANCHI WA KAREMA

  • Awaomba radhi wananchi wa Karema kwa kuchelewa kukamilika kwa mradi wa bandari ambao umesimama kabisa baada ya mkandarasi aliyepewa mradi huo kushindwa kuumaliza .
  • Asikitishwa na watumishi wengi wa serikali kuendeleza tabia ya umangi meza kwani miradi mingine inasimama kwa kipindi kirefu kwa sababu kuna kiongozi wa serikali amechelewa kujibu barua itakayofanikisha mradi kuendelea na kumalizika kwa wakati.
  • Asisitiza Viongozi na wana CCM kuwa wakali katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kusema si vyema tusubiri wapinzani waseme ,tunayaona matatizo inabidi wana CCM wayasemee wenyewe na si vinginevyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kapalamsenga wilayani Mpanda mkoani Katavi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Kapalamsenga ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM inazidi kuimarika na kuzidi kuaminika kwa wananchi siku hadi siku .




 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungmza mbele ya waandishi wa habari kwenye eneo lililopaswa kujengwa bandari ya Karema baada ya kujionea mradi wa ujenzi wa bandari ya Karema ulivyosimama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia majengo yaliyokuwa yameenza kujengwa kisha mradi wa ujenzi wa bandari kusimama kwa muda mrefu,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya siku tatu mkoani Katavi ambapo moja ya shughuli atakazofanya ni kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kujenga na kuimarisha Chama.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye , Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk. Rajab Rutengwe wakikagua mradi wa Ujenzi wa Mwalo uliopo kijiji cha Ikola.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mbunge wa Mpanda Vijijini Ndugu Moshi Selemani Kakoso wakati wa kukagua mradi wa ujenzi wa Mwalo katika Kijiji cha Ikola ambao utasaidia kuongeza thamani ya samaki,mradi huu una thamani wa zaidi ya millioni 700.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi mkubwa wa soko la Samaki (Mwalo),ambao imeelezwa kuwa utapunguza umaskini kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo. Hata hivyo imeelezwa kuwa mradi huo wa soko na kuhifadhia samaki umechelewa kukamilika na kupitisha miaka miwili ya zaidi ya muda ulipangwa kwenye mkataba,Kinana amewahidi Wananchi kuwa atalifuatilia tatizoo hilo na kuhakikisha mradi huo unakamilika kama ilivyoahidiwa.Eneo hilo la kisasa kabisa litatumika kuongeza thamani ya samaki. 
 Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,akiuliza swali la zahanati na ,Elimu na Barabara kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana (pichani kulia),alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi mkubwa wa Samaki (Mwalo). 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishirikii ujenzi wa mradi wa soko la samaki (Mwalo),katika kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,
 Kinana akipata maelezo mafupi kuhisiana na eneo la soko hilo la kukaushia samaki na dagaa
 Ndugu Kinana akikaribisha kwa balozi.
 Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakiwa wameketi kwa balozi wa shina namba 2,tawi la Ikolasto katika kijiji cha Ikola,Wilayani Mpanda jioni ya leo mkoani Katavi.
  Ndugu Kinana akizungumza na wajumbe wa shina namba 2 (hawapo pichani),tawi la Ikolasto katika kijiji cha Ikola,Wilayani Mpanda jioni ya leo mkoani Katavi.
 Wajumbe wa tawi la Ikolasto wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.(hayupo pichani). 
Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso, akijibu na kutoa taarifa  mbalimbali kuhusiana na jimbo lake katika suala zima la kutekeleza na kuhumiza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,mbele ya wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
 Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo,katika mkutano wa hadhara,Kinana alijikuta akigeuka mbogo na kuwaomba radhi wakazi wa kata ya Kirema, Ikola na Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi, baada ya kubaini kuwa,kumekuwepo na kutowajibika kwa baadhi ya watendaji wa Serikali.Kinana amesema chama chake kamwe hakitowavumilia watendaji wanaoendekeza vitendo vya urasimu na umangimeza wa kutumia makaratasi ofisini badala ya kuwatumikia wananchi kwa kuwajibika ipasavyo.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia kwa ufupi wakazi wa mji wa Karema mkoani Katavi usiku huu mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Kigoma kwa boti na kusafiri nayo ndani ya ziwa Tanganyika takribani kwa masaa kumi na manne.Kutokana na safari hiyo kuwa ndefu ya majini,inaelezwa kuwa kuna baadhi ya Watu wamedai msafara wa Katibu Mkuu huyo,Kinana umepotewa ziwa la Tanganyika,jambo amabalo si la kweli na la kizushi.PICHA ZOTE NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-KATAVI
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwapungia wenyeji wake (hawapo pichani) waliofika kumpokea usiku huu kwa boti akitokea mkoani Kigoma  katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne.Kinana pia alipata nafasi ya kupita ufukweni mwa ziwa Tanganyika na kukutana na baadhi ya wavijiji kuwasilikiliza matatizo yao.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanal Mstaaf Issa Machibya akishuka kwenye boti usiku huu kwenye bandari ya Karema mkoani Katavi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,na Viongozi wengine wa Taifa,Mkoa na Wilaya tayari kwa kuanza ziara ya siku nne mkoani Katavi. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuka kwenye boti wakati wenyeji wake (hawapo pichani) walipokuwa wakimsubiri kumpokea usiku huu akitokea mkoani Kigoma  katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa na Wilaya ndani ya Mkoa wa Katavi usiku huu,alipokuwa akiwasili kwenye bandari ya Karema mkoani humo usiku huu.Kinana ameongoza na Katibu Wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye,Mjumbe wa NEC,Balozi Ali Karume,Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanal Issa Machibya,Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Kigoma ndugu Kabouru na wengineo.
 Kinana akipokelewa na Gwaride la chipukizi usiku huu ndani ya mkoa wa Katavi.





















No comments: