Friday, February 21, 2014

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI WA ZANZIBAR MHE. ALI JUMA SHAMHUNA AFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI OMAN

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa serikali ya Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna, alifanya ziara ya Kikazi nchini Oman kuanzia tarehe 16 hadi 20 February 2014 kwa Mwaliko wa mwenyeji wake Mheshimiwa Dr. Rawiyah Al Busaidi, Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman.

Ziara hii ilikuwa na madhumuni makuu ya kuimarisha uhusiano wa kindungu uliopo baina ya Oman na Tanzania kupitia sekta ya Elimu na kuimarisha uhusiano wa karibu na ushirikiano baina ya taasisi za elimu kati ya Tanzania na Oman.

Katika ziara hii Mhe. Ali Juma Shamhuna alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Dr. Rawiyah Al Busaidi ambapo pia walitia saini nyongeza katika Mkataba wa Mashirikiano katika Elimu ya Juu baina ya Zanzibar na Oman . Mheshimiwa Waziri Shamhuna pia alikutana na Waziri wa Elimu wa Oman Mheshimiwa Dr. Madihana Ahmed Al Shibaniya na Waziri wa Kazi wa Oman Mheshimiwa Abdullah Nassor Al Bakri, .

Mbali na kukutana na viongozi hawa wa Oman, Mheshimiwa Waziri Shamhuna alipata nafasi kutembelea maeneo kadhaa kujonea shughuli mbalimbali za Taasisi zinazoshughulika na elimu za Oman, alitembelea makumbusho ya Jeshi la Oman, Chuo cha Ufundi na Teknolojia, chuo kikuu cha Sultan Qaboos na Baraza la Taifa la Utafiti.

Katika maeneo yote aliyotembelea Mheshimiwa Waziri Shamhuna alifurahishwa sana na shughuli za taasisi za elimu Oman na kuridhika na hatua iliyopigwa na Oman katika sekta ya Elimu na mafunzo ya Amali. Mheshimiwa Waziri Shamhuna pia alitembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Oman kujionea shughuli mbalimbali za Ubalozi na pia kuhudhuria hafla ya chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa heshima yake nyumbani kwa Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna mara alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Muscat kuanza Ziara ya kikazi nchini Oman, kushoto ni Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi, wa kwanza kulia ni Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna wa pili kutoka kushoto akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi, wa pili kulia , wa kwanza kushoto ni Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhunawa tatu kulia akiongoza ujumbe wa Zanzibar katika mazungumzo na Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi akiongoza ujumbe wa Oman Kushoto , wa nne kushoto ni Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna kushoto na Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi wakitia saini nyongeza katika mkataba wa ushirikiano wa Elimu ya Juu baina ya Oman na Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna kushoto akiwa katika Mazungumzo na Waziri Kazi wa Oman kuhusu ushirikiano katika sekta ya mafunzo ya amali.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna kushoto akiwa na Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh kulia , Balozi wa Tanzania nchini Oman alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Oman pichani chini maafisa wa ubalozi na ujumbe wa mheshimiwa waziri wakifuatilia mazungumzo.

No comments: