Friday, February 21, 2014

CRDB YATOA SOMO KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ZAIDI YA 1000 KUHUSU KUWEKA AKIBA

Zaidi ya wajasiriamaili wanawake 1000 kutoka katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamepata mafunzo ya kuwajengea uwezo wakati wa tamasha la Mwanamke na Akiba, 2014 lililofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala.

Akizungumzia Tamasha hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, Naima Malima alisema kuwa lengo la semina hiyo ni kuchochea utamaduni wa kuweka akiba kwa wanawake wajasiriamali na kuwaelimisha aina tofauti ya kuweka akiba.

Aidha Naima aliongeza kuwa pia itachoche kuwakomboa wanawake toka kwenye lindi la umaskini kupitia uwekaji wa akiba, uwekezaji wa kuongeza kipato, pia kuongeza wanawake katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

"Kupitia semina hii wanawake wataweza kupata njia bora za kuwawezesha kuweka akiba kwa muda mfupi, mudac wa kati na muda mrefu"

Tamasha hilo lilidhaminiwa taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo, Benki ya CRDB, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). PSPF,  SS Bakhresa, GEPF, Stanbic Bank, Convenant Bank, K-Finace, UTT, Montage, HSC, Minjingu Mazao, Dar Live, Afrcan Real Estate na ETG Group.

Kupitia tamasha hilo wadhamini walipata fursa ya kujitangaza na kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao kwa wanawake wa Kitanzania.
 Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB tawi la Mbagala, Mohamed Madengelo akitoa mada wakati wa Tamasha la Wanawake na Akiba 2014 lililoandaliwa na Kampuni ya Angels Moment  kwa ajili ya kuwajenga uwezo wanawake wajasiriamali na kufanyika jijini Dar es Salaam. Benki ya CRDB ilikuwa moja ya wadhamini wa tamasha hilo. 
 Baadhi ya akinamama wakifuatilia mada wakati wa Tamasha la Wanawake na Akiba 2014 lililowashirikisha wanawake wajasiriamali kutoka maeneo ya Mbagala na vitongoji vyake. 
 Tumekuja kupata elimu ua ujasiriamali................
 Tunapata elimu ya ujasiriamali.......
 Mkurugenzi Mkuu wa Angels Moment, Naima Malima (kushoto), akifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa tamasha la wajasiriamali wanawake jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Kampuni ya Angels Moment kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima akizungumza wakati wa semina hiyo.

No comments: