Thursday, February 20, 2014

Whatsapp yanunuliwa na Facebook, nini tutegemee

Kama ulikuwa haufahamu, habari kuu katika ulimwengu wa Teknohama kwa siku ya leo ni Facebook kuinunua Whatsapp kwa bei ya dola bilioni 19.  Nunuzi hilo ni la programu pekee na siyo kampuni ingawa wafanyakazi wa whatsapp watajiunga na timu ya Facebook moja kwa moja, mission za whatsapp zitaendelea kubaki kama zilivyo, alieleza Jan Koum ambaye ni muanzilishi wa whatsapp.

Kwa wasio fahamu, whatsapp ni moja ya programu ya simu za mkononi inayokuwezesha kutuma ujumbe wa simu kupitia kwenye intaneti badala ya ujumbe mfupi (sms). Kwa kutumia whatsapp, inamaana utaepuka gharama za sms huku ikiwa imesheheni matumizi mengine mengi zaidi kama kutuma picha, sauti uliyojirekodi nk.

Hadi sasa, whatsapp ina watumiaji hai milioni 450 kila mwezi kutoka nchi nyingi duniani, huku kukiwa na watumiaji wapya zaidi ya milioni moja kila siku. Hivyo, ni dhahiri kuwa whatsapp ni programu pendwa na yenye kutumika.

Whatsapp inaweza kutumika kama njia rahisi zaidi ya mawasiliano kwa watu binafsi na hata makampuni, kwa mfano, sisi Dudumizi tunatumia whatsapp kama njia ya kuwasiliana na mamia ya wateja wetu walio nje ya nchi na kutuwezesha kupunguza gharama za mwasiliano.

Ingawa makampuni mengi ikiwemo Facebook yamekuwa yakitegemea huduma za matangazo kama njia ya kuingeza kipato, whatsapp ni programu ambayo, huwezi kuonana na matanagazo na wamejizatiti kuwa ni wataendelea hivyohivyo bila ya matangazo. Na pia whatsapp ni bure kwa kwa mwaka wa kwanza na huchaji $1 kwa mwaka kama gharama ya kujiunga kwa miaka inayofuata. Hivyo kabla ya Facbook kuinunua whatsapp ni dhahiri walishajipanga kwenye hili, kwani, hili ndilo linaloifanya whatsapp iwe tofauti.

Akielezea sababu ya kuinunua whatsapp, mwanzilishi wa Facebook alisema, wameinunua whatsapp kwa sababu whatsapp ina thamani. Na wao wakiwa kama wafanya biashara lengo lao kubwa ni kuongeza thamani ya biashara yao illi waendelee kuwa salama. Hivyo, wanaamini nunuzi la whatsapp litakuwa na tija na manufaa kwa wote, wanunuzi na walionunuliwa. Hivyo ubora na misingi ya huduma ya whatsapp utaendelea kuwa juu kama ilivyo sasa.

Lakini, dili hili la kuinunua whatsapp halikuja ghafla, bali limekuja kwa kuangalia muelekeo na mabadiliko ya watumiaji wa mtandao. Taarifa zinaonesha kuwa, asilimia zaidi ya 52% ya watumiaji wa mtandao kwa sasa ni wale wanaotumia simu. Na pia matumizi ya email kama njia ya mawasiliano yamezidi kupunguasiku hadi siku. Na siku zinavyozidi kwenda mbele inamaanisha idadi hii itakua. Pia, kwenye uwanja wa ujasiriamali, unatakiwa kuishi kwa kuyachunga mazingra na siyo kuomba dua mambo yasibadilike, hivyo ununuzi huu umekuja ili kuhakikisha Facebook inakuwa na udhibiti wa mazingira ya watumia intaneti na mtandao.Kitendo cha Facebook kuinunua whatsapp, kinaiwezesha kujikita zaidi kwenye kundi kubwa la watumiaji wa intaneti ambao wengi ni vijana.

Kwakuwa watumiaji wengi wa whatsapp ni wa kwenye simu, na kwakuwa yao ni moja ya programu zenye mamilioni ya watumiaji, hivyo kuimiliki whatsapp inamaanisha kumiliki hisa kubwa kwenye soko la watumiaji hao. Na hii itaiweka Facebook katika hali ya kudhitibi soko. la intaneti na mitandao jamii. Facebook pia watapata njia wa kuwafikia watumiaji hawa moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa instagram, hivyo hii ni moja nunuzi lenye faida kwao.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza, je kitendo za Facebook kuinunua whatsapp kina faida yoyote kwa kampuni? na nini sisi watumiaji wa whatsapp tutegemee? Kutokna na sababu nilizozitaja juu (thamani), hivyo ni yumkini kabisa, Facebook wanaweza kufanya kati ya vifuatavyo.

1. Kuiunganisha whatsapp moja kwa moja na Facebook.
Ikumbukwe kuwa, whatsapp itaendelea kuwa whatsapp, hivyo usifikiri kwamba kesho hakutakuwa na whatsapp bali watumiaji wote watapelekwa Facebook, la , ila whatsapp itakuwa na ushirikiano wa kiutendaji na Facebook na kuzifanya ziwe imara zaidi. Ila, ili whatsapp iunganishwe na facebook, ni dhahiri kuwa whatsapp lazima ifanyiwe maboresho na kuongezewa baadhi ya matumizi ambayo yataiwezesha kuiunganisha moja kwa moja na Facebook, isiishie kwenye mawasiliano tu. Kunatakiwa kuongezwe / boreshwa zaidi zile huduma ya kijamii.


Kwa mfano, tutegemee kuwa na uwezo wa kutuma visasisho(updates) ambavyo vitaonekana kwenye Facebook yako. Hii itaipe ya maisha yako hapohapo kwenye whatsapp. Hii itaipeleka whatsapp kufanana sana na moja ya mtandao unaofanya kazi zake kama whatsapp unaoitwa Wechat.Huu ni mtandao uliofanikiwa sana kwa China.


2. Kutafuta / alika marafiki wa facebook kwa kutumia namba za simu na siyo email pekee
Facebook ilipoanza, ilikuwa inategmea sana email kama njia ya kutafuta marafiki, ila kadri siku zinavyozidi kwenda, matumizi ya email kama njia ya mawasiliano ya kawaida yamekuwa yakipungua, hivyo kutegemea email kunaiweka facebook kwenye kikomo cha kutanuka. Kwakuwa whatsapp inatumia namba za simu, na kwakuwa facebook imeinunua whatsapp, basi tutegemee kuwa kutakuwa na uwezo kwa watumiaji wa Facebook kuwaalika watu wajiunge na facebook kwa njia ya ujumbe wa simu, na hii itaunganishwa vyema kwa kutumia whatsapp.


3. Kuongezwa huduma zaidi ambazo ni za kulipia.
Kwakuwa lengo la kuwekeza ni kuongeza kipato.Iwe moja kwa moja au la, ni dhahiri kuwa facebook watakuja na njia zitakazowawezesha kuongeza kipato kwa kutumia whatsapp, hivyo kutakuwa na huduma zaidi ambazo si za lazima, ila kama utazihitaji, basi utatakiwa kulipia kiasi fulani. Hii ni moja ya njia zinazotumika kipindi unaandaa bando la huduma.


Hivyo,kwa watumiaji wa Facebook na Whatsapp, tutegee mambo mengi zaidi.

Usipitwe na chambuzi/ habari za Teknohama zenye mlengo wa Kitanzania, Jiunge Facebook Fan Page yetu. www.facebook.com/dudumizi

Mkata Nyoni (ITIL)
Dudumizi Technologies Limited

No comments: