Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (Kati kati) akiongoza Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma
Katibu wa Chama cha Walimu Bw.Ezekiel Oluoch akitoa mchango wake mkutano huo
Katibu wa TUGHE Bw. Ally Kiwenge akitoa maoni yake katika mkutano.
Mjadala ukiendelea
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome akijitambulisha kwa wajumbe wa mkutano ika mkutano. |
Moja kati ya mada zilizowasilishwa katika mkutano kuhusu muundo wa utumishi wa walimu unaotumika hivi sasa.
Katibu wa Sekretariati ya Ajira bw. Xavier Daudi akitoa mchango wake katika mkutano.
Katibu wa Bodi ya Mishahara Bi. Tamika Mwakahesya akitoa mchango wake katika mkutano.
Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma imeitisha Mkutano
maalum wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma ili
kupata mrejesho kuhusu masuala yanayowagusa watumishi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.
George D. Yambesi akifungua mkutano huo mjini Dodoma amesema
mkutano huo maalum unafuatia maagizo yaliyotolewa katika mkutano
uliopita.
“Kati ya yale yaliyosisitizwa na kukubalika ni kuitisha Mkutano Maalum
wa Baraza kwa ajili ya kujadili Muundo wa Maendeleo ya Utumishi wa
Walimu na masuala mengine muhimu yanayohitaji ushauri wa Baraza”
Bw. Yambesi alisema.
Bw. Yambesi, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo alisema baraza
limeundwa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha sheria ya
Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa Umma, Na. 19 ya mwaka
2003, ambapo jukumu lake kubwa ni kuishauri Serikali kuhusu masuala
mbalimbali yanayohusu ustawi wa watumishi wa umma ikiwa ni pamoja
na utumishi wao. Utumishi wa Umma unasimamiwa na sheria, Kanuni
na Taratibu mbalimbali. Hivyo, Baraza linao wajibu wa kushauri kuhusu
miongozo mbalimbali inayosimamia Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu Bw. Yambesi alisema serikali inapenda kupata maoni
ya wajumbe wa baraza kuhusu Tathmini ya utekelezaji wa Waraka
wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 1 wa mwaka 2000 unaohusu
watumishi wa umma kujiunga na Siasa.
Alifafanua kuwa kwa sababu tunatarajia kuwa na uchaguzi wa
Serikali za Mitaa mwakani na huenda baadhi ya watumishi wa Umma
wakapenda kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa ambapo utaratibu
uliopo sasa uliandaliwa miaka kumi na tatu (13) iliyopita, hivyo kuwepo
umuhimu wa kupima kama bado unakidhi matarajio.
Pamoja na wajumbe wa baraza, katika mkutano huo maalum
ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka mifuko ya Hifadhi ya Jamii na
Taasisi mbalimbali ndani ya Utumishi wa Umma.
No comments:
Post a Comment