Tuesday, December 17, 2013

UZINDUZI WA KITUO CHA AFYA KAJENGWA MAKUNDUCHI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Daktari dhamana Wilaya ya kusini (DMO) Daniel Francis Pius,(katikati) baada ya kukifungua
kituo cha Afya Kijiji cha Kajengwa Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja jana,katika shamra shamra  kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
 Wasoma Utenzi Amina Makame Omar,na Marium Amour Haji,kutoka Shehia ya Kijini,walipokuwa wakitoa burudani hiyo kwa wananchi wakati wa  ufunguaji  Kituo cha Afya Kijiji cha Kajengwa,Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja jana,katika shamra shamra  kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Katibu wa Kamati ya maendeleo Shehia ya Kajengwa Makunduchi Nassor Simba,alipokuwa akisoma risala ya wananchi wa kijiji hicho wakati wa  ufunguzi wa  kituo cha Afya Kijiji cha Kajengwa,Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja jana,katika shamra shamra  kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
 Baadhi ya Wananchi wa Shehia ya  Kijiji cha Kajengwa Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja,na Vijiji jirani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza nao wakati wa ufunguzi  wa Kituo cha Afya Kijiji hapo,katika shamra shamra   kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk.Saleh Mohamed Jidawi,alipokuwa akitoa Taarifa na shukurani wa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,baada ya kukifungua kituo cha Afya cha Shehia ya Kajengwa  Makunduchi,Wilaya ya Kusini Unguja jana,katika shamra shamra   kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Wafanyakazi wa Kituo cha Afya Kajengwa Makunduchi,Wilaya ya Kusini Unguja,wakiwa sherehe za Ufunguzi wa Kituo hicho,katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,sherehe hizo zilifanyika jana,na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa mgeni rasmi
 Juu na chini: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kajengwa Makunduchi,Wilaya ya Kusini Unguja,jana wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Afya,katika maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

No comments: