Monday, November 25, 2013

BENKI YA CRDB YASHEREHEK​EA SIKU YA FAMILIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa sherehe ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Hoteli jijini Dar es Salaama na kuwashirikisha wafanyakazi wa Benki hiyo pamoja na familia zao. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasirimali Watu wa Benki ya CRDB, Dorah Ngaliga.
Mkurugenzi wa Rasirimali Watu wa Benki ya CRDB, Dorah Ngaliga akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Nahodha wa timu ya Fahari Huduma, Shaban Badi akipokea kombe kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimeia wakati wa sherehe ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Hoteli jijini Dar es Salaam.
Washindi wa mpira wa wavu wakipokea zawadi ya kombe.
Furaha ya ushindi.
Mshindi wa kucheza muziki, Messi Dyama akipokea zawadi pamoja na fedha sh. 100,000 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Wanamuziki wa Skylight band wakiongozwa na Meneja wa bendi hiyo, Aneth Kushala akiimba wakati wa sherehe hiyo.

Watu wengi walijitokeza.
Watoto wakicheza katika bwawa la kuogelea.
Watoto wakiogelea.

Francis Dande 14:06 (1 hour ago) to me, Othman

DAR ES SALAAM, Tanzania

 BENKI ya CRDB imejipanga kupunguza masharti mazito na riba kubwa kwa mwaka ujao wa fedha, ili kuwawezesha wateja wake kukabiliana na changamoto kuu ya ugumu wa kurejesha mikopo utokanao na mdororo wa uchumi, unaokwaza harakati zao.
Hayo yalisema na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk Charles Kimei, alipokuwa akiongea na wanahabari, wakati wa hafla ya Siku ya Familia ‘CRDB Family Day 2013,’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kunduchi Wet ‘n’ Wild.
Dk Kimei alisema kuwa, mdororo wa uchumi ni changamoto kuu miongoni mwa wateja wa CRDB na wajasiriamali kwa ujumla na kwa kulitambua hilo, benki yake imejidhatiti kuhakikisha hawawabebeshi mzigo mzito wateja wao katioka aina tofauti za mikopo.
“Baada ya mdororo wa uchumi wa Dunia, bado hali ya uchumi kwa mataifa mbalimbali haijatulia. CRDB tunalitambua hilo, na tunajua kwamba ni kikwazo kwa wateja kurejesha mikopo kwa wakati, ndio maana tunapanga kulifanyia kazi,” alisema Dk Kimei.
Alisema kuwa, mipango endelevu inafanyika na uongozi wa CRDB ili kuibakisha benki hiyo kama taasisi kinara wa katiika utoaji huduma bora kwa jamii miongoni mwa taasisi za fedha nchini, huku akiwataka Watanzania kuchangamkia huduma zao.
CRDB hutumia ‘Family Day’ ya kila mwaka kunadi bidhaa moja mpya inayotolewa na benki hiyo, ambapo mwaka huu siku hiyo ilipambwa na bidhaa ya Fahari Huduma ‘Ulipo Tupo’ ambayo aliitaja kupata mafanikio katika kipindi kifupi cha uwapo wake.
“Fahari Huduma ni bidhaa iliyo na takribani miezi mitatu, lakini CRDB imeweza kuwa na mawakala 420 nchini kote, wanawawezesha wateja wetu kupata huduma za kibenki kupitia mawakala hao walionea nchini kote,” alisema Dk Kimei.
Aliongeza kuwa, ‘Family Day’ ni siku muhimu, inayowawezesha viongozi kujadiliana na wafanyakazi nje ya vituo vya kazi, ikiwamo kutambuana na kukusanya mawazo kuelekea mwaka ujao, jambo litakalochangia ustawi wa utendaji miongoni mwao.
CRDB Family Day 2013 ilikusanya zaidi ya watu 10,000 pamoja na kushangilia mafanikio ya benki kwa mwaka mzima na kujipanga kwa mwaka ujao, ambapo kila mfanyakazi alitakiwa kufika akiwa na nduguze wasiozidi watano.

No comments: