Monday, October 21, 2013

DK. SHEIN AFUNGUA SEMINA YA WATENDAJI WA CCM, DODOMA

 Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua semina ya mafunzo ya siku nne kwa Watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya nchini, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo, Oktoba 21, 2013. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (zanzibar) Vuai  Ali Vuai. (Picha na Bashir Nkoromo)
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa maelezo kuhusu lengo la mafunzo hayo.
 Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Kartibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuzungumza  kwenye semina hiyo.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma, leo kwa ajili ya kufungua semina hiyo.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili katika ukumbini kwa ajili ya kufungua semina ya mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya, leo kwenye Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa.
 Wajumbe wakishangilia, Dk. Shein alipowasili ukumbini. Washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini
 Wajumbe wakiwa ukumbini
 Wajumbe wakishangilia baada ya semina yao kufunguliwa na Dk. Shein.
 Makatibu wa NEC, Zakiah Meghji (Uchumi na Fedha) na Mohammed Seif Khatib (Oganaizesheni) wakifuatilia kwa makini hali ya mambo ukumbini wakati wa semina hiyo.
Dk. Shein akiwaaga wajumbe na viongozi wengine baada ya kufungua semina hiyo.

No comments: