Tuesday, June 18, 2013

UBALOZI WA TANZANIA WATANGAZA UTALII WA TANZANIA KWENYE USIKU WA SAN DIEGO ZOO

Balozi wa Hiari wa Tanzania Bw. Ahmed Issa akijitambulisha kwenye hafla fupi iliyoandaliwa kwa heshima yake na mabalozi wengine wa hiari watatu na Bw. Richard Rovsek wa taasisi ya Spirit of Liberty mjini San Diego CA tarehe 15 Juni 2013
Bw. Ahmed Issa kwenye picha ya pamoja na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga na Bwana na Bibi Richard and Jerry Rovsek baada ya chakula cha mchana na kumtambulisha Bw. Ahmed kwa washiriki wa biashara na wadau wa utalii jijini San Diego, CA.
Mabalozi wa Hiari wa Botswana - Bibi Diane Neiman, Tanzania - Ahmed Issa, afisa kutoka ubalozi wa Tanzania Mindi Kasiga na Balozi wa Hiari wa Burkina Faso Bw. Allein Neiman kwenye picha ya pamoja na msaidizi wa Bw. Richard Rovsek, Bi. Angela
Juu na chini ni Wawakilishi wa Tanzania kwenye usiku wa San Diego Zoo Gala ama kwa jina jingine R.I.T.Z "Rendezvous In The Zoo 2013. Washiriki hao walipata nafasi ya kutangaza utalii kwa kujibu maswali na kugawa taarifa mbalimbali za utalii Tanzania.

Kwa mara ya kwanza Tanzania imeshiriki kwenye usiku wa San Diego Zoo, Jimboni California kwa kutangaza utalii wa wanyama Tanzania na vitutio vyake tarehe 15 Juni 2013.

Tanzania iliwakilishwa na Balozi wake wa Hiari kutoka jiji la San Francisco, CA Bw. Ahmed Issa na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga ambapo walipata fursa ya kuzungumzia utalii wa Tanzania kwa wageni waliohudhuria na pia kuendeleza mahusiano baina ya San Diego Zoo na Tanzania hususan kwenye upande wa uhifadhi.

Tamasha hili ambalo hufanyika kila mwaka huvutia maelfu ya wadau na washirika wa sekta ya wanyama na utalii wa Marekani na wengi wao hutokea Jimbo la California na vitongoji vyake.

Mwaka huu 2013, ubalozi ulipata mwaliko kutoka kwa mmoja wapo wa waandaji wa tamasha hilo Bw. Richard Rovsek kwa kupitia taasisi yake ya Spirit of Liberty, ambaye alishirikisha (kwa mialiko) baadhi ya nchi ambazo zinatangaza utalii wa wanyama Tanzania, South Africa, Botswana na Kenya.

San Diego Zoo ni mojawapo ya bustani za wanyama kubwa nchini Marekani ambapo ina ukubwa wa hekari za eneo (acres) mia moja (40ha) na inahifadhi aina (species) mia nane za wanyama wapatao elfu nne.

Bustani hii ambayo inashika nafasi ya sita duniani kwa ukubwa wake huandaa tamasha hili maalum kila mwaka ikizawadia washirika wake na kuchangisha pesa kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake hususan zile za uhifadhi na elimu kwa umma.

Kwa mwaka 2012 bustani hii ya wanyama iliingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni mia saba kwenye uchumi wa Jiji la San Diego ambapo nusu ya gharama hizo ni kutokana na viingilio vya wageni wanaomiminika kila siku.



Mbali na mualiko wa tamasha la San Diego Zoo, Bw. Rovsek aliandaa hafla ya chakula cha mchana kwa heshima ya Mabalozi wa Hiari wa Tanzania, Botswana na Afrika ya Kusini iliyofanyika San Diego Yatch Club nje kidogo ya jiji hilo.
Juu na chini ni Consulate General wa Afrika Kusini Bw. Cyril Ndaba na Honorary Consul wa Tanzania Bw. Ahmed Issa wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye meza za Afrika Kusini, Kenya, Tanzania na Botswana.
Juu na chini ni Mwanamitindo maarufu wa California Leonard Simpson wa Fashion Forward akifurahia gauni lililobuniwa kwa hisia ya rangi za bendera (inspired by) ambalo lilinakshiwa kwa mkanda na pochi yenye rangi za bendera ya taifa. Nakshi hizo zimetengenezwa na Mtanzania aishiye Maryland Susan Malima wa Bioto Fashion.

Mindi Kasiga akiwa kwenye picha ya pamoja na familia ya Richard Rovsek kabla ya hafla hiyo kuisha
Picha ya pamoja (kutoka kushotoo - kulia) Diane Neima (Botswana) Ahmend Issa (Tanzania), H.E. Jean Kamau (Kenya), Nancy Assenga (Tanzania Investment Group of USA-TIGU), Mindi Kasiga (Ubalozi wa Tanzania DC), Cyril Ndaba (Ubalozi Mdogo Afrika Kusini mjini LA)




1 comment:

Anonymous said...

mindi naona unazidi kupendeza tuu-friend from MN