Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa picha ya X-Ray, ya mmoja kati ya majeruhi waliolazwa kwenye Hospitali ya Mount Meru, Joseph Anthony, mkazi wa Karoleni, baada ya kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotokea wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema eneo la Soweto jijini Arusha. Imeelezwa kuwa hadi jana Juni 17, 2013, wakati makamu alipowatembelea majeruhi hao watu watatu waliliripotiwa kufariki dunia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wa jijini Arusha waliokusanyika nje ya Hospitali ya Mount Meru jana, wakati Makamu alipokuwa na ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema jijini Arusha, ambapo jumla ya watu 70 walijeruhiwa na watatu walifariki dunia. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, aliyelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Selian, mkoani Arusha baada ya kudaiwa kushambuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika uchaguzi mdogo wa Udiwani wa Kata ya Makuyuni, Monduli. Awali Nasari alikaririwa akieleza kuwa anamaumivu ya mgongo baada ya kushambuliwa na vitu vigumu na vijana wa Kimasai. Kwa mujibu wa maelezo ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Paul Kweka, anayemtibu Mbunge huyo, alimueleza Makamu wa Rais kuwa mbunge huyo, baada ya kupimwa na kupigwa picha za X-Ray, ameonekana kuwa hana tatizo lolote la kiafya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Geofrey, kuhusu jinsi mtoto, Aboubakar Adam, mkazi wa Sakina jijini Arusha, aliyelazwa katika Hospitali ya ARumeru baada ya kujeruhiwa na bomu wakati akiwa miongoni mwa watu waliokuwa katika Uwanja wa Soweto kwenye Mkutano wa Chadema wiki iliyopita. Makamu wa Rais, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo, waliolazwa katika Hospitali za Arumeru, Selian na Mtakatifu Elizabeth, jana Juni 17, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali, Gabriel Kivuyo (52) aliyelazwa Hospitali ya Rufaa Selian, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali, mtoto aliyetambuliwa kwa jina moja la Fahad (7) aliyelazwa katika chumba cha watu mahututi Hospitali ya Rufaa Selian, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo A, Sarah John (45) aliyelazwa Hospitali ya Mtakatifu Elizabeth, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment