Monday, June 17, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AFUNGA TAMASHA LA ASILI LA WATU WA MANGAPWANI UNGUJA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja na msimamizi wa Kisima cha Chini kwa Chini, Abdulwakir Zahro, wakati alipofika kutembelea na kujionea Kisima hicho cha Chini kwa Chini, kilichopo Mangapwani, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja jana Juni 15, 2013. Kushoto ni Mlezi wa Tamasha la Asili la watu wa Mangapwani, Ali Hassan Mwinyi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mlezi wa Tamasha la asili la Watu wa Mangapwani, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Mwinyi Jamari Ramadhan Nasib, pamoja na baadhi ya viongozi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mangapwani jana Juni 15, 2013 kwa ajili ya kufunga rasmi Tamasha hilo lililoanza Juni 14.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia bidhaa zinazotengezwa na vikundi vya akina mama wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika Tamasha la Asili la Watu wa Mangapwani, alipofika kufunga rsmo tamasha hilo jana Juni 15, 2013, mjini Munguja.
  Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiingia shimoni wakati alipofika Mangapwani Kutembelea na kujionea Kisima cha Chini kwa Chini, kilichokuwa kikitumiwa na Wakoloni kupitishia Watumwa. Kisima hicho kilicho chini ya Ardhi huko ndani kuna Njia tatu, mbili zinatokezea Baharini na moja inatokezea katika moja ya Kijiji cha Mangapwani, ambayo hadi leo haijajulikana mwisho wa njia hiyo inapotokezea. 
 Katika Tamasha hilo kulikuwa na mashindano ya michezo mbalimbali ya asili, kama Bao la Kete, Kufua Nazi, na kama mchezo huu pichani vijana wakishindana kukwea Minazi, ambapo kwa upande wa michezo Tamasha hilo lilihitimishwa kwa mchezo wa fainali ya Soka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mlezi wa Tamasha la asili la Watu wa Mangapwani, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Mwinyi Jamari Ramadhan Nasib, pamoja na baadhi ya viongozi, kwa pamoja wakifurahia mchezo wa kukwea minazi wakati wa Tamasha hilo.
 Baadhi ya washiriki wa mchezo wa kufua Nazi, wakichuana kufua Nazi hizo ambapo kila mmoja alitengewa jumla ya Nazi 20, na mchezaji wa kwanza (kushoto) ndiye aliibuka mshindi kwa kuwaacha wenzake na Nazi nyingi zaidi wakiendelea kuchuana wawili.

  Wasanii wa Kikundi cha Sanaa na michezo ya asili cha Luperwa Zanzibar Group, chenye maskani yake Bububu, wakitoa burudani wakati wa hafla ya kufunga Tamasha hilo, lililofungwa na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana Juni 15, 2013 Mangapwani.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka shimoni kuangalia Kisima cha chini kwa chini kilichopo Mangapwani, ambacho kilikuwa kikitumiwa na Wakoloni kupitishia Watumwa. Kisima hicho kilicho chini ya Ardhi ndani kuna Njia tatu, mbili zinatokezea Baharini na moja inatokezea katika moja ya Kijiji cha Mangapwani, ambayo hadi leo haijajulikana mwisho wa njia hiyo inapotokezea.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunga mlango wa Kibanda cha Makuti kama ishala ya kufunga rasmi Tamasha hilo la Watu wa Mangapwani, jana Juni 15, 2013, lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Juni 14.  Picha na OMR

No comments: