Saturday, March 9, 2013

WAZIRI MKUU WA DENMARK AMALIZA ZIARA YAKE HAPA NCHINI

Waziri Mkuu wa Denmark, Mhe. Helle Thorning-Schmidt akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara alipotembelea Hospitalini hapo kujionea shughuli mbalimbali.


Mhe. Thorning-Schmidt akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Madaktari katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu alipotembelea Wadi ya Watoto hospitalini hapo. Mwingine katika picha ni Mhe. Mary Nagu (Mb.), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye amefuatana na Mhe. Helle katika ziara yake mkoani humo.

Mhe. Thorning-Schmidt akizungumza na mmoja wa kina mama waliolazwa hospitalini hapo kuhusu maendeleo ya afya ya mtoto wake.

Mhe. Thorning-Schmidt akiwa amembeba mtoto mmoja alipotemebelea Wadi ya Watoto katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu

Mhe. Thorning-Schmidt akisikiliza maelezo kuhusu Chuo cha Mafunzo ya Afya kilichopo katika Hospitali ya Wialaya ya Mbulu. Wengine katika picha ni Mhe. Waziri Nagu na Mhe. Eraston Mbwilo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Mhe. Thorning-Schmidt akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Afya kilichopo katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu.

Wanafunzi wa Chuo hicho wakimsikiliza Mhe. Thorning-Schmidt (hayupo pichani) alipozungumza nao.

Mhe. Thorning-Schmidt akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbulu.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbulu wakimsikiliza Mhe. Thorning-Schmidt alipozungumza nao

Mhe. Thorning-Schmidt akisalimiana na Dkt. Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mara baadaya kuwasili Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha.

Picha ya Pamoja kati ya Mhe. Thorning-Schmidt, Mhe. Waziri Nagu, Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na baadhi ya wajumbe aliofuatana nao katika ziara yake.

Mhe. Thorning-Schmidt akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha TCDC kilichopo Usa River mkoani Arusha. Kituo hicho kinafadhiliwa na Denmark na kilianzishwa miaka 40 iliyopita.

Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na Mhe. Waziri Nagu mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Arusha.

Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Magesa Mulongo mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani humo.

Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na viongozi mbalimbali waliofika kumsindikiza.

Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na Balozi wa Denmark hapa nchini Mhe. Johnny Flento mara baada ya kuhitimisha ziara yake.

Mhe. Thorning-Schmidt akielekea kupanda ndege tayari kwa kuondoka nchini.

No comments: