Saturday, March 9, 2013

MAMA SALMA KATIKA SHEREHE ZA SIKU YA WANAWAKE MKOANI MWANZA

IMG_4132.JPG
IMG_4139.JPG
IMG_4158.JPG
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa Jiji la Mwanza wakati wa kilele cha siku ya wanawake iliyofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana

IMG_4189.JPG
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaongoza wananchi wa Mwanza kuimba na kucheza wimbo wa 'wanawake na Maendeleo' kwenye uwanja wa Nyamagana jijini wakati wa sherehe za siku ya wanawake

IMG_4195.JPG 
IMG_4248.JPG
IMG_4288.JPG
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na baadhi ya wananchi wenye ulemavu wa ngozi waliohudhuria sherehe za siku ya wanawake zilizofanyika kwenye uwanja wa Nyamagan

IMG_4359.JPG
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya kabila la Wasukuma wakati alipotembelea katika kijiji cha Kisesa kilichoko wilayani Magu ambako nako kulifanyika sherehe ya siku ya wanawake kiwilaya

IMG_4378.JPG
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na akinamama wa wilaya ya Magu wakati wa sherehe za siku ya wanawake zilizofanyika kiwilaya katika kijiji cha Kisesa
 
IMG_4404.JPG
IMG_4415.JPGI
IMG_4513.JPG
IMG_4565.JPG
Mama Salma Kikwete akimsalimia mmoja ya wacheza ngoma huku mtu huyo akiwa amemshika nyoka aina ya chatu wakati wa sherehe za siku ya wanawake zilizofanyika huko Bujora-Kisesa wilayani Magu


IMG_4590.JPG
IMG_4593.JPG
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amekaakwenye kiti kinachokaliwa na machifu wa kabila la Wasukuma wakati wa sherehe za siku ya wanawake huko Kisesa wialyani Magu.


IMG_4598.JPG
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipewa zawadi mbalimbali za jadi za kichifu na wake wa Machifu wa Kisukuma wakati wa sherehe za siku ya wanawake zilizofanyika  huko Bujora -Kisesa katika wilaya ya Magu tarehe 8.3.2013. Baada ya kupewa zawadi hizo walimkalisha kwenye kigoda na kumpa jina la Kisukuma la 'Mbula'  likimaanisha mtu aletaye mvua kwani mara baada tu ya kuwasiri kijijini hapo mvua ilinyesha 

PICHA NA JOHN LUKUWI




No comments: