Mrisho Mpoto ni moja kati ya wasanii
wakubwa wa Muziki na Maigizo ya Jukwani hapa nchini. Michezo hii ya jukwaani ambayo
ni adimu na adhimu sana hapa nchini kutokana na umakini na utaalaam mkubwa unao
hitajika katika uandishi, uongozaji na hata uchezaji jukwaani.
Hapa nchini kuna wasanii wachache wenye
uwezo wa kutimiza hatua zote za maandalizi ya mchezo wa jukwaani. Tumekuwa
tukishuhudia wataalam walio pikwa kutoka
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo na wale wa Chuo kikuu cha Mlimani katika
Idara ya Sanaa na Maonesho na Chuo kikuu Huria wakishughulika sana na tasnia
hii.
Baada ya kuona Tasnia hii inasua sua, Bwana
Mrisho Mpoto aliamua kwa dhati kurudisha heshima ya michezo hiyo kwa kuishawishi
kampuni inayo jishughulisha na Maonesho ya Jukwaani ya nchini Kenya Kuuleta
mchezo ulio jipatia umaarufu mkubwa kwenye nchi mbali mbali ulimwenguni na hata
kupata heshima ya nyota tano nchini Uingereza ambapo Mrisho yeye mwenyewe
akiucheza mchezo huo kama mhusika mkuu.
Kutokana na kukubali kwa kampuni hiyo Bwana
Mrisho aliwashirikisha wadau wapenda maendeleo ya sanaa mchini, Clouds FM na
Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam ambao ndio walitoa mchango mkubwa
wa kufanikisha onesho hilo lifanyikie hapa nchini.
Mwishoni mwa wiki hii Onesho hilo
lilifanyika katika Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na kuhudhuriwa
na watazamaji wengi wanao elewa umuhimu wa michezo ya jukwaani.
Watazamaji walisifia Umahiri ulio oneshwa
na Mrisho Mpoto na waigizaji wengine ambapo waliwafanya watazamaji kutabasamu
kwa furaha kubwa kila wakati wa mchezo huo.
Baadhi ya washabiki walisema kuwa,
wameshangazwa sana kwa kuona kuwa wasanii wa filamu hapa nchini hawajajitokeza kabisa
kuja kushuhudia uzuri wa sanaa za jukwaani, kwani kwa kufanya hivyo wangeweza
kujifunza uigizaji wa kweli, na unao hitaji umakini na taalam wa kutosha tofauti
na michezo ya filamu inayo ibuka sasa kila kukicha. Wametoa wito kwa watanzania
na wasanii wote nchini kuwa na tabia ya kushiriki katika maonesho mbali mbali
hapa nchini yenye sura ya kuelimisha kwakupitia utamaduni wetu.
Nae mmoja wa wasanii kutoka Kenya ambae
hakupenda jina lake litaje alisema kuwa, wamependezwa na kufurahishwa sana na
jitihada za msanii Mrisho Mpoto anazo zionesha pindi anapo kuwa mazoezini na
kisha jukwaani, na ametoa wito kwa wasanii mbali mbali Tanzania kufuata nyao za
Msanii huyu katika harakati zake za kuurejesha heshima ya Michezo ya jukwaani
kwani ndio inae weza kuhudhuriwa na wanafamilia tofauti na sanaa zingine ambazo
ni maarufu kwa sasa.
Akitoa shukrani zake baada ya onesho Bw,
Mpoto alimshukuru sana Mkurugenzi wa Clouds Media Bw Ruge Mutahaba kwa kukubali
kuisaidia tasnia ya Michezo ya kuigiza ya Jukwaani. Ili kurudisha heshma ya
michezo hiyo hapa nchini, pia Bw Mpoto aliushukuru Uongozi wa Makumbusho na
Nyumba ya Utamaduni kwa kukubali kutoa mchango wake mkubwa katika kufanikisha
onesho hilo na kuonesha moyo wa kuendelea kusaidia wasanii hapa nchini katika
kuinua na kuendeleza Utamaduni wa Mtanzania.
Mchezo wa Wanawake wa Heri wa Winsa uliotokana na kitabu
kitabu kilicho andikwa na Shakespeare takribani miaka 1600 iliyo pita, na
kutafasiriwa na Bw Ogutu Mulaya wa nchini Kenya, ulishirikisha waigizaji nane
ambapo kila mwigizaji alivaa husika zaidi ya tatu, na wote walizimudu vyema
husika hizo.
Habari na SIXMUD J. BEGASHE wa Makumbusho ya Taifa.
No comments:
Post a Comment