Monday, February 18, 2013

Vodacom,HPSS zazindua mfumo mpya wa menejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF Iliyoboreshwa) kwa Mkoa wa Dodoma


  Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Vodacom Joseline Kamuhanda akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa menejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF Iliyoboreshwa) iliyofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kupitia mfumo huo mpya Vodacom inawezesha huduma za Intaneti na SMS bure kwa wadau wa CHFkuwezesha shughuli za mfuko huo kielektroniki
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri akihutubia hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa menejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF Iliyoboreshwa) mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Mradi wa HSPP Madfred Stroemer watekelezaji wa mfumo huo mpya kwa ufadhili mkuu wa Serikali ya Uswisi na Vodacom(katika mawasiliano).
  Naibu Waziri Mwanri akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi kadi ya uanachama wa mfuko wa Afya ya Jamii Ulioboreshwa - CHF muda mfupi baada ya kuzindua mfumo mpya wa nmenejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya mfuko huo utakaowezesha uandikishaji, ukusanyaji  na uwasilihaji madai ya malipo kwa wato huduma na ufuatiliaji wa taarifa za wanachama kwa njia rahisi ya kielekrtoniki kutumia mtandao wa Vodacom mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
  Naibu Waziri Mwanri akijiandikisha uanachama wa CHF Iliyoboreshwa muda mfupi baada ya kuzindua mfumo mpya wa nmenejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya mfuko huo utakaowezesha uandikishaji, ukusanyaji  na uwasilihaji madai ya malipo kwa wato huduma na ufuatiliaji wa taarifa za wanachama kwa njia rahisi ya kielekrtoniki kutumia mtandao wa Vodacom.
  Meza Kuu ikiwafuatilia ikifuatilia matukio yanayovyoendelea wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa menejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF Iliyoboreshwa). Kutoka kulia ni Naibu Waziri TAMISEMI Aggrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Fidelis Mwedipandu na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Vodacom Joseline Kamuhanda.
Wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa menejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF Iliyoboreshwa) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri(hayupo pichani)katika ukumbi wa mikutano wa Dodoma Hotel mwishoni mwa wiki.Mfumo huo unatekelezwa kupitia mradi wa HSPP kwa ufadhili mkuu wa Serikali ya Uswisi.
 Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwassa,  Mkuu Wilaya ya Chamwino Fatma Salum Ally, Meneje Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Francis Isaac na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Vodacom Joseline Kamuhanda muda mfuoi baada ya kuzinduliwa kwa mfumo mpya wa menejementi ya taarifa za mfuko wa Afya ya Jamii Ulioboreshwa - CHF iliyoboreshwa mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

No comments: