Matamshi yaliyofanywa na Don
Smith, Mkurugenzi wa Fly540 Kenya, kuashiria kuwa anayo haki ya kuondoa nembo
na pia leseni ya uendeshaji hayafai na hayana msingi. Bodi ya wakurugenzi ya
Fly 540 Kenya haijawahi kukutana kwa ajili hata ya kufikiria suala hili na hii
imethibitishwa na wakurugenzi wengine. Imetambulika kwa mapana na umma wa
Tanzania kuwa suala hili si kitu kingine bali jaribio la kuhujumu sifa na
uaminikaji katika kibiashara.
Fastjet ingetaka kuvishauri
vyombo vya habari na abiria ambao husafiri nasi katika Afrika nzima katika
ndege za fastjet, ndege za Fly540 au ndege za Fly540 Afrika, kuwa, tunatazamia kupanua shirika
letu lenye gharama za chini ili liwepo katika bara zima la Afrika.
Hadi sasa, tunakaribia idadi ya
maombi ya kusafiria ya abiria 100,000, ambapo 30% wamelipia shilingi za
kitanzania 32,000 tu kwa ajili ya tiketi zao. Vile vile, tunafanya kazi kwa
kuzingatia muda na hatujakuwa na safari zilizofutwa au zilizobadilishwa huku
ndege zetu nyingi zikiwasili ziendako kabla ya muda uliopangwa.
================================
Akitoa kauli kuhusu
takwimu za fastjet, Mkurugenzi Mkuu Ed Winter alisema:
“Haya ni matokeo mazuri kwa mwezi wa pili tu
wa utendaji kazi hasa ukizingatia kuwa kipindi hiki kilikuwa ni kile
kinachofuata baada tu ya krisimasi ambapo kazi hupungua, kipindi ambacho, kama
kilivyotarajiwa, kiliendelea hadi mwezi huu, kabla ya biashara kurudia hali
yake ya kawaida.”
“Uzingatiaji wa muda katika mwezi huu ulikuwa
mzuri sana ukiwa katika kiwango cha 99.7% huku kukiwa hakuna safari
zilizofutwa. Masuala ya ubebaji na uombaji wa nafasi za kusafiri wa kabla kwa
mwezi Februari umezidi matarajio. Baada ya kujenga imani kuwa tunaweza kutegemewa
kwa ujumla wake katika safari za ndani ya Tanzania, hivi karibuni tutalitazama
suala la kufanya safari za kimataifa
kama zile za Johannesburg na Entebbe”
______________________________________________________________________________
Kazi zote Zingatio 1
Mwezi Januari
2013 Januari 2012 Badiliko
AbiriaZingatio 2 84,645 51,676 63.8%
Masuala ya ubebaji zingatio 3 63.1% Haihusiki Haihusiki
Miezi 12 iliyokwisha Januari 2013
Januari 2012
Badiliko
Abiria Zingatio 2 734,373 478,110 53.6%
_______________________________________________________________________________
Kazi za fastjet Zingatio 4
Mwezi Januari
2013 Januari 2012 Badiliko
Abiria Zingatio 2 26,414 0 Haihusiki
Masuala ya ubebajiZingatio 3 66.0 % 0 Haihusiki
Miezi 12 iliyokwisha Januari 2013 Januari 2012 Badiliko
Abiria Zigatio 2 58,329 0 Haihusiki
_______________________________________________________________________________
Mazingatio:
1.
“Kazi zote” ni pamoja na takwimu za
fastjet Tanzania, Fly 540 Kenya, Fly 540 Ghana na Fly540 Angola.
2.
“Abiria” kwa ajili ya utendaji wa 540
ni wale wanaosafirishwa, na kwa fastjet, ni viti vilivyouzwa kwa ajili ya
safari na inajumuisha pia watoto kwa fly 540 na fastjet.
3.
“Masuala ya ubebaji” ni idadi ya abiria
ikiwa kama asilimia ya idadi ya viti vya
kusafiria vilivyopo.
4.
”Kazi za fastjet” inajumuisha takwimu za
fastjet Tanzania tu kuanzia tarehe 29 Novemba 2012.
No comments:
Post a Comment