Na
Mwandishi Maalum
Nchi 188 kati ya 193 ambazo ni wanachama wa
Umoja wa Mataifa, zimepiga kura ya ndiyo
kuunga mkono Azimio linaloitaka Marekani
kuiondelea Cuba vikwazo vya
kiuchumi, kibiashara na kifedha.
Upigaji kura huo ,ulifanyika siku ya Jumanne hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni
mwaka wa 21 ambapo nchi wanachama zimekuwa zikilipigia kura azimio hilo
bila ya kuchoka.
Wakati nchi 188 zilipiga kura ya ndiyo , nchi tatu ikiwamo Marekani ilipiga
kura ya hapana. Nchi nyingine zilizopiga kura ya hapana ni Israel na Palau,
huku Marshall Islands na Micronesia zikipiga kura ya kutofungamana na upande
wowote. Baada ya Rais wa Baraza Kuu la
67 kutangaza matokeo hayo, wajumbe walishangilia kwa nguvu.
Kabla ya
kulipigia kura Azimio hilo ambalo liliwasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bw Bruno
Rodriquez Parrila. Wawakilishi wa nchi mbalimbali walizungumza
kuonyesha mshikamano wao na Cuba
kwa kusisitiza pamoja na mambo mengine kwamba sasa imetosha Marekani
ifikie mahali na kukubali ukweli halisi
wa mambo na kuondoka vikwazo hivyo
ambavyo vimedumu kwa miaka 50
tangu kuasisiwa kwake mwaka 1962.
Aidha, wasemaji kadhaa wameeleza kwamba vikwavyo hivyo
na ambavyo vimepitwa na wakati vinakwamisha
juhudi za Cuba kujiletea maendeleo , kuupiga vita umaskini na vinaifanya Cuba ishindwe kutekeleza Malengo
ya Maendeleo ya Millenia.
Vilevile
wawakilishi hao wakaeleza bayana kwamba kuendelea kwa vikwazo hivyo siyo
tu ukiukwaji wa sherika za kimataifa,
lakini pia ni kubinya uhuru wananchiwa
Cuba kujimulia mambo yao.
Baadhi
ya wasemaji kama vile mwakilishi wa Urusi yeye alikwenda mbali zaidi kwa
kusema, msimamo wa nchi yake dhidi ya vikwazo hivyo unajulikana wazi na
haujawahi kubadilika.
Akasema
nchi yake inapinga vikwazo vya Marekani
kwa Cuba na kusisitiza kwamba vikwazo hivyo ni masalia ya vita baridi ambayo
yamepitwa na wakati.
Akiwasilisha
Azimio hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Bruno Parrila, pamoja na kuainisha
madhara na hasara zinazotokana na vikwazo hivyo ambapo alisema madhara ya
kiuchumi katika miaka hiyo 50 yanakadiriwa kufikia trillion moja na dola
bilioni sita hadi mwishoni kwa mwaka
jana.
Ameitaka serikali ya Obama na hasa baada ya kurejea tena madarkani,kuonyesha
utashi wa kisiasa kwa kutekeleza kwa ukamilifu uondoaji wa vikwazo hiyo badala
ya kufungua milango nusu nusu.
Kwa Upande wake, msemaji wa Marekani,
akizungumza kwa nini nchi yake imepiga kura ya kupinga azimio hilo, alisema
kwamba si kweli kwamba nchi yake imekuwa
ndiyo chanzo cha wananchi wa Cuba
kuendelea kuteseka bali wa kulaumiwa ni Serikali yenyewe ya Cuba.
Akasema
inachofanya serikali yake ni kuwawezesha wananchi wa Cuba kujiamulia mambo yao
wenyewe na kuitaka serikali ya Cuba kuondoa sheria kandamizi zinazowabana wananchi wake hoja ambayo
ilipingwa vikali na msemaji wa Cuba.
No comments:
Post a Comment