Thursday, August 16, 2012

TAARIFA YA TUKIO LA MAUAJI YA MTU ANAYESADIKIWA KUWA NI JAMBAZI NA UKAMATAJI WA BUNDUKI MBILI

Kamanda wa Polisi mkoa wa (ACP) Liberatus sabas akiwaonyesha waaandishi wa habari silaha aina ya Rifle 458 iliyokuwa inatumiwa na jambazi ambaye alifariki dunia baada ya kupigwa risasi na askari wa Polisi walipokuwa wanarushiana risasi katika eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru tarehe 13/08/2012 (Picha na Rashid nchimbi wa Polisi Arusha)

MNAMO TAREHE 13/08/2012 MUDA WA SAA 8:30 USIKU KATIKA KIJIJI CHA LEVOROSI KATA YA KIMNYAKI WILAYANI ARUMERU, MTU ASIYEFAHAMIKA JINA, MWANAUME ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA 28 NA 30 AMBAYE ANADHANIWA KUWA NI JAMBAZI ALIFARIKI DUNIA AKIWA NJIANI ANAPELEKWA HOSPITALI KWA AJILI YA MATIBABU BAADA YA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI MARA BAADA YA KUKAHIDI AMRI HALALI YA KUJISALIMISHA.

TUKIO HILO LILITOKEA WAKATI ASKARI WA JESHI LA POLISI NA JAMBAZI HUYO AMBAYE KWA SASA NI MAREHEMU WAKIJIBIZANA KWA KURUSHIANA RISASI NA HIVYO ASKARI KUFANIKIWA KUMPIGA RISASI TUMBONI NA MARA BAADA YA UPEKUZI WALIFANIKIWA KUMKUTA AKIWA NA BUNDUKI AINA YA RIFLE 458 YENYE NAMBA 7052602464 MODEL ZKK-620 AMBAYE ILIKUWA IMEKATWA MTUTU PAMOJA NA KITAKO IKIWA NA RISASI MBILI.

AWALI ASKARI HAO WALIKWENDA KATIKA NYUMBA YA MAREHEMU NA KUIZINGIRA NA MAREHEMU ALISHTUKA BAADA YA KUSIKIA MILIO YA MBWA NA AKAFUNGUA MLANGO NA MARA ALIPOGUNDUA KUNA ASKARI ALIANZA KUWARUSHIA RISASI MBILI ILI APATE NJIA YA KUTOROKA JAPOKUWA ALIPEWA AMRI HALALI YA KUJISALIMISHA LAKINI ALIKAIDI.

UCHUNGUZI WA JESHI LA POLISI ULIBAINI KWAMBA MAREHEMU ALIKUWA ANASHIRIKIANA NA WENZAKE KATIKA MATUKIO MBALIMBALI YA UHALIFU NA JITIHADA ZA JESHI LA POLISI ZILIFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WATATU AMBAO WALIKUWA WANASHIRIKIANA NA MAREHEMU KATIKA MATUKIO YA UHALIFU YALIYOFANYIKA KATIKA MAENEO TOFAUTI YA NCHI.

WATUHUMIWA HAO WALIKIRI KUSHIRIKIANA NA MAREHEMU KATIKA MATUKIO MBALIMBALI NA KUELEZA ANAPOISHI, NDIPO ASKARI WALIPOENDELEA NA UPELELEZI NA SIKU HIYO YA TAREHE 13/08/2012 WALIFANIKIWA KUIZINGIRA NYUMBA HIYO AMBAPO KULITOKEA MAJIBIZANO YA RISASI NA HATIMAYE MTUHUMIWA KUPIGWA RISASI YA TUMBO NA KUFARIKI DUNIA AKIWA ANAPELEKWA HOSPITALI KWA AJILI YA MATIBABU.

MARA BAADA YA KUIPATA BUNDUKI HIYO KUTOKA KWA MAREHEMU KATIKA UCHUNGUZI WETU TULIGUNDUA KWAMBA, BUNDUKI ILIYOKUWA INATUMIWA NA MAREHEMU PAMOJA NA WENZAKE ILIPORWA TOKA KWA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GABRIEL S/O WILLIAM MKAZI WA SEKEI SIKU YA TAREHE 01/04/2012 MUDA WA SAA 4:00 USIKU AMBAPO MMILIKI HUYO ALIVAMIWA NA MAJAMBAZI HAO AKIWA ANAINGIA KATIKA GETI LA NYUMBA YAKE HUKU AKIWA NA GARI YAKE AINA YA SUZUKI ESCUDO YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 887 APC.

KATIKA TUKIO JINGINE LILITOKEA HUKO ILBORU TAREHE 02/08/2012 USIKU ASKARI WA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA WAKIWA DORIA WALIFANIKIWA KUKAMATA BUNDUKI MOJA AINA YA SHORT GUN-GREENERS GP GUN IKIWA IMEFUTWA NAMBA BAADA YA WATU WANAOAMINIKA KUWA NI MAJAMBAZI KUITELEKEZA BAADA YA KUGUNDUA KUWA WANAFUATILIWA NA ASKARI.

TUKIO HILO LILITOKEA BAADA YA ASKARI HAO KULITILIA SHAKA KUNDI LA WATU HAO NA MARA BAADA YA KUNDI HILO KUGUNDUA KWAMBA NI ASKARI POLISI WALIANZA KUKIMBIA NA MMOJA WAO KUTUPA CHINI MFUKO MWEUSI NA MARA BAADA YA ASKARI KUUPEKUWA WALIONA BEGI DOGO AMBAPO NDANI YAKE WALIIKUTA BUNDUKI HIYO AMBAYO ILIKUWA IMEKATWA MTUTU NA KITAKO IKIWA NA RISASI 12.

MPAKA HIVI SASA WATUHUMIWA HAO BADO HAWAJAPATIKANA NA JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA JUHUDI ZA KUWATAFUTA. MAFANIKIO HAYO YAMETOKANA NA MSAKO ENDELEVU ULIOANZA TOKA TAREHE 08/06/ MWAKA HUU KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MKOA HUU. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,

KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,

(ACP) LIBERATUS SABAS

TAREHE 14/08/2012.

No comments: