Mgunga Discussion with Zodi ,the costume designer on her designs
Eva (Antigone) in rehearsal
The Production Directors
Mgunga Presenting Parapanda actors to the swedish counterpart actors
The Production Directors Mgunga mwa Mnyenyelwa of Parapanda Theatre and Ronny Hallgren
The Gothernburg City Theatre building |
Wasanii 7 na Mwongozaji mmoja wa kundi la sanaa za maonyesho la Parapanda wako nchini Sweden kwa ziara ya maonyesho ya Utambaji wa mashairi na uandaaji wa tamthiliya ya ANTIGONE. Tamthiliya hii imeandikwa miaka 42 kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Mwandishi wake ni Yule msanii mwandishi nguli wa kigiriki wa tamthiliya za jukwaani aliyejulikana kwa jina la Sophocles.
Tamthiliya hii imetafsiriwa katika lugha zote kuu za dunia kasoro Kiswahili na kwa mara ya kwanza itachezwa kwa Kiswahili na Kiswidi.
Maandalizi na maonyesho ya tanthiliya hii yanafanywa na taasisi mbili za sanaa za maonyesho: Parapanda Theatre Lab Trust na Gothernburg City Theatre ya Swideni .kuanzia tarehe 2/8/2011 mpaka 14/12/2011. Maandalizi na maonyesho yanafanyika Swideni na Tanzania.
Majina ya wasanii na Waongozaji
| Wasanii wa Parapanda | Wasanii wa Gothernburg Theatre |
| Jane Mwatonoka | Nina Zanjani |
| Frank Samatwa | Johan Karlberg |
| Daud Joseph | Fredrik Evers |
| Shabo Makota | Anna Bjelkerud |
| Amani Lukuli | |
| Habiba Nguogani | |
| Eva Nyambe | |
| | |
Waongozaji
Kuhusu Mahusiano
Wakati wa mradi huu vikundi na taasisi za sanaa za maonyesho kutoka nchi za mashariki mwa Afrika ziliweka urafiki na wasanii wa vikundi na taasisi za Uswidi. Katika Mahusiano hayo vikundi vilitembeleana,vikafanya warsha na kushiriki katika matamasha ya Uswidi na Tanzania.
Parapanda & Gothernburg City Theatre.
Chimbuko la mahusiano ya taasisi hizi mbili ni Tamasha la Sanaa la EATI lilifanyika Mombasa Kenya. Mkurugenzi wa GCT mr Ronnie Heglen alifika kutoka Swideni na kushuhudia onyesho la “Kalunde” ambalo lilikuwa ni mchanganyiko wa utambaji wa hadithi, muziki na ushairi. Uongozi wa kutoka Jumba la sanaa la Gothernburg ulikaa kikao na uongozi wa Parapanda chini ya bwana Mgunga Mwa Mnyenyelwa kuhusu nia ya kuanzisha ushirikiano wa kisanii.
Ushirikiano huu uliwasilishwa rasmi katika vikao vya PACSEA na EATI na kukubaliwa.
Hatua ya awali katika ushirikiano huo ika ni kuwa na warsha ya kutambuana na kubadilishana mawazo . Warsha hii ilifanyika mwaka 2005 katika ofisi za Parapanda. Wasanii sita kutoka GCT walikutana na wasanii nane wa Parapanda kwa muda wa wiki moja. Ni katika warsha hii ambapo wasanii wa Parapanda walionyesha hazina waliyonayo katika sanaa.Warsha kama hiyo ikafanyika mwaka 2008 nchini Uswidi. Halikadhalika huko wasanii wa Parapanda walijifunza mbinu na aina ya sanaa inayofanywa na GCT.
Wasanii wa Parapanda walishiriki katika matamasha ya Utambaji hadithi na ushairi nchini Swideni mara mbili; 2005 na 2007.Baada ya kufahamiana vizur,i Uamuzi wa kuandaa onyesho la pamoja ulifanyika. Mapendekezo yalitolewa na GCT kwamba tamthiliya ya Antigone ndiyo ingefaa kuandaliwa. Sababu kubwa ilikuwa; ni tamthiliya kongwe inayoheshimika duniani na pili ni tamthiliya inayoeleza masuala kadhaa ambayo yanaakisi maisha ya leo ya sehemu nyingi duniani ikiwemo Tanzania. Suala kubwa ni Harakati za Mwanamke kupambana na mifumo gandamizi, wajibu wa raia, migogoro ya kitabaka na kiutamadini na nafasi ya vijana katika jamii inajitokeza.
Uamuzi wa kuandaa tamthiliya hii ulikubaliwa na Parapanda na kuanza kuandaa ratiba ya utekelezaji . Kwa mujibu wa mradi huu, wasanii saba wa Parapanda na wanne wa GCT watachukua husika. Kutakuwa na waongozaji wawili, Mgunga Mwa Mnyenyelwa (Parapanda) na Ronnie Hegllen (GCT). Onyesho litatumia sehemu kubwa ya mbinu za uwasiishaji za Parapanda husussani katika muziki,ngoma na ushairi.
Ratiba ya maandalizi na maonyesho
Tarehe | Tanzania |
Juni 31 | Kuondoka kwenda Swideni kuandaa onyesho |
Agosti 28 | Kurudi Tanzania na kuendelea na maandalizi |
Sept 21 | Ufunguzi wa onyesho Tanzania |
Sept 22- 25 | Maonyesho Tanzania. Waterfront, Kituo cha Utamaduni cha Urusi – 22/9 wazi, 23/9 wanafunzi - tamasha la sanaa Bagamoyo: 25/9 |
Sept 29 | Kwenda Swideni |
Oktoba 8 | Kufungua maonyesho Swideni |
Desemba 14 | Kumaliza maonyesho Swideni |
Desemba 16 | Wasanii kurudi nyumbani. |
Jumla ya maonyesho swideni 28
Wakati wa ziara hiyo Parapanda mealikwa kufanya maonyesho ya muziki na utambaji wa mashairi na ngoma katika tamasha la Utamaduni la watu wa Gothernburg wiki ijayo tarehe 19/8/2011 usiku katika uwanja maarufu wa maonyesho ya nje wa Gothernburg City . Makundi mbalimbali zaidi ya ishiriki kutoka ndani na nje ya Swideni yantarajiwa kushiriki. Wasanii wa Parapanda wapo katika mazoezi makali ya kushiriki tamasha hilo sambamba na maandalizi ya tamthliya ya Antigoni
Mwongozaji &Mkuu wa msafara.
No comments:
Post a Comment