Thursday, August 11, 2011

uzinduzi wa Vodacom house miss tanzania 2011



Pichani ni Washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 wapatao 30 wakiwa katika pozi.
Ofisa Mkuu wa Masoko na mahusiano wa kampuni ya Vodacom,Mwamvita Makamba akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Vodacom House Miss Tanzania 2011 usiku huu,kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency inayoratibu shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundega pamoja  Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza wakishuhudia tukio hilo.
Vigele gele na shwangwe zilizuka mara baada ya uzinduzi wa nyumba hiyo ambayo watakuwa wakikaa Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 na kufanya shughuli mbalimbali ndani ya jumba hilo ambalo limesheheni kila kitu.
Mandhari ya jengo hilo la Vodacom  house Miss Tanzania likionekana kwa nje.
Ofisa Mkuu wa Masoko na mahusiano wa kampuni ya Vodacom,Mwamvita Makamba akizungumza jambo usiku huu na washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kabla ya uzinduzi wa nyumba ya V house.
 Mkurugenzi Lino International Agency ambao ndio waratibu wa Miss Tanzania ,Hashim Lundega akiwashukuru wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi huku akiwa amezungukwa na washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2011.
 Mdau Angela Msangi kutoka TBC akiripoti usiku huu wakati wa uzinduzi wa nyumba ya Vodacom house Miss Tanzania 2011 usiku huu.
Ofisa Mkuu wa Masoko na mahusiano wa kampuni ya Vodacom,Mwamvita Makamba akiwaelekeza baadhi washiriki wa Miss Tanzania namna ya kufungua kinywaji aina ya Shampeni,kabla ya shamra shamra za uzinduzi wa nyumba ya washiriki hao kuzinduliwa rasmi usiku huu.
 Ankal Lundenge naye akipiga cheeerzzz na Walimbwende.
 Washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2011 wakicheeersss kwa pamoja.
 Ofisa Mkuu wa Masoko na mahusiano wa kampuni ya Vodacom,Mwamvita Makamba akicheeerss na Walimbwende wa Vodacom Miss Tanzania 2011 usiku huu.
 Washiriki wakiwa wamejiachia kwa namna yao usiku huu huku wakibadilishana mawazo hapa na pale.
 Pichani kati ni Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akiwa na baadhi ya wageni waalikwa usiku huu wakati wa uzinduzi wa Vodacom House 2011.
 Wageni waalikwa wakijadiliana jambo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa wamekula pozi kwa picha huku wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea usiku huu. Picha zote na Michuzi Jr.

Vodacom Miss Tanzania 2011, Top Model Mwajabu Juma akipozi mbele ya wenzake kwa ajili ya picha mara baada ya kutwa kuwa ndiye mshindi wa taji hilo na mrembo wa kwanza kuingia katika Nusu Fainali za Vodacom Miss Tanzania mwaka huu. Shindano hilo lilifanyika juzi usiku na matokeo kutangazwa jana mbele ya waandishi wa habari
Vodacom Miss Tanzania 2011, Top Model Mwajabu Juma (katikati) akipongezwa na washiriki wenzake wa Miss Tanzania baada ya kutajwa kuwa ndiye mshindi wa taji hilo na mrembo wa kwanza kuingia katika Nusu Fainali za Vodacom Miss Tanzania mwaka huu. Shindano hilo lilifanyika juzi usiku na matokeo kutangazwa jana mbele ya waandishi wa habari.
Warembo walioingia tano bora ya shindano la Vodacom Miss Tanzania Top Model, Kutoka kushoto ni Jeniffer Kakolaki, Alexia William, Zerulia Manonko, Cynthia Kimath na Mwajabu Juma wakiwa katika picha ya pamoja.



No comments: