Monday, March 14, 2011

TAMIM AWADH AMTIA ADABU ASHARFF SELEMANI

Mgeni rasmi akitambulishwa na muandaaji
Bw. Kimbau akiwa na Rashid Matumla

Majigambo ya muda mrefu baina ya mabondia wawili wenye uzito Mzito Tamim Awadh na Asharaf Suleiman yalimalizika wikiendi hii katika ukumbi wa DDC Mliman City jijini Dar es Salaam.

Mpambano huo ulianza majira ya saa 4 usiku ulianza kwa kasi kwa kila bondia kumsoma mwenzake katika raundi ya kwanza tu Asharaf alimtwisha konde mpinzani wake Tamim na kumuangusha chini .

Katika raundi ya pili Tamim tena alilamba sakafu kwa mara ya pili baada ya kuona hivyo mashabiki waliokua wamejaa katika ukumbi huo walianza kushangilia na Asharaf aliendelea kummwagia dozi mpinzani wake kwa ngumi nzito ambazo zilikuwa zikimwingia vilivyo hadi kumchana puani .

katika raundi ya tano Tamim alionyesha ishara ya kuchinja akiwa na maana ya kuwa ndivyo alivyoingia kwa nguvu katika round hiyo na kuanza kumiminia makonde Asharaf ambapo katika round hiyo alionyesha kuishiwa pumzi na kukubali kupigwa ngumi iliyomsababishia na yeye aanguke chini

katika raundi ya sita Tamim ambaye ni bingwa wa mkamnda wa Afrika Mashariki alimtwanga konde la usoni Suleiman na kumfanya kuanguka tena hivyo ngoma ikawa sawa kila mmoja kuanguka mara mbili,

Katika raundi ya Saba Asharaf alizidiwa kabisa kwa kukubali kupigwa makonde mfulululizo yaliyomfanya kuomba asiendelee tena hivyo Tamim alishinda kwa Technical KO.
Mashabiki wa Tamim
Tamim (shoto) na Ashraf wakipambana
Refa wa kimataifa Bw. Kavishe akimhesabia Tamim
aliyenoa stepu na kupigwa upper cut
Tamim akivuta pumzi raundi ya nne
Mpambano ukiendelea
Tamim akishukuru kwa ushindi
Mshabiki akimshangilia Tamim
Ngoma nzito...
Tamim akigalagala kwa furaha
Tamim akishuka jukwaani baada ya kumwaga dozi

No comments: