Monday, March 14, 2011

Washindi wa bahatika na Tigo wakabidhiwa ndinga zao

Mshindi wa gari aina ya Nissan Hard Body ya promosheni ya Bahatika na Tigo, yenye thamani ya shs milioni 56 Jackline Mambo mkazi wa Kilimanjaro akifurahi mara baada ya kukabidhiwa gari lake katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Coco Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Uhusiano wa Tigo Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya gari ya promosheni ya Bahatika na Tigo ambako washindi wawili walikabidhiwa magari yao aina ya Nissan Hard body yenye thamani ya shs milioni 56 kila moja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Viwango wa Tigo, David Zakaria akikabidhi funguo ya gari aina ya Nissan Hard Body yenye thamani ya shs milioni 56 kwa mshindi wa promosheni ya Bahatika na Tigo, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Coco Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwanamuziki wa kizazi kipya wan kundi la Wanaume Halisi, Juma Kassim Nature, akitoa burudani katika tamasha la Bahatika na Tigo ambalo washindi wawili wa gari walikabidhiwa magari yao aina ya Nissan Hard Body kweny ufukwe wa Coco Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Chidi Benz akifanza vitu vyake katika
onyesho hilo.
Mwasiti Alimasi (shoto) akiimba moja ya nyimbo zake pamoja na baadhi ya washirika wake katika onyesho hilo katika viwanja vya Coco Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Mwamba wa Kaskazini Joe Makini akiwachengua umati wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam katika onyesho la Bahatika na Tigo katika viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam.



Roma Mkatoliki naye alikuwepo katika
kuhakikisha onyesho hilo linakuwa la kukata na shoka.

Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofurika katika viwanja vya Coco Beach, Dar es Salaam kushuhudia onyesho la Bahatika na Tigo ambalo washindi wawili walikabidhiwa magari yao aina ya Nissan Hard Body.

No comments: