Tuesday, January 11, 2011

TAARIFA YA MATATIZO YANAYOWAKABILI WAFANYAKAZI WANATAALUMA WA CHUO KIKUU CHA DODOMA

Utangulizi

Tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2007 kumekuwa na maendeleo makubwa ya miundo mbinu mbalimbali hasa majengo na barabara. Chuo kimepanuka kwa kiwango cha kuridhisha na hii ni hatua ya kupongezwa na mpenda maendeleo yeyote.

Sanjari na ujenzi wa miundo mbinu kutokana na kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi watumishi wa fani mbalimbali wamekuwa wakiajiriwa tangu kuanzishwa kwa chuo. Katiba ya Chuo (University Charter) imeweka wafanyakazi katika makundi makuu mawili. Moja ni kundi lenye wafanyakazi wanataaluma ambao pamoja na mambo mengine kazi yao kubwa ni ufundishaji, utafiti na ushauri; na pili ni kundi la wafanyakazi wa upande wa utawala. Hata hivyo chuo kinakua kwa haraka sana na hivyo kuhitaji idadi ya wafanyakazi iendanayo na kasi ya ukuaji wa chuo.

Matatizo ya Wafanyakazi Wanataaluma UDOM

Pamoja na jitihada nzuri ya kuajiri wafanyakazi ili kukidhi mahitaji ya chuo, kumekuwapo matatizo mbalimbali yanayowakabili wafanyakazi katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Matatizo makubwa yanaegemea katika swala la malipo ya stahili mbalimbali pamoja na mishahara kama inavyoelekezwa katika nyaraka mbalimbali za serikali. Mkutano wa 4 wa UDOMASA umeainisha matatizo hayo ni kama yafuatavyo: BOFYA HAPA

No comments: