Wednesday, May 30, 2018

RC Wangabo kutumia nguvu ya dola kukomesha Kipindupindu

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema atalazimika kuwatumia polisi kusimamia zoezi la usafi na ujenzi wa vyoo salama katika Kijiji cha Namasinzi, kata ya Kapenta, bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga baada ya wananchi hao kushindwa kujenga vyoo hivyo mbali na elimu ya umuhimu wa vyoo waliyopewa kwa muda mrefu.

Amesema kuwa ikifikia hatua hiyo Kijiji hicho kitafungiwa na hakuna atakayetoka wala kuingia na hatimae kusitisha shughuli za kiuchumi za Kijiji hicho ambacho ni maarufu kwa kilimo cha mpunga hali itakayopelekea maisha magumu kwa wananchi hao jambo ambalo asingependa litokee.

Katika kuhakikisha hali hiyo haitokei Mh. Wangabo alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule na timu yake ya usafi ya halmashauri kuhakikisha wanapita kaya kwa kaya ili kuzibaini kaya zisizopenda usafi na zisizokuwa na vyoo na kuzichukulia hatua za kisheria kwani kwa kushindwa kufanya hivyo kipindupindu hakitamalizika katika bonde hilo.

“Sasa tutatumia nguvu ya dola, ili kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi katika maisha ya usafi wala sio uchafu, na kila mtu ahakikishe kwamba anakuwa na kiboko Fulani ambacho ni kigumu amuone mtu anachemsha maji, anayaweka maji yake yanapoa akienda shambani anakwenda na maji mbayo yamekwisha poa, lakini mkilea lea hivi, waswahili wanasema ukicheka na nyani unavuna mabua, mabua ambayo tunayavuna ni vifo.” Alisisitiza.

Aliyasema hayo katika Mkutano wa hadhara alioufanya katika  kijiji cha Namasinzi, Kata ya Kapenta, Wilayani Sumbawanga, kijiji ambacho wananchi watatu wamefariki kwa ugonjwa wa kipindupindu na wengine wakiendelea kupatiwa huduma. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa hlamshauri ya Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Fani Musa aliendelea kuishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka misaada katika bonde hilo ili kuhakikisha wanakabiliana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa wataendelea kutoa elimu bila ya kuchoka akiamini kuwa wananchi hao wataelewa wakiendelea kusimamiwa.

“Serikali imekuwa ikifanya kazi tatu kwa wakati mmoja, tumekuwa tukitoa elimu ya ugonjwa huu kwa lengo la kuzuia haya yasitokee, lakini yakitokea tunatumia nguvu kubwa ya kukabiliana na tatizo hili lakini pia serikali inatoa dawa za kutosha ili kuweza kuponya pia, ugonjwa wa kipindupindu ni kitendo cha kula kinyesi ambacho ni kibichi, hivyo watu ni muhimu kujenga vyoo salama,” Alimalizia.

Tangu kulipuka kwa ugonjwa huo tarehe 6 Mei, 2018 watu 14 wameshafariki na wengine 221 wakiendelea na kupatiwa matibabu katika kambi za wagonjwa hao katika bonde la ziwa Rukwa, Wilayani Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili toka kushoto) akiwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (wa kwanza kushoto pamoja na timu ya afya ya wilaya na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakikagua vyoo katika Kijiji cha Namasinzi, Kata ya kapenta, Wilayani Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akikabidhi tenki la lita 5000 kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Liweliyamvula, Kijiji cha Lumbesa, Kata ya Kapenta, Wilayani Sumbawanga Paulo Maufi, ikiwa ni miongoni mwa juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama na kuhifadhiwa sehemu salama, kuepukana na kipindupindu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akikabidhi dawa za “Water guard” kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Liweliyamvula, Kijiji cha Lumbesa, Kata ya Kapenta, Wilayani Sumbawanga Paulo Maufi, ikiwa ni miongoni mwa juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama, kuepukana na kipindupindu.

DC SANGA ATOA TATHMINI YA AWALI YA MAAFA YA MVUA MKURANGA

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mkuranga ,Juma Abeid akizungumza jambo katika kikao cha baraza la madiwani ,wa kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,Mshamu Munde.

Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkuranga, Filberto Sanga, ametoa tathmini ya awali ya maafa yaliyotokea katika mvua zilizonyesha hivi karibuni ambapo wanafunzi watano wamepoteza maisha kwenye mvua hizo. Aidha ametoa tahadhari kwa watu na watoto kuacha kukatiza katika mito na maeneo hatarishi ili kuepukana na maafa yanayoweza kujitokeza.

Akitoa tathmini hiyo kwa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, Sanga alitaja kata walizopoteza watoto hao kuwa ni Tambani wanafunzi wawili ambao walizama, kata ya Mianzi, Mwarusembe,Mwandege mwanafunzi mmoja mmoja. Alieleza kuwa, pia ipo miundombinu ya barabara ambayo imeharibika vibaya na haipitiki. Sanga alisema ,wakati mvua ikiwa ni neema lakini mazingira yalishindwa kuhimili ,hivyo wamejipanga kuanza kukarabati baadhi ya miundombinu baada ya mvua kukoma. Alifafanua ,tathmini bado inaendelea na watatoa ukubwa wa maafa yaliyotokea baadae.
Diwani viti maalum Mkuranga, Daima Utanga akizungumza jambo wakati wa kikao cha baraza la madiwani wilayani humo .

WAKATI HUO HUO , Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mkuranga wamemtaka afisa elimu msingi wa halmashauri hiyo, kuweka wazi idadi ya shule zilizotumika kiasi cha fedha mil.29. Fedha hizo ni kati ya mil.151 iliyopangwa kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa shule mbalimbali wilayani humo ambapo inadaiwa kutumika mil.29 .

Diwani wa kata ya Mwandege ,Kowero Edward na diwani wa viti maalum Daima Utanga waliibua hoja hiyo, katika kikao cha madiwani kilichofanyika wilayani hapo. Walitaka kujua zilizotumika kwenye ukarabati na ujenzi wa madarasa na shule ngapi kwani taarifa inaonyesha gharama bila idadi ya shule husika, zilizotumika fedha hiyo.

"Tunahitaji majibu ya fedha hizi ,na mchanganuo ili tuweze kujiridhisha" alieleza Daima.

Nae Mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na maji ,Shaban Manda alibainisha ,fedha hizo zimetumika kweli lakini kutokana na suala la idadi ya shule zilipoelekezwa fedha hizo ,watarejea kwenye kamati na kikao kijacho kutaletwa majibu ya uhakika ya hoja hiyo.

Alisema ,afisa elimu msingi wa halmashauri ya Mkuranga ni mgeni ,hivyo kutokana na hilo ,hawezi kuwa na majibu ya moja kwa moja. Manda ,alieleza jumla ya Tsh. mil.151 zimetengwa kwa ajili ya kukarabati na ujenzi ambapo hadi sasa mil.29 pekee.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ,Juma Abeid alisema masuala ya fedha na matumizi yazingatiwe ili kuondoa maswali kwa madiwani. Alisema ,uongozi wowote ni vijiti hivyo hakuna ugeni kwenye ofisi. Abeid aliwataka madiwani wawe na subira ,kuiachia kamati kwenda kukaa ,na kikao kinachofuata watapatiwa majibu ya uhakika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mkuranga, Mshamu Munde alisema wanajivunia kupata hati safi .

"Hati safi hii tuliyoipata sio sifa ya mtu mmoja ,tunajipongeza wote watendaji,mbunge wetu Abdallah Ulega, madiwani na wilaya ";

",Tusiishie hapa tuendelee na jitihada na kufanya kazi kwa kujituma ili kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano" alifafanua Munde.

Aliwaomba watendaji kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi ya wanaMkuranga. Munde alisema ,ushirikiano ndio nguzo pekee katika utendaji kazi hivyo aliwaomba watendaji hao na madiwani kuwa kitu kimoja ili kuleta maendeleo chanja na kuinua uchumi.

MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameutaka uongozi wa wilaya ya Gairo unamsimamia mkandarasi na kuhakikisha upanuzi wa kituo cha afya na unakwisha kwa wakati. 
Akizungumza na uongozi na mkandarasi wakati wa ziara yake mwishoni mwa wiki iliyopita ya kukagua maendeleo ya Wilaya ya Gairo, Mhe. Kebwe amesema kuwa hajaridhishwa na kasi wanayokwenda nayo katika upanuzi wa kituo cha afya unaofanyika hivi sasa licha ya kuwa fedha za kituo hizo zote zimeshatolewa.
 "Ni nini kinakwamisha ujenzi kuisha wakati fedha mmeshapewa???? amemuuliza Mkandarasi na Uongozi unaosimamia jengo hilo ... nawaomba sana, hebu fanyeni haraka maana kuna baadhi ya huduma wananchi wanakwenda kuzipatia mbali," amesema. 
Amesema kuwa ipo haja ya kila mtu kutimiza majukumu yake bila ya kusukumwa sukumwa maana hali ya sasa ni kazi tu. Awali akitoa maelezo ya ujenzi, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba amesema kuwa ujenzi huo umeshagharimu zaidi ya milioni 139 na baada ya kukamilika jumla ya wananchi wapatao 218,000 wataweza kupatiwa huduma huku vipimo vyote vikipatikana. 
"Kituo hiki cha afya kitakuwa ni cha kisasa na kitakuwa na vipimo vyote huku huduma zote zikipatikana maana kimekaa pembezoni mwa barabara ya Gairo-Dodoma," amesema. 
Upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe kwa kuweza kutembelea wilaya yao na kuhamasisha wananchi kuendelea kujitoa katika shughuli za maendeleo. 
Mhe. Mchembe amewashukuru wananchi kwa kuendelea kujitolea katika shughuli za maendeleo ya wilaya yao na kuwaomba kuwa bega kwa bega kuwafichua wale wote wanaokwamisha shughuli za maendeleo.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (aliyeshika tofali na mwiko) na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (wa kwanza kulia) wakishirikiana kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (aliyebeba tofali) kumsaidia fundi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akikagua ujenzi kwa ajili ya kupanua eneo la kulaza, na sehemu ya kuhifadhia maiti wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (wa kwanza kushoto) wakati akikagua upanuzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba (wa kwanza kulia) wakati akitoa maelezo juu ya upanuzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakiangalia mchanganyo wa saruji na mchanga.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) akipima ukuta kuona kama wamefikia viwango vinavyotakiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba (wa kwanza kulia) wakati akitoa maelezo juu ya ujenzi wa jengo ya kuhifadhi maiti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakiwa mbele ya jengo jipya la kuhifadhi maiti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakikagua kijengo kidogo kilichokuwa kikitumika miaka ya nyuma kuhifadhia maiti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakiwa mbele ya jengo la zamani la kuhifadhi maiti. 

Tuesday, May 29, 2018

Tanzania itaendelea kushiriki katika ulinzi wa amani duniani, Balozi Mahiga


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika maadhimisho ya miaka 70 ya Siku ya Walinda Amani Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vya Mnanzi Mmoja Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Mei 2018. 

Siku ya Walinda Amani Duniani huadhimishwa tarehe 29 Mei ya kila mwaka ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa: Miaka 70 ya huduma na kujitoa (UN Peacekeeping: 70 Years of Service and Sacrifice).

Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Mahiga alieleza kuwa yapata miaka 12 tangu Tanzania ianze kushiriki katika ulinzi wa amani chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. 

Pia akasisitiza Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia kupatikana kwa amani katika mataifa mengine kwakuwa hakuna taifa linaloweza kufanikiwa katika maendeleo pasipo kuwepo na amani ya uhakika. " Sio jambo rahisi kukubali kutoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine lakini Tanzania itaendelea kuungana na mataifa mengine duniani katika kusaidia kupatikana kwa amani ya mataifa hayo" alisema Mhe. Mahiga.

Aidha, Katika kuwakumbuka Walinda Amani wote Duniani waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao, pamoja na kutoa heshima kwa wale ambao bado wanaendelea na jukumu la kulinda amani, Tanzania imepoteza jumla ya askari wapatao 30 ndani ya miaka 10, pia dunia imepoteza zaidi ya askari 3500 na kwa sasa Tanzania inajivunia kuwa na jumla ya askari wapatao 2,600 wanaohudumu katika misheni sita (6) za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Walinda Amani Duniani ambapo alieleza pamoja na kuendelea kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo, Umoja wa Mataifa utaendelea kuhakikisha Dunia inakuwa mahali salama pa kuishi ili kuweza kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu. 
Mhe. Waziri Mahiga akiweka shada la maua katika Mnara wa Mashujaa uliopo Viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa Walinda Amani Duniani. 
Wakitoa heshima kwa ajili ya kuwakumbuka Walinda Amani, waliosimama mbele kutoka kushoto ni Mhe. Waziri Mahiga akiwa na Mwakilishi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Maj. Gen. Henry Kamunde, Bw. Alvaro Rodriguez na Mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Nsato Marijani. 
Mhe.Waziri Mahiga akisalimiana na Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. 

Mhe. Waziri Mahiga akisalimiana na sehemu nyingine ya Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. 
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Deusdedit Kaganda pamoja na askari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi Tanzania wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi. 
Sehemu nyingine ya Askari na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi. 
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo. 
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo. 
Waheshimiwa Mabalozi na Wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Walinda Amani Duniani. 
Gwaride la heshima kwa Mgeni Rasmi. 
Askari wa JWTZ wakiingia viwanja vya Mnazi Mmoja. 

OFISA UTUMISHI TRA AIELEZEA MAHAKAMA KUWA MALI ALIZOJAZA MSHTAKIWA NI ZA FAMILIA NA ZINA UMILIKI WA NUSU KWA NUSU

Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

OFISA Utumishi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Evans Emil (53) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mali ambazo alijaza mshtakiwa Jenifa Mushi kwenye fomu za rasirimali na madeni ni za familia ambapo amedai mali nyingi zilizojazwa kwenye fomu hizo, zina umiliki wa nusu kwa nusu mshtakiwa na mkewe na watoto wao.

Evans ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka amedai hayo wakati akitoa ushahidi katika kesi inayomkabili, Aisa Msaidizi wa Forodha Wa  (TRA), Jennifer Mushi ya  kukutwa akimiliki magari 19 mali ambayo hailingani na kipato chake,

Akitoa ushahidi wake leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Shaidi huyo alidai, yeye aliajiliwa TRA mwaka 1996 akiwa na majukumu ya kushughulikia ajira, kusimamia nidhamu, maslahi ya wafanyakazi, utawala na majukumu mengine atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

Alidai taratibu moja wapo kwa mtu ambaye atakuwa ameajiriwa na kuthibitishwa pamoja na mambo mengine anatakiwa kujaza fomu ya tamko ya rasilimari na madeni  ambazo anatakiwa kuijaza kila mwaka wa kalenda na isizidi ndani ya miezi mitatu.

Alidai,  fomu hizo ujazwa chini ya sheria ya maadili ya viongozi wa umma na kanuni ya utumishi ya TRA pale mtumishi anapoajiriwa na kuripoti kazini.

Amedai, lengo kubwa la kujaza fomu hiyo ni kujua mali na madeni ya mfanyakazi na kufahamu uadilifu wa mtumishi, kutokana na mazingira ya kazi ya TRA ikiwa ni kudhibiti vitendo vya rushwa na kujilimbikizia mali.

Alidai anamfahamu Jeniffer kama Ofisa Forodha Msaidizi wa TRA  tangu mwaka 2010 ambapo alikuwa akifanya kazi ya kuthaminisha bidhaa zinazoingia na kutoka nje ya nchi.

Alidai mwanzo aliajiriwa TRA kwa mkataba wa miezi mitatu mitatu kuanzia Januari Mosi, 2011 mpaka Machi 2011 baada ya hapo Juni 30 mwaka 2011 aliongezewa mkataba na Julai Mosi mwaka huo huo, alipatiwa mkataba wa kudumu ambapo alijazaa fomu mbalimbali  ikiwamo fomu ya Tamko ya Rasilimali na madeni.

Alidai, mwaka 2016 Mkuu wake wa kazi alimuelekeza kuwa kulikuwa na uchunguzi unaendelea kuhusiana na fomu ya tamko ya rasilimari na madeni ya Jeniffer ambayo  haikuwa sawa na kumtaka awapatie Takukuru na kufanya hivyo.

Alidai katika mkataba wa kidumu ilionyesha anaajiriwa na mshahara wake ulikuwa Sh 800,000 ambapo ungekuwa ukiongezeka hadi milioni 2.

Shahidi Evans aliisoma fomu ya tamko ya rasilimari ya Machi 30/2012 ambayo inaonyesha Jeniffer alieleza kuwa anamiliki Sh. 600,000, zilizopo katika benki na taasisi za fedha Sh 800,000.

Alikuwa na Hisa na gawio la thamani ya Sh 600,000. Pia alikiwa na nyumba kinyerezi  kichangani yenye thamani ya milioni 30  ambayo yeye mshtakiwa alikuwa akimiliki kwa asilimia 50 na mumewe asilimia 50.

Aidha Shamba la heka moja eneo la Mabwepande lenye thamani ya sh. 700,000 umiliki wake yeye asilimia 50 mumewe asilimia 50. Pia Kiwanja heka moja kipo kigamboni chenye thamani ya Sh. Milioni 9 milioni ambapo umiliki wake wake ni asilimia 50 yeye na mume wake 50.
 Mali zingine ni gari aina ya Van,  yenye thamani ya Sh milioni 8 umiliki wake mke asilimia 50 mume asilimia 50. Pia katika upande wa madeni alikuwa na deni la bodi ya mikopo ya vyuo vikuu.

Katika fomu ya tamko ya rasilimali na madeni ya Februari 20/ 2013 Jeniffer alijaza alikuwa na fedha taslimu Sh 800,000 Kiwanja fedha zilizopo katika benki na taasisi za fedha Sh 1,040,000, nyumba kinyerezi yenye thamani ya Sh 35milioni, umilikiwake mke asilimia 50 mume asilimia 50.

Pia alijaza kuwa na kiwanja eneo la Bunju chenye thamani ya Sh milioni 1.7 ambacho mmliki wake ni yeye,  Kiwanja kilichopo Kigamboni chenye thamani ya Sh milioni 9 wamiliki watoto.


Magari  RV 4 lenye thamani ya Sh  milion 8,  RV 4 lenye thamani ya Sh, milioni 13 umiliki wake asilimia 50 mke na asilimia 50 mume. Pia anadeni la bodi ya mikopo ya vyuo vikuu.

Katika fomu ya tamko ya rasilimari na madeni ya Desemba 11/ 2015 inaonyesha Jeniffer anafedha taslimu Sh 550,000, fedha zilizopo benki na katika taasisi za fedha Sh milioni 2.7

Kiwanja Kigamboni cha sh. Milioni 9 umiliki wake wake asilimia 50 mume asilimia 50, magari Toyota la Sh milioni 18 na Toyota ya Sh  milioni 14


Deni  la saccos ya TRA la Sh 6, 168,513 na deni la  mkopo Wa bodi ya mikopo ya vyuo vikuu la Sh 1.5 milioni. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 6 mwaka 2018

Katika kesi hiyo mshtakiwa Jenifer alikutwa akimili magari 19.


yakiwa na thamani ya Sh 197,601,207 Mali ambayo hailingani na kipato chake halali, pia alikutwa akiishi maisha ya kifahari  yenye thamani ya Sh 333,255,556.24 fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali.

VIJANA 966 WAHITIMU MAFUNZO YA KIJESHI MLALE JKT

 Mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa(Jkt)Kanal Hassan Mabena kulia akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika kikosi cha 842 Kj Mlale jana wakati mkuu wa mkoa alipkwenda kwa ajili ya kufunga mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali kwa vijana 966 Operesheni Mererani.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiangalia Tikiti maji katika Bustani ya kikosi cha 842 Kj Mlale JKT mkoani Ruvuma alipokwenda kwa ajili ya kufunga mafunzo   ya vijana Operesheni Mererani jana.
 Mkuu wa kikosi cha 842 Kj Mlale Jkt Luteni Kanali Absolomon Shausi akimuonesha  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma sehemu ya  Shamba la Mahindi  ya chakula yanayolimwa  na vijana  wa jeshi la kujenga Taifa katika kikosi hicho.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akitoa kitambaa kama Ishara ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la mradi wa ufugaji Kuku katika kikosi cha 842 Kj Mlale mkoani Ruvuma,anayemsaidia  kuondoa kitambaa ni mkuu wa kikosi  hicho    Lutewn Kanali Absolomon Shausi.
 Baadhi ya vijana wa  Jeshi la kujenga Taifa Operesheni Mererani 2018 waliopo katika kikosi cha 842 Kj Mlale wakionesha umahiri wa kuvuka vikwazo.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akikagua Gwaride maalum la vijana wa kujitolea waliomaliza mafunzo ya miezi minne ya kijeshi katika kikosi cha 842 Kj Mlale wilayani Songea ambapo jumla ya vijana 966 walimaliza mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali katika kikosi hicho.
 Baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali katika kikosi cha 842 Kj Mlale Operesheni Mererani wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme(hayupo pichani)wakati wa kuhitimu mafunzo yao ya miezi minne katika kikosi hicho.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiongea na vijana,wazazi,Askari na maafisa mbalimbali wa jeshi la kujenga Taifa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika kikosi cha 842 wakati wa kufunga mafunzo ya miezi minne ya kijeshi na Ujasiriamali kwa vijana 966 waliohitimu mafunzo yao jana,kushoto kwake ni mkuu wa kikosi cha 842 Kj Mlale Luten Kanal Absomlomon Shausi.
Picha na Muhidin Amri

TPA TANGA YAJIVUNIA KASI YA UTOAJI HUDUMA

 MENEJA wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama kulia akimueleza Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Charles Mwijage  mipango ya bandari hiyo na namna walivyoboresha huduma zao kwa wafanyabiashara wanayoitumia
 Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Charles Mwijage akisalimia na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga alipokwenda kufungua maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kushoto akisisitiza jambo kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya kufungua maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella

MENEJA wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama amesema wanajivunia kuboreshwa huduma zao kwa kiwango kikubwa ikiwemo uandaaji wa nyaraka kwa kasi na usalama wa kutosha kwa wateja na hivyo kutumia muda mfupi kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja.

Salama aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya kimataifa ya sita ya biashara ambapo alisema kutokana na hali hiyo hakuna sehemu ambayo mteja anaweza kupita akikwama bila wao kujua mara kila hatua wanazokuwa wakipitia wanatambua mara moja.

Alisema kuwa sehemu ambazo mteja anaingia kwenye bandari hiyo anapata taarifa moja kwa moja hiyo ikiwa wanakumbana na vikwazo vya namna yoyote zikijitokeza inawawia rahisi kuweza kuona na kuvishughulia kwa muda mfupi ili kuweza kuondoa usumbufu ambazo unaweza kuwakabili wafanyabiashara.

“Kwa kweli huduma za bandari ya Tanga tumeziboresha kwa kiasi kikubwa kutokana na kasi ya uandaaji wa nyaraka lakini hata usalama wa kutosha kwa wateja ambao wamekuwa wakiitumia hali iliyofanya kutumia muda mfupi kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja “Alisema.

Akizungumzia ujenzi wa gati,Meneja Salama alisema gati hilo litakalokuwa la usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga hakutakuwa na uchimbaji eneo hilo kwani lina kina zaidi ya mita 20 linajisholeza na meli zinazotarajiwa kubeba tani laki moja hadi laki mbili na nusu kuingia na kufanya upakuaji.

“Sehemu ambayo serikali na TPA inataka kuchimba eneo ambalo kuna gati ya sasa kwa muda wa miaka 129 wanahudumia meli nangani kwani wanaona msingi wake uwezo wa Bandari ya Tanga ni shehena 750,000 lakini mwaka 2016 Bandari hiyo ilizidi kiwango cha uhudumiaji na kufikia tani 843,000 hivyo kutokana na matokeo hayo wakaona ipo haja ya kuboresha Bandari hii”Alisema.

Alisema mwaka Agosti 8 mwaka jana Rais Dkt John Magufuli akiwa mkoani Tanga alitoa maagizo kuwa anataka bandari ya Tanga inayohudumia mizigo sasa ichimbwe na meli zifike kwenye gati ambapo wao tayari wamekwisha kuanza utekelezaji wa agizo hilo.

Meneja huyo alisema wameanza kutekeleza maagizo hayo tayari mkandarasi wa BICO ameingia kazini na amesaini mkataba wa miezi minne kuanza kufanya kazi ya utafiti kwenye eneo la sasa la Bandari ili kujua chini ya bahari kuna udongo wa namna gani ili hatua nyengine ya kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi na ushauri zifanyike.

Monday, May 28, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AWAANDALIA FUTARI WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally akiswalisha viongozi na waalikwa mbalimbali swala ya Magharibi kabla ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheik Aboubakary Zubeiry Ally  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wageni wake wakiingia ukumbinini kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek akipakua futari akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed bin Mansour al Malik Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Mawaziri Wakuu Wastaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Sinde Warioba na waalikwa wengine wakichukua futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na wageni mbalimbali kuchukua futari aliyowaandalia 
Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018  
 Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akiwa na Jaji Mkuu Profesa Inbrahim Juma na  Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe wakichukua futari

 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) akifuatiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro, Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (wa pili kulia) na wageni wengine wakichukua futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018   
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Janeth Magufuri, Mama Mary Majaliwa, Mama Anna Mkapa na Mama Khadija Mwinyi wakiongea baada ya kupata  futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018  
 Kamishna  Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akiwa na Mama Evelyn Warioba wakiwa katika futari hiyo
 Waalimwa wakibadilishana mawazo baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubery mara baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa masuala ya Dini kutoka Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na  Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula kwenye futari aliyoandaa
Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa amekaa  na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wa pili kutoka kulia, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na viongozi na wageni mbalimbali walioshiriki Futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi walioshiriki katika futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Janeth Magufuri, Mama Mary Majaliwa, Mama Anna Mkapa na Mama Khadija Mwinyi wakati wa  futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018  
   Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais Dkt, Magufuli baada ya futari
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa pamoja na viongozi na waalikwa wengine wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais Dkt, Magufuli baada ya futari
Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa hotuba  Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek bada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa hotuba  Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek bada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wageni wake baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wageni wake baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wageni wake baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt Mohamed Ghalib Bilali baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana ujumbe kutoka Saudi Arabia mara baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangwalla baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na IGP Simon Sirro baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na vingozi mbalimbali baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana wakitoka ukumbini baada ya futari.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek na  Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed bin Mansour al Malik baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinsi Jenerali Venance Mabeyo baada ya futari
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangwalla akiongea na wakuu wa wilaya za Kinondoni, Mhe. Ally Hapi, Temeke Mhe. Felix Lyaniva na wa Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa baada ya kufuturu
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum baada ya futari
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim. Nyuma yake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba baada ya kufuturu
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na IGP Simon Sirro  baada ya kufuturu
 Katibu Mkuu wa CCM mstaafu Ndg. Abdulrahman Kinana akiongea na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa na IGP Simon Sirro
 Mawaziri wakuu wastaafu Dkt. Salim Ahmed Salim na Jaji Joseph Sinde Warioba na wake zao Mama Evelyn Warioba na Mama Amne Salim
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameongozana na Mama Janeth Magufuli na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na IGP Simon Sirro
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mstaafu Ndg. Abdulrahman Kinana
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt.  Mohamed Ghalib Bilali
 Mama Janeth Magufuli akiwa na Mama Mary Majaliwa na Mama Asha Bilali na Mama Zakia Bilali
 Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula
 Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
 Mama Janeth Magufuli akiongea na Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Ndg. Abdulrahman Kinana
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Shehe Mkuu wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Amne Salim 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulsiha Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma  kwa Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi mbalimbali baada ya futari  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.  Zuberi Ali Maulid baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018.
Picha na IKULU