Saturday, December 31, 2016

MBUNGE WA MKURANGA AOMBA RAIS MAGUFULI KUFUTA HATIMILIKI YA SHAMBA LENYE HEKARI 2472 LINALODAIWA KUMILIKIWA NA WAWEKEZAJI

MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga Mkoani Pwani, Abdallah Ulega amemuomba Rais Dkt. John Magufuli kufuta hatimiliki ya shamba lenye hekari 2472 linalodaiwa kumilikiwa na wawekezaji wenye asili ya Kiasia baada ya wawekezaji hao kushindwa kuliendeleza kwa muda mrefu na badala yake wapewe wananchi.
Hayo ameyasema leo jimboni humo wakati wa mkutano kati ya wananchi na kamati ya usalama ya wilaya hiyo uliokuwa na lengo la kujadili shamba hilo linaloonekana kutishia usalama wa raia pamoja na mali zao.
Alisema shamba hilo lilitelekezwa kwa kipindi kirefu na wawekezaji hao, hali iliyopelekea wakazi wa kata ya Tambani pamoja na Mipeko kuyaendeleza kwa kufanya ujenzi na shughuli mbalimbali za maendeleo.
Ulega alisema Wakazi wa maeneo hayo waliweza kutafuta hati miliki ya maeneo waliyokuwa wanamiliki kwa kipindi chote na kushangazwa na kitendo cha wamiliki hao kuwataka kutoka katika maeneo yao kwa madai kuwa wakazi takribani 45,000 wamevamia eneo hilo.
Alidai wananchi wa vijiji vya Mlamleni, Luzando, Mwanambaya pamoja na Mipeko wamekuwa katika hali ya taharuki toka walipopewa notisi ya siku 21 ya kuwataka waondoke katika maeneo hayo ambayo wameyaendeleza kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

"Mi najua Rais wetu ni msikivu na anaweza kuzifanyia kazi kero za wananchi kwa wakati, na kero hii ya kwenye hivi vijiji vyetu anapaswa kutilia mkazo kwa sababu wananchi wa vijiji hivi wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi na hata kujadili shughuli za maendeleo kwa sasa hakuna kabisa kwa kuogopa hawa watu wawili wanaotaka kutudhurumu haki zet," alisema Ulega.

Aliongeza anaamini kuwa Rais sio kabaila na kamwe hatoweza kukaa upande wa makabaila ambao wanategemea kuwalalia wananchi na kujiingizia pesa kupitia wao.

Hata hivyo Ulega alimueleza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga kumuagiza Ofisa Ardhi wa wilaya hiyo kumuandikia notisi ya siku 90 ili kueleza wapi hilo shamba lililo na ni kwa nini hawakuliendeleza kwa muda wote huo.

Pia alimueleza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kutoruhusu kampuni ya 'Ardhi Plan' kupima maeneo ya wilaya hiyo kwani kama ataruhusu kampuni hiyo kufanya upimaji watapelekea kutokea kwa vurugu ambazo zinaweza kusababisha hali ya amani na utulivu kutokuwepo katika wilaya hiyo.

Kwa Upande wake Mkuu wa wilaya hiyo ya Mkuranga, Philberto Sanga aliwataka wakazi wa vijiji hivyo kukaa vikao vya kutayarisha mihutasari ya kuipeleka katika ngazi za juu ili Rais kufuta hati ya maeneo hayo ambayo yamekuwa msaada kwa wananchi hao kwa muda mrefu.

Alisema Viongozi wa vijiji hivyo wanapaswa kuhakikisha shughuli zote za upimaji ardhi katika vijiji hivyo vilivyodaiwa kumilikiwa na wamiliki hao wa kiasia zinasitishwa mpaka pale taratibu mbalimbali zitakapokamilishwa.

Aliongeza kuwa hatokubali kuona ardhi hiyo ikimilikiwa na watu wawili wenye kutumia fedha na badala yake atahakikisha haki inapatikana kwa wananchi hao kwa kupata ardhi yao.

Sanga alisema viongozi wa vijiji hivyo wanapaswa kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayeweza kufanya maamuzi ya aina yoyote katika vijiji hivyo pasipo kupata ruhusa na kibali kutoka katika ofisi za Serikali.
Mbunge Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Mwanambaya, Luzando, Mipeko na Mlamleni juu ya kumuomba Rais Dkt. John Magufuli kufuta hatimiliki ya shamba lenye hekari 2472 linalodaiwa kumilikiwa na wawekezaji wenye asili ya Kiasia baada ya wawekezaji hao kushindwa kuliendeleza kwa muda mrefu na badala yake wapewe wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filberto Hassan Sanga wapili kutoka kushoto akiwasili katika mkutano uliofanyika leo mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Msham Munde akizungumza na wananchi wa Mwanambaya, Luzando, Mipeko na Mlamleni katika mkutano uliofanyika leo mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid akizungumza na wananchi wa Mwanambaya, Luzando, Mipeko na Mlamleni katika mkutano uliofanyika leo mkoani Pwani.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Salum Ally Papen akifafanua jambo kwenye mkutano uliofanyika leo mkoani Pwani. 
Baadhi ya wananchi wa Mwanambaya,Luzando,Mipeko na Mlamleni wakimsikiliza Mbunge Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega, Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Mamia ya wananchi  katika mkutano huo uliofanyika leo mkoani Pwani. 
Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

KAIMU KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AWAASA MAOFISA MAGEREZA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA UFANISI


Na Lucas Mboje
KAIMU Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa (pichani) amewaasa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza  nchini kuzingatia  kuwa utendaji wao wa kazi za kila siku uende sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya tano ili kuleta ufanisi unaotarajiwa.

KAIMU Kamishna Jenerali, Dkt. Malewa ameyasema hayo jana wakati wa Baraza la Kufunga Mwaka 2016 na kuukaribisha Mwaka 2017 lililowahusisha baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani pamoja na Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha, amewataka Maofisa na Askari wa Jeshi hilo kudumisha nidhamu wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kazi  ikiwemo kutekeleza mara moja Amri mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wao wa Jeshi.

"Kila mmoja wenu atimize wajibu wake katika eneo lake la kazi kwa bidii, ari na moyo wa kujituma ili kuliwezesha Jeshi letu kupata ufanisi unaotarajiwa". Alisisitiza Kaimu Jenerali Dkt. Malewa.
Wakati huo huo Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa  pia ametumia fursa hiyo kuelezea baadhi ya mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa Mwaka uliopita 2016 ambapo Jeshi la Magereza limeweza kupata jumla ya leseni 102 za uchimbaji wa madini ya ujenzi kama vile chokaa, mawe, kokoto, mchanga na Murram katika maeneo mbalimbali ya magereza. Pia katika mwaka 2016 Jeshi limeweza kujenga nyumba 129 kwa njia ya kujitolea ambapo nyumba 231 zipo katika hatua mbalimbali ya ukamilishaji. 

Aidha, Ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya askari katika eneo la Gereza Ukonga maandalizi ya ujenzi yanaendelea na ujenzi wa nyumba hizo ni kufuatia ziara ya Rais Magufuli  Novemba 29 mwaka huu  ambapo alipokea taarifa ya uhaba wa nyumba za kuishi askari wa jeshi hilo na akaagiza Jeshi la Magereza lipatiwe Tsh. bilioni 10 haraka ili kupunguza tatizo hilo.

Shirika la Magereza na Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PPF wameingia Makubaliano ya Mkataba wa ubia katika mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha kusakata ngozi pamoja na uwekezaji wa mashine za kisasa za kutengnezea bidhaa za ngozi katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Karanga, Moshi. 

Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga kimepata Ithibati na hivyo kuwa na hadhi ya kuwa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji na mapema mwakani kinatarajia kudahili wanafunzi 30 katika fani ya Taaluma ya Urekebishaji ngazi ya cheti.  
Pamoja na Mafanikio hayo, Kaimu Kamishna Jenerali Dkt. Malewa ameelezea changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi hilo ikiwemo ufinyu wa bajeti, makazi duni ya maofisa na askari, uhaba wa vitendea kazi, ukosefu wa pembejeo pamoja na madeni ya wabuni na watumishi wa jeshi hilo. 

Kuhusu maeneo yatakayopewa kipaumbele kwa Mwaka mpya 2017 ni kuwa Jeshi la Magereza litaendeleza jitihada za kuimarisha na kuongeza uzalishaji kwenye miradi ya uzalishaji wa mazao ya Kilimo na mifugo lengo ikiwa ni kujitosheleza kwenye chakula cha wafungwa, kuhakikisha wafungwa wanafanya kazi za uzalishaji mali kwa kiwango chenye tija badala ya kukaa tu magerezani pia kuendeleza mikakati ya kupunguza msongamano magerezani.
Baraza la kufunga Mwaka na kuukaribisha Mwaka unaofuata ni utamaduni wa siku nyingi ambao unaenziwa na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Magereza ambapo Baraza la aina hii hufanyika kila Mwaka ili Kamishna Jenerali wa Magereza nchini aweze kuongea na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini kupitia Baraza hilo lengo ikiwa ni kufanya tathmini ya yale yaliyojiri katika Jeshi kwa kipindi cha Mwaka unaisha kwa kuzungumzia mafanikio na changamoto zilizojitokeza na  kutazama matarajio ya Mwaka mpya.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 31, 2016




NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHANDISI RAMO MAKANI AUNDA KAMATI YA KUSULUHISHA MGOGORO WA MUDA MREFU WA PORI TENGEFU LA LOLIONDO, ATOA UFAFANUZI WA TAARIFA ZA FARU JOHN


NA HAMZA TEMBA -WMU.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani amesema hakuna mamlaka nyingine ya Serikali chini ya ofisi ya waziri mkuu yenye mamlaka ya kutoa tamko au ufafanuzi kuhusiana na Faru John kwa sasa kwakua jambo hilo bado lipo kwenye uchunguzi.

Amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika tarafa ya Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mbili wialayani humo kwa ajili ya kufuatilia changamoto za uhifadhi pamoja na utekelezaji wa maagizo wa Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Arusha.

Amesema miongoni mwa maagizo aliyoyatoa Waziri Mkuu katika ziara hiyo ni kuwasilishwa kwa taarifa ya inayoelezea utaratibu uliotumika kumuhamisha Faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti pamoja na kuwasilishwa kwa pembe zake ambapo baadae aliunda tume ya kuthibitisha ukweli wa taarifa hiyo.
.
"Ripoti hii ya uchunguzi ni mali ya Waziri Mkuu atakayeweza kutoa ripoti hii nje kwa ajili ya matumizi  ya kila mmoja wetu ni Waziri Mkuu, kwa maana ya mamlaka, kwa hiyo hakuna mamlaka nyingine yeyote ya Serikali chini ya Waziri Mkuu yenye uhalali wa kutoa tamko au ufafanuzi wa jambo hili, mpaka pale Waziri Mkuu atakapokamilisha kusoma ripoti kwa kina kwa kutumia wataalam wake, kufanya vipimo kama ambavyo tunasikia amevipeleka kwa mkemia mkuu wa Serikali, pamoja na udadavuzi wa ripoti.

"Kwa kipindi hiki nnapozungumza, zaidi ya kwamba tunasubiri maagizo au maelekezo au muelekeo sasa juu ya jambo hili kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, hakuna jambo jingine ambalo Wizara inaweza kufanya wala kusema kuhusiana na suala la Faru John, hatuna mamlaka hiyo", amesema.

Akizungumzia tukio la hivi karibuni la baadhi ya watumishi wa wizara kuonekana kwenye chombo kimoja cha habari wakitoa ufafanuzi juu ya jambo hilo amesema "Mimi kwa sasa nnachoweza kusema kwa chochote kilichofanyika kama kuna utaratibu umetumika kuwafanya waweze kwenda mbele ya vyombo vya habari, kwenda kutoa taarifa hizo, lakini pia tukijua kabisa kwamba wao sio wasemaji wa wizara na wala kwa level  (hatua) ya jambo lenyewe pale lilipofikia wao hawana mamlaka ya kuweza kutosha kulizungumzia jambo hilo, sasa kwanini limekua hivo jana ni jambo ambalo tunalifanyia kazi, bila shaka walipoitwa pengine hawakuambiwa sawasawa wanaenda kuzungumzia nini",.

"Kama wizara tutachukua sasa muda wa kuweza kuzungumza nao tujue nini kilitokea lakini kimsingi baada ya hiki nnachokisema hapa sasahivi ieleweke hivo na taifa zima kwa ujumla kuwa hakuna tunachoweza kusema sasa hakuna tunachoweza kufanya sasa mpaka uchunguzi unaofanyika chini ya ofisi ya waziri mkuu ukamilike mpaka waziri mkuu asome aridhike na taarifa yetu na aweze kuina taarifa ile inafaa kwa namna gani na kama kuna maagizo mengine atayatoa baada ya hatua hiyo.

Wakati huo huo ametoa wito kwa wananchi kuwa na subira juu ya taarifa sahihi za faru John "Unaweza kusikiliza habari kutoka vyanzo vingi tu, lakini ukishapata habari usiifanyie kazi haraka haraka bila ya kujiridhisha juu ya ubora wa taarifa unayoipata, wawe na subira, wananchi waendelee kusubiri, si waliapata taarifa ya faru John kupitia kwa Waziri Mkuu?, busara ya kawaida inasema kwamba wangesubiri kutoka kwa Waziri Mkuu au mtu atakayekasimiwa madaraka na Waziri Mkuu atasema kitu kingine kinachofuatia baada ya pale na si vinginevyo".

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Makani ameunda kamati maalum ya kuushulikia mgogoro wa muda mrefu katika  pori tengefu la Loliondo baina ya wananchi, wawekezaji na hifadhi hiyo. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya waziri mkuu ya kuwakutanisha wadau katika eneo hilo kumaliza mgogoro huo.

Kamati hiyo imehusisha taasisi za serikali, asasi za kiraia, viongozi wa dini, wazee wa kimila (Leigwanan), viongozi wa vijiji, wajumbe wa kamati teule za vijiji, wawakilishi wa wanawake na vijana. Ameunda pia kamati ya kuandaa kanuni za kundesha vikao  vya kamati hiyo.

"Kuna watu humu ndani na hata nje ambao hawataki tumalize migogoro Loliondo, nitoe rai kwao, waache chokochoko. Wananchi muone umuhimu wa jitihada za Serikali kumaliza changamoto hii na kutuunga mkono", alisema Makani.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza katika kikao cha wadau wanaohusika na mgogoro wa pori tengefu la Loliondo alichokiitisha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana. Kupitia kikao hicho aliunda kamati maalum ya kutatua mgogoro wa muda mrefu wa pori tengefu la Loliondo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mfaume Taka.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza katika kikao hicho.

Baadhi ya wadau wanaohusika na mgogoro wa pori tengefu la Loliondo wakiwa kwenye mkutano huo.

MUSOMA VIJIJINI WAWEKA WAZI MATUMIZI MFUKO WA JIMBO

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo. Kushoto ni wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Tegeruka, Musoma Vijijini waliohudhuria mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo hilo.
Katibu wa Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini na Afisa Mipango wa Wilaya ya Musoma, Mukama Rugina (aliyesimama) akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za mfuko huo.
Diwani wa Kata ya Tegeruka, Benjamin Maheke (aliyesimama) akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini wameagizwa kuhakikisha wanakagua utekelezaji wa miradi ya kilimo ya vikundi vilivyokabidhiwa vifaa kutoka kwenye mfuko huo ili kujiridhisha.

Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati husika wakati wa mkutano wa hadhara wa kuainisha matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo kwa Awamu ya Pili uliofanyika katika kijiji cha Tegeruka, Musoma Vijijini.

Ilielezwa kwamba Awamu ya kwanza ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya Mfuko wa Jimbo hilo ni shilingi milioni 70,820,000 ambazo zilitumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo shilingi milioni 20,000,000 kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Murangi.

Fedha zingine ni milioni 27,500,000 ambazo zilitumika kwa ajili ya kurekebisha nyumba na madarasa yaliyokuwa yameezuliwa na upepo kwa shule mbili za msingi, milioni 22,500,000 ilitumika kununulia mashine za umwagiliaji, mbegu za mbogamboga na matunda pamoja na dawa za kilimo na shilingi 820,000 zilitengwa kwa ajili ya kuwezesha ufuatiliaji.

Profesa Muhongo alisema ni jukumu la Kamati husika kuhakikisha fedha imetumika kwa matumizi yaliyokubaliwa na aliagiza vikundi vyenye miradi ya kilimo ambayo haijaanza vinyang’anywe vifaa vilivyokabidhiwa na vipewe vikundi vingine vyenye vyenye nia dhabiti ya kuendeleza kilomo.

“Tembeleeni hivi vikundi, mkikuta havijaanza kutumia vifaa tulivyowapatia mvinyanga’anye na vifaa hivyo vigawiwe kwenye vikundi vyenye nia ya dhati,” aliagiza Profesa Muhongo.Akizungumzia Awamu ya Pili ya Mfuko wa Jimbo, Profesa Muhongo alisema Mfuko wa Jimbo umepokea kiasi cha shilingi milioni 38,479,000 ambazo alisema Kamati husika kwa kushirikiana na wananchi pamoja na madiwani wamependekeza zitumike kwa ajili ya kuboresha kilimo.

Alisema shilingi milioni 16,000,000 zitatumika kwa ajili ya kununulia mbegu za kisasa za mihogo za mkombozi kiasi cha vipando 532,000 ambazo zitagawiwa kwenye Kata 21 kwa ajili ya vijiji 68, na shilingi milioni 21,900,000 itatumika kununulia mashine 21 za kukamulia alizeti. 

Aliongeza kuwa hapo awali alisambaza mbegu za alizeti za majaribio kiasi cha kilo 4000 ambazo alisema zimeonesha mafanikio na hivyo aliongeza mbegu zilizoboreshwa kutoka Arusha kiasi cha kilo 5000 ambazo pia zilisambazwa.

Alisema ili kujiongezea kipato kutokana na kilimo cha alizeti, wameamua badala ya kuuza mbegu, wakulima hao watauza mafuta na ndiyo sababu ya kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya mashine hizo ambazo alizielezea kuwa ni za kuzungusha kwa mikono na hazihitaji mafuta wala umeme.


“Hizi nilitoa fedha yangu na sio katika mfuko wa jimbo; na kukitokea mapungufu nifahamisheni nijazilizie,” alisema.Akizungumzia utaratibu wa mashine hizo, alisema kila Kata itakabidhiwa mashine yake na kwamba zitafungwa kwenye ofisi za kata chini ya usimamizi wa Afisa kilimo.

Friday, December 30, 2016

UFUNGUZI WA MSIKITI FUJONI MZAMBARAUNI WILAYA KASKAZINI "B" UNGUJA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed wakati alipowasili katika ufunguzi wa msikiti, Masjid Muhammad (S.A.W) huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja leo,uliojengwa kwa usimamizi wa Bw,Yakoub Othman mwakilishi wa Kampuni ya Al-Buwardy Tanzania
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Msimamizi wa Ujenzi wa msikiti, Masjid Muhammad (S.A.W) Bw,Yakoub Othman wakati alipowasili katika ufunguzi  wa Msikiti huo  uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria ufunguzi  wa Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja leo (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mhe,Balozi Seif Ali Iddi
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akikata Utepe fkama ni ishara ya  ufunguzi  wa Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa Kaskazini Unguja leo chini ya usimamizi wa Bw,Yakoub Othman (hayupo pichani) pia wakiwepo (kulia} Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman (kushoto)
 Sheikh Othman Maalim alipokuwa akitoa mawaidha baada ya ufunguzi wa  Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa Kaskazini Unguja leo,ambapo umefunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati waliokaa)
 Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Fujoni Mzambarauni na Vijiji jirani wakiwa ndani ya Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W) uliofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ambao umejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Al-Buwardy,chini ya Usimamizi wa Bw,Yakoub Othman mwakilishi wa kampuni hiyo
 Sheikh Abdulkadir Imamu wa Masjid Maamur kutoka Dar es Salaam (mbele) akiwaongoza Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Swala ya Ijumaa baada ya Msikiti Masjid Muhammad (S.A.W) huko Fujoni Mzambarauni uliofuguliwa rasmi leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) ambao  umejengwa kwa ufadhili Kampuni ya Al-Buwardy,chini ya Usimamizi wa Bw,Yakoub Othman mwakilishi wa kampuni hapa Nchini
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa nasaha zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya swala ya Ijumaa leo alipoufungua Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja,uliojengwa chini ya usimamizi wa Bw,Yakoub Othman (hayupo pichani) kwa ufadhili Kampuni ya Al-Buwardy
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Bw.Samir Ayoub miongoni mwa familia ya Msimamizi wa Ujenzi wa msikiti, Masjid Muhammad (S.A.W) Bw,Yakoub Othman wakati alipowasili katika ufunguzi  wa Msikiti huo  uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja leo. Picha na Ikulu.

MBUNGE MUSSA WA JIMBO TANGA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA WAKULIMA JIMBONI KWAKE

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Golani Shutashuta,Saidi Bakari  wakati alipokwenda akikagua mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji eneo la Golani Shutashuta Kata ya Pande Jijini Tanga jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao na changamoto ambazo zinawakabili
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikangalia naamna mradi huo unavyopandwa

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua mradi huo leo mara baada ya kuwasilia kwenye eneo hilo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua hoho wakati alipokuwa akitembelea mradi huo wa kilimo cha Umwagiliaji wa Kikundi cha Golani Shutashuta eneo la Kata ya Pande Jijini Tanga
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua hoho wakati alipokuwa akitembelea mradi huo wa kilimo cha Umwagiliaji wa Kikundi cha Golani Shutashuta eneo la Kata ya Pande Jijini Tanga
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua tikitiki maji wakati alipotembelea mradi wa umwagiliaji leo wa  Kikundi cha Golani Shutashuta eneo la Kata ya Pande Jijini Tanga

Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaji Mussa Mbaruku akipata tunda la tikiti maji mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea kilimo cha Umwagiliaji wa Kikundi cha Golani Shutashuta eneo la Kata ya Pande Jijini Tanga katikani ni mwandishi wa gazeti la tanzania Daima Tanga Mbaruku Yusuph. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.