Tuesday, March 31, 2015

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MILIONI 10 UJENZI WA KANISA LA KKKT USHARIKA WA MATOSA

 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Matosa Kimara jijini Dar es Salaam, Rabisante Lema akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kukabidhi hundi ya sh. milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu ya kanisa hilo wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa. Jumla ya shilingi milioni 50 zilipatikana katika harambee hiyo. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akimkabidhi hundi ya sh. millioni kumi Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Matosa Kimara jijini Dar es Salaam, Mhandisi Simon Kihunzi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kanisa hilo, wakati wa harambee iliyofanyika kanisani hapo, ambapo jumla ya shillingi milioni 50 zilipatikana. 
Godwin Semunyu akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charls Kimei baada ya kutoa mchango wake. Kulia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Rabisante Lema.
Baadhi ya wazee wa kanisa wakiwa katika ibada hiyo.
Dk. Kimei akipiga mnada kikombe kilichoandikwa.
Martin Mmari akinunua kikombe kilichoandikwa jina lake, kikombe alikinunua kwa shilingi milioni moja.
Mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, John Kyaruzi akipokea kikombe baada ya kukinunua kwa shilingi milioni moja katika harambee hiyo.
Ibada ikiendelea.
Waumini.
Waimbaji wa Kwaya Kuu.
Waumini.
Dk. Charle Kimei akiteta jambo na Lucy Naivasha (kulia).
Waumini wakishiriki kuimba nyimbo za injili.
Mchungaji Kiongozi Rabisante Lema akitoa mahubiri.
Dk. Charles Kimei akiteta jambo na Martin Mmari.
Waumini wakiwa katika ibada hiyo.
Dk. Charles Kimei akitoa neno.

Mayai yakisubiri kuuzwa katika harambee hiyo.

Asante kwa mchango wako wa sh. laki tano, Dk. Kimei akimshuru mchangiaji.
Lucy Naivasha akitoa neno la shukrani baada ya kutoa mchango wake.
Lucy Naivasha akipeana mkono na Dk. Charles Kimei.

SAKATA LA ASKOFU GWAJIMA, MAASKOFU KUTINGA KWA IGP LEO KUMUOMBEA MSAMAHA

 Maaskofu na wachungaji wa makanisa ya kipentekosti wakiingia ukumbini katika Hoteli ya Tamari iliyopo Mwenge tayari kwa kutoa tamko lao.
Katibu wa Maaskofu wa makanisa ya Kipentekosti Dk. Damas Mukassa akisoma tamko la maaskofu hao Dar es Salaam jana, kuhusu sakata la kukamatwa kwa Askofu wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima ambalo leo hii wanatarajia kwenda kumuona Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Mangu kuzungumzia suala hilo. Kulia ni Askofu Dk.Mgullu Kilimba na Askofu Mwaviga Mwafululila.
 Askofu Dk. Paul Shemsanga akizungumza katika mkutano huo ambapo maaskofu hao walitoa tamko lao.
 Wachungaji mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wachungaji mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.


 Wanahabari wakisubiri kuchukua taarifa hiyo.
 Baadhi ya maaskofu wakiwa kwenye mkutano huo.

Mpiga picha wa gazeti la Mtanzania, Hamphrey Shao akipiga picha katika mkutano huo.

 Na Dotto Mwaibale

 MAASKOFU wa makanisa mbalimbali ya Kipentekoste nchini wamesema wanatarajia kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ili kulimaliza sakata la Askofu Josephat Gwajima, kwani kuliendeleza ni kuleta mpasuko wa kidini katika jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Maaskofu hao, Askofu Dk. Damas Mukassa alisema hakuna sababu ya jambo hilo kukuzwa, kwani mhusika amemsamehe Askofu Gwajima.

Dk. Mukassa alisema ni vema Serikali na vyombo vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi, kwani yanaweza kusababisha chuki baina yao.

"Tunaomba Serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu, na busara itumike ili kuepusha uvunjifu wa amani katika jamii," alisema Mukassa.

Katibu huyo alisema wanasikitishwa kukamatwa kwa wasaidizi wa Gwajima, kwa kisinginzio kuwa, walitaka kumtorosha, jambo ambalo haliwezekani.

Alisema wamekaa na kutafakari kilichomkuta Askofu Gwajima, kwani kiuhalisia afya yake ilikuwa salama, hivyo wamebaki na shaka, kama vyombo vya usalama si sehemu salama kama zamani.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwajima aliyelazwa katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam amejitokeza hadharani na kusema kuwa, hakuna njama  ya yeye kutoroshwa na wachungaji wake na amekiri kuwa, bastola iliyokutwa katika begi ni yake na anaimiliki kihalali.

Alisema iwapo angekuwa na lengo la kutoroka nchini angeondokea Arusha, ambapo alikuwepo, lakini aliamua kuitikia mwito wa jeshi la Polisi na kurejea Dar es Salaam.

Askofu Gwajima alisema baada ya wachungaji wake kupata taarifa  ya kuwa, amefariki ndipo walikwenda kumwona na kumpelekea silaha hiyo ili aweze kujilinda.

"Kwa kuwa, palikuwa na mpango huo nikawaambia wachungaji wangu waende nyumbani kwangu na kuchukua begi lililokuwa chumbani, ambapo ndani yake palikuwa na baadhi ya nguo na bastola  ninayoimiliki kihalali, kwani humo ndani kulikuwa na nyaraka zilizokuwa zikionesha umiliki na vitu vingine," alisema Gwajima.

Alisema alishangaa kuona Askari wakiwavamia wachungaji wake na  kuwafikisha kituoni kwa kosa la kutaka kumtorosha, jambo ambalo si la kweli.

Gwajima alisema walipofika hospitalini usiku, wachungaji wake walimfikishia begi na kuliweka ndani ya chumba, lakini walitokea watu ambao walijitambulisha kuwa, ni askari na kuomba mzigo ulioingizwa ndani na hapakuwa na ushindani akawapa.

Kuhusu kuzimia kwake, alitoa taarifa ya kusumbuliwa na kichwa kwa muda mrefu bila ya kusikilizwa ili apatiwe huduma, ambapo kilichotokea ndiyo hicho walichokiona.

Gwajima alisema alikuwa akihojiwa na Kamanda wa Upelelezi wa Kanda (ZCO), ambapo aliendelea kumhoji huku akimpa taarifa ya kuumwa kichwa, lakini hakumsikiliza, hivyo mpaka anaanguka na kuzimia hakujua kilichoendelea hadi alipofikishwa hospitalini.

Askofu Gwajima alisema hana mgogoro wowote na Askofu mwenzake na anampenda, kilichotokea alikuwa katika kazi yake ya kukemea aliyoyasema.

Kwa upande, Dk. Willibrod Slaa, mara baada ya kumtembelea Askofu Gwajima hospitalini hapo, alisema haingilii ugomvi wa Askofu Pengo na Gwajima, bali anachokipinga ni upotoshaji unaofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia.

Dk. Slaa alisema polisi waache maneno yao ya kusema mtu anajifanya anaumwa, kwani ni kitendo ambacho kinaonesha kuwa, halithamini utu wa mtu.

Aidha, alisema mambo anayofanyiwa Askofu Gwajima hata yeye aliwahi kufanyiwa akiwa Arusha, baada ya umma kupotoshwa kuwa, alikamatwa na silaha kana kwamba yeye ni jambazi.

“Nilikamatwa na jeshi la polisi huko Arusha, ambapo kisheria unapokuwa na silaha unaisalimisha, nilifanya hivyo na nikaambiwa nijisajili, lakini siku iliyofuata taarifa ikatolewa kuwa, nimekamatwa na silaha, hivyo inaonesha jinsi gani jeshi la polisi linavyofanya hila kwa raia," alisema.

Dk. Slaa alisema mahakama ndiyo itakayotoa ukweli wa jambo hilo kama ilivyotokea katika kesi ya ugaidi dhidi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati fulani.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba alisema kinachoonekana kwa sasa ni ukiukwaji wa haki za binadamu ambao unaendelea kufanywa kwa vyombo vya usalama.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema anatarajia kufanya mazungumzo na Askofu Gwajima kutokana na kauli yake ili kujua nini kilimsukuma kutoa kauli hiyo.

Akizungumzia sakata hilo la kukutwa na silaha na kuendelea kuwashikilia wachungaji na wafuasi wa Gwajima, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema silaha hiyo haimilikiwi kihalali na Gwajima.

Wakati huohuo, Methusela Gwajima ambaye ni Mwanafamilia amekemea vikali kitendo cha kutukanwa kwa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na kwamba ni kinyume cha sheria.

Alisema kitendo hicho ni cha fedheha, ni kinyume cha sheria ya nchi na kwamba, alitakiwa kumfuata na kumweleza na si kumtukana matusi makubwa na kumsababishia aibu kubwa.

Aliongeza, Gwajima abebe msalaba wake mwenyewe kwa kwenda kuomba msamaha, kwani aliamua kumchafua kiongozi huyo wa kiroho, na kwamba itamsaidia kurudisha heshima ya mwanzo aliyokuwa nayo. 

(Imeandaliwa na mtandao www.habari za jamii.com)

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YAFANYA KIKAO CHAKE CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye ni Katibu wa Tume Bi. Agnes Mgeyekwa akitoa hotuba fupi katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi TUMESHERIA.
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la TUMESHERIA Bw. Fredy Kandonga akizungumza katika kikao cha Baraza.
Mwenyekiti wa Tume Mh. Jaji Aloysius Mujulizi akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi.
Katibu wa Kikoa cha Baraza Bi. Marlin Komba akitoa ufafanuzi wakati wa kikao cha Baraza.
Wajumbe wa Baraza wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Baraza.
Wajumbe wa Baraza pamoja na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Tume wakiimba wimbo wa Mshikamano katika kikao cha Baraza la wafanyakazi TUMESHERIA (Picha zote na Munir Shemweta)

NMB NA DSE WAZINDUA SHINDANO LA UWEKEZAJI KWA WANAFUNZI WA VYUO VYA JUU NCHINI

Soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kupitia udhamini wa benki ya NMB imezindua shindano la uwekezaji lijulikanalo kama ‘DSE Scholar Investment Challenge’ linalowahusisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu ambapo washindi wanatarajia kuibuka na kitita cha shilingi milioni 2 na nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo.

Shindano hilo ambalo litadumu kwa miezi mitatu, litawakutanisha wanafunzi wa vyuo vikuu ambao watapewa mitaji ya kielectroniki (Virtual Capital) ya shilingi milioni moja na wao kufanya uwekezaji kwa njia ya kununua hisa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.

Washindi watatu watakaopatikana, watagawana kitita cha shilingi milioni 2 ambapo mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni 1, mshindi wa pili laki 6 na mshindi wa tatu atapata shilingi laki nne. Washindi watapatikana kutokana na faida watayoipata katika uwekezaji wao kwenye soko la hisa na ushiriki wao kwenye majadiriano yanayoonyesha njia walizotumia kufikia faida walizopata. Shindano hili litafanyika kwa njia ya mtandao wa simu.

Hii ni mara ya pili kufanyika kwa shindano hili kuendelea kupata udhamini mzuri kutoka benki ya NMB, Lengo la shindano hili ni kuwahamasisha wanafunzi kujenga utamaduni wa kuwekeza na kutunza akiba katika taasisi za fedha.
Afisa kutoka DSE – Aleck Ngoshani akiwasilisha mada kwa wanafunzi wa CBE wakati wa semina za kuwahamasisha wanafunzi kushiriki shindano la DSE na jinsi watakavyoweza kufanya uwekezaji kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.
Wanafunzi wa chuo cha biashara cha CBE wakisikiliza mada kutoka kwa maafisa wa DSE jinsi ya kushiriki shindano la DSE Scholar Investment Challenge.
Meneja Mradi na Biashara wa soko la hisa la Dar es Salaam – Magabe Maasa akitoa mada juu ya nafasi ya wanafunzi katika uwekezaji.

Global Health catalyst Cancer Summit 2015 at Havard Medical School


Mhe.Liberatus Mulamula

Balozi wa Muungano ya Jamhuri ya Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberatus Mulamula, alipozungumza  katika kongamano  la mapambano dhidi ya gojwa la saratani duniani, aliwataka wanaDiaspora wa nchi za kiAfrika kuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na watalaamu wa vitengo vya afya duniani ili kuboresha upatikana wa huduma za afya barani Afrika. 
Mhe. Balozi Mulamula, ambaye pia ndie aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo alizungumzia faida za kutumia Teknolojia  ili kuboresha mawasiliano kati ya wataalam, utafiti na  elimu . 
Nia mojawapo ya  kongamano la Global Health Catalyst Cancer Summit 2015 ni kuboresha huduma mahiri za saratani barani Afrika kwa  kutumia ( Information and Communication Technologies (ICTs);Teknolojia ya mawasiliano kati ya wataalam wa gojwa la saratani wa nchi za nchi za ng'ambo  na wataalam waliopo barani Afrika.Mhe. Balozi L. Mulamula, alikabidhi Tunzo Maalum kwa Bigwa wa Tiba ya Saraatani Dr. Twalibu Ngoma. Dr.Ngoma ni miongoni mwa wataalam wa kuigwa ambaye amepata elimu ya juu nje ya nchi na kureja nyumbani ili kuboresha upatikanaji wa huduma na elimu ya saratani nchini Tanzania
 Dr.Twalibu Ngoma
Proffesor na Mkuu wa Kituo cha Kliniki ya Mafunzo ya Sarataani kilichopo University ya Muhimbili Dar es salaam nchini Tanzania
       Mhe.Balozi Mulamula na waTanzania wanaDiaspora wakimpongeza Dr.Ngoma kwa furahaa

Uniting Africans in Diaspora (AID)  Against Cancer;
Sehemu ya pili  ya kongamano la Global Health Catalyst cancer  Summit ilijumuisha wanaDiaspora waafrika  ambao ni nguvu kubwa na rasilimali endelevu kwa katika nchi zao za kuzaliwa. Ripoti ya utafiti uliofanywa kwa baadhi ya viongozi wa  USA Afrikan Diaspora imedhihirisha kuwa karibu asilimia 90 % ya wanadiaspora wana nia na malengo ya kuleta mabadiliko katika nyanja mbali mbali nchini mwao ukiwemo uwanja wa afya  barani afrika.
Dr. Doyin Oluwole
      Mkurugenzi wa Taasisi ya Pink Ribbon Red Ribbon, jitihada zilizoanzishwa na   Rais  Mstaafu 
                                                              Mhe. George W. Bush 
Mashirika mbalimbali yalionyesha  mipango ya ujenzi wa vituo vya kutoa tiba ya saratani nchin Tanzania

Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV, Mhe. Iddi Sandaly alieleza nia ya wanaDaspora kuwa mstari wa mbele katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya  nchini Tanzania na malengo ya kupeleka huduma ya afya kwa jamii zenye uhitaji  hivi karibuni.

Mabigwa wa Saaratani mbalimbali duniani wakijadili njia bora  za kuborehsa huduma za saratani.

Ukosefu wa Elimu Afya kwa jamii ni kati ya changamoto zinazopelekea ongezeko la vifo vya gojwa la saratani barani Afrika. Saratani nyingi huweza kutibika endapo zimegundulika mapema na kupata utafiti na huduma sahihi.


Mwanzilishi wa http://www.nesiwangu.com/ ; mtandao unahusika na utoaji wa Elimu Afya kwa lugha ya kiswahili  Bi. harriet Shangarai, alizungumzia faida za kutoa Elimu Afya kwa kutumia lugha ya asilia na  kusema kuwa baadhi ya wasomaji wake walitafuta huduma ya haraka baada kujisomea na  kuelewa dalili  zenye kuashiria hitilafu katika mifumo mbali mbali mwilini. Bi. Harriet alizungumzia faida zitokanazo na Teknolojia ya mawasiliano ambayo ni fursa kubwa kwa Wanadiaspora kutoa mchango wao wa kielimu kwa jamii na kujenga mawasilino ya karibu na wataalam wa afya nchini mwao ili kwa pamoja waweze kushirikiana katika  kuziba  mapengo yaliyomo kwenye uwanja wa huduma na elimu ya afya.

Wataalam wa afya katika diaspora walipata fursa ya kujadili njia mbali mbali zitakazowawezesha kushirikiana  na kupata  fafanuzi za huduma za afya nchini mwao.


        Taasisi binafsi na vyombo mbali mbali vinavyotumika kuboresha huduma za saratani barani Afrika
                                Afrikan Women cancer Awareness association (AWCAA)


Mkurugenzi na Mwanzilishi wa African Women Cancer Awearness association NGO ( AWCAA)
Mrs.Ify Nwobuke (kushoto) na Mwakilishi wa AWCAA (kulia),  walizungumzi huduma za saratini ya matiti  mbazo wamekuwa wakizitoa barani Afrika. Mrs Ify alisema saratani ya matiti yaweza kutibika iwapo imegunduika mapema hivyo elimu kwa jamii ni muhimu katika mapambano ya saratani.

Shukrani;
Waandalizi wa Global Health Catalyst Cancer Summit @ Harvard Medical School, 2015
Kwa maelezo zaidi pitia