Soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kupitia udhamini wa benki ya NMB imezindua shindano la uwekezaji lijulikanalo kama ‘DSE Scholar Investment Challenge’ linalowahusisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu ambapo washindi wanatarajia kuibuka na kitita cha shilingi milioni 2 na nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo.
Shindano hilo ambalo litadumu kwa miezi mitatu, litawakutanisha wanafunzi wa vyuo vikuu ambao watapewa mitaji ya kielectroniki (Virtual Capital) ya shilingi milioni moja na wao kufanya uwekezaji kwa njia ya kununua hisa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.
Washindi watatu watakaopatikana, watagawana kitita cha shilingi milioni 2 ambapo mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni 1, mshindi wa pili laki 6 na mshindi wa tatu atapata shilingi laki nne. Washindi watapatikana kutokana na faida watayoipata katika uwekezaji wao kwenye soko la hisa na ushiriki wao kwenye majadiriano yanayoonyesha njia walizotumia kufikia faida walizopata. Shindano hili litafanyika kwa njia ya mtandao wa simu.
Hii ni mara ya pili kufanyika kwa shindano hili kuendelea kupata udhamini mzuri kutoka benki ya NMB, Lengo la shindano hili ni kuwahamasisha wanafunzi kujenga utamaduni wa kuwekeza na kutunza akiba katika taasisi za fedha.
Afisa kutoka DSE – Aleck Ngoshani akiwasilisha mada kwa wanafunzi wa CBE wakati wa semina za kuwahamasisha wanafunzi kushiriki shindano la DSE na jinsi watakavyoweza kufanya uwekezaji kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.
Wanafunzi wa chuo cha biashara cha CBE wakisikiliza mada kutoka kwa maafisa wa DSE jinsi ya kushiriki shindano la DSE Scholar Investment Challenge.
Meneja Mradi na Biashara wa soko la hisa la Dar es Salaam – Magabe Maasa akitoa mada juu ya nafasi ya wanafunzi katika uwekezaji.
No comments:
Post a Comment