Dr.Twalibu Ngoma Proffesor na Mkuu wa Kituo cha Kliniki ya Mafunzo ya Sarataani kilichopo University ya Muhimbili Dar es salaam nchini Tanzania |
Mhe.Balozi Mulamula na waTanzania wanaDiaspora wakimpongeza Dr.Ngoma kwa furahaa
Uniting Africans in Diaspora (AID) Against Cancer;
Sehemu ya pili ya kongamano la Global Health Catalyst cancer Summit ilijumuisha wanaDiaspora waafrika ambao ni nguvu kubwa na rasilimali endelevu kwa katika nchi zao za kuzaliwa. Ripoti ya utafiti uliofanywa kwa baadhi ya viongozi wa USA Afrikan Diaspora imedhihirisha kuwa karibu asilimia 90 % ya wanadiaspora wana nia na malengo ya kuleta mabadiliko katika nyanja mbali mbali nchini mwao ukiwemo uwanja wa afya barani afrika.
Dr. Doyin Oluwole
Mkurugenzi wa Taasisi ya Pink Ribbon Red Ribbon, jitihada zilizoanzishwa na Rais Mstaafu
Mhe. George W. Bush
|
Mashirika mbalimbali yalionyesha mipango ya ujenzi wa vituo vya kutoa tiba ya saratani nchin Tanzania
Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV, Mhe. Iddi Sandaly alieleza nia ya wanaDaspora kuwa mstari wa mbele katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya nchini Tanzania na malengo ya kupeleka huduma ya afya kwa jamii zenye uhitaji hivi karibuni.
Mabigwa wa Saaratani mbalimbali duniani wakijadili njia bora za kuborehsa huduma za saratani.
Ukosefu wa Elimu Afya kwa jamii ni kati ya changamoto zinazopelekea ongezeko la vifo vya gojwa la saratani barani Afrika. Saratani nyingi huweza kutibika endapo zimegundulika mapema na kupata utafiti na huduma sahihi.
Mwanzilishi wa http://www.nesiwangu.com/ ; mtandao unahusika na utoaji wa Elimu Afya kwa lugha ya kiswahili Bi. harriet Shangarai, alizungumzia faida za kutoa Elimu Afya kwa kutumia lugha ya asilia na kusema kuwa baadhi ya wasomaji wake walitafuta huduma ya haraka baada kujisomea na kuelewa dalili zenye kuashiria hitilafu katika mifumo mbali mbali mwilini. Bi. Harriet alizungumzia faida zitokanazo na Teknolojia ya mawasiliano ambayo ni fursa kubwa kwa Wanadiaspora kutoa mchango wao wa kielimu kwa jamii na kujenga mawasilino ya karibu na wataalam wa afya nchini mwao ili kwa pamoja waweze kushirikiana katika kuziba mapengo yaliyomo kwenye uwanja wa huduma na elimu ya afya.
Wataalam wa afya katika diaspora walipata fursa ya kujadili njia mbali mbali zitakazowawezesha kushirikiana na kupata fafanuzi za huduma za afya nchini mwao.
Taasisi binafsi na vyombo mbali mbali vinavyotumika kuboresha huduma za saratani barani Afrika
Afrikan Women cancer Awareness association (AWCAA)
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa African Women Cancer Awearness association NGO ( AWCAA)
Mrs.Ify Nwobuke (kushoto) na Mwakilishi wa AWCAA (kulia), walizungumzi huduma za saratini ya matiti mbazo wamekuwa wakizitoa barani Afrika. Mrs Ify alisema saratani ya matiti yaweza kutibika iwapo imegunduika mapema hivyo elimu kwa jamii ni muhimu katika mapambano ya saratani.
Shukrani;
Waandalizi wa Global Health Catalyst Cancer Summit @ Harvard Medical School, 2015
Kwa maelezo zaidi pitia
No comments:
Post a Comment